Tetesi: Upi ukwel

zlatan Peter

Member
Aug 23, 2016
58
87
R[8/28, 21:44] ‪+255 764 042 120‬: KAULI YA MBOWE KUAHIRISHA UKUTA

Ndugu waandishi,

Awali ya yote natanguliza shukrani kwa ushirikiano wenu na kwa kazi kubwa mnayoifanya kama mhimili muhimu wa kuendeleza demokrasia katika nchi yetu.

Pili nitumie fursa hii kutoa pole kwa familia za askari Polisi waliopoteza maisha katika uvamizi wa majambazi katika benki ya CRDB, Mungu azilaze mahali pema roho za Askari wetu.

Dhumuni la kuwaiteni hivi leo ni kuzungumza nanyi maamuzi ya kikao cha viongozi wakuu na mgombea wetu wa Urais mwaka jana, Mh. Edward Lowasa, juu ya hali ya kisiasa nchini, mwenendo wa hali ya usalama wa nchi yetu na uhalisia uliopo toka tutangaze operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA).

Tunawashukuru wananchi na wanachama wote kwa hamasa walioionyesha na utayari wao wa kupigania demokrasia ya nchi yetu, wameonyesha kuwa watanzania hawako tayari kuona nchi yetu ikiingia katika utawala wa kidikteta, na hicho ndicho chama chetu kimekuwa kikipigania toka kuanzishwa kwake.

Pili, nyote ni mashahidi kuwa baada ya kutangaza operesheni UKUTA kumekuwa na matamko, vitisho vya maneno na matendo na ukamatwaji hovyo wa viongozi wetu wa ngazi mbalimbali wakiwa katika maandalizi ya operesheni UKUTA, haikuishia hapo, serikali imeamua hadi kuingilia masuala yangu ya kibiashara, yote hii ni kunikatisha tamaa juu ya harakati tunazopigania katika nchi yetu.

Pamoja na hayo yote, sisi kama viongozi ilitulazimu kukaa kikao cha dharura, cha kamati ya viongozi wa juu na wazee ndani ya chama chetu ili kutathmini hali iliyopo na jinsi gani tutaendelea kupigania demokrasia bila kuleta madhara kwa watanzania wenzetu na kuondoa hali ya amani na utulivu iliyodumu nchini kwa miaka mingi.

Mkirejea ushauri alioutoa Mh. Lowasa, mwezi Julai, wakati BAVICHA wakijiandaa kwenda Dodoma kulisaidia jeshi la Polisi kuzuia mkutano wa CCM, alishauri tuahirishe zoezi hilo ili vijana wetu wasije kudhurika na kuumizwa maana tuliona mazoezi makali kule Dodoma kama inavyoendelea sehemu mbalimbali nchini.

Kimsingi UKUTA hadi sasa umefanikiwa katika malengo kwa asilimia 90%, nia yetu ilikuwa kuionyesha dunia kuwa serikali ya awamu ya Tano inatumia mabavu na kutawala bila kujali misingi ya Taifa letu, hasa katika eneo la kuendeleza demokrasia.

Hivyo, katika ari ile ile, iliyotupelekea kuahirisha safari ya BAVICHA kuelekea Dodoma, tunatumia sababu hizohizo kuahirisha maandamano na mikutano hapo Septemba mosi, hatutaki watanzania waumizwe, lakini meseji senti kuwa Rais Magufuli anatawala kidikteta.

Pia tumeamua kuahirisha maandamano na mikutano kupisha siku Jeshi la Wananchi Tanzania litakapokuwa linaadhimisha miaka 52 toka kuundwa kwake.

Tunakusudia kuchukua hatua zaidi ili kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa nchi ya kidemokrasia. Tumeitisha kamati kuu ya dharura ili kujadiliana na kutoka na njia mbadala itayotufanya tufikie malngo bila kuleta madhara, chama chetu hakiko tayari kuona nchi yetu ikiingia kwenye utawala wa kidikteta.

Pamoja na salaam za chama.

Freeman Aikael Mbowe
Mwenyekiti - CHADEMA, Taifa.
[8/28, 21:48] ‪+255 754 711 243‬: TAARIFA

KUHUSU

KINACHODAIWA KUWA KAULI YA MWENYEKITI KUAHIRISHA UKUTA

CHADEMA inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu andiko linalosambazwa mitandaoni likimnukuu Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kuwa ameahirisha Operesheni UKUTA na maandalizi ya Septemba 1.

Tunaomba umma upate taarifa sahihi kuwa Mwenyekiti Mbowe hajafanya mkutano na waandishi wa habari mahali popote pale kuzungumzia kuahirisha Operesheni UKUTA inayoendela nchi nzima wala kuzuia maandalizi ya Septemba 1.

Kupitia taarifa hii, chama kinawataka viongozi, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA na Watanzania wote wazalendo na wapenda haki, kupuuza andiko linalosambazwa mitandaoni .

Msisitizo unaendelea kutolewa kuwa Operesheni UKUTA ambayo imelenga kusimamia utawala unaoheshimu Katiba ya Nchi na kulinda sheria na maandalizi yanaendelea nchi nzima.

Imetolewa na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
[8/28, 21:51] ‪+255 754 711 243‬: BREAKING NEWZ....!

Profesa Ibrahim Haruna Lipumba na wafuasi wake 10 WATIMULIWA RASMI UWANACHAMA WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF). Wengine wapewa onyo kali.

HAYO NI MAAMUZI YA BARAZA KUU LILILOKETI LEO HUKO ZANZIBAR.

KWA TAARIFA ZAIDI FATILIA PRESS CONFERENCE YA CHAMA KESHO SAA 5 ASUBUHI ITAKAYOSOMWA NA MHE. MAZRUI
 
wahairishe tu,,naona kama rais kanywea vile,kama hayupo vile,siku mbili tatu hz,sijazisikia zile kauli zake,
 
Back
Top Bottom