Upi ni ukweli kuhusu bara la Atlantis

Zito utajusumbua bure, hiyo Sumerian hypothesis ni academic propaganda kufunika ukweli wa Africa chanzo cha ustaarabu....na weupe inawafariji sana, lakini chimbuko la Egypt ni mchanganyiko wa Ethiopia na Meroe, Sudan kusini
 
Asante
 
Mawazo maxuri Asante
 
Mtazamo wangu,

Atlantis imetajwa na Plato kwenye Timaeus na Critias. Inaelezwa sababu za kutajwa kwenye hii mijadala ni mawazo ya Socrates juu ya nchi ambayo angependa kuishi. Mawazo ya Socrates ndo yalimpa wazo Plato juu ya aina ya taifa analotaka kuishi kwenye " the republic".
Kazi hizi zote za Plato zilikuwa za kubuni, lakini habari za Atlantis zilikuwepo na kwamba watu waliosafiri kutoka ugiriki kwenda misri walipitia Atlantis.
Story ya Plato inaishia kwa Atlantis kuzamishwa baharini kwakua miungu haikupendezwa nao.
Nionavyo mimi,
Uwepo wa Atlantis ni simulizi na hakuna ukweli, ubatili huu ni kwasababu wakati Plato anatunga hizo simulizi miaka 9000 nyuma yake ndo inasemekana Atlantis ilikuwepo. Mpaka anaandika hakua na ushahidi wowote zaidi ya simulizi tu, hata hivyo dhumuni lake halikua kuielezea Atlantis ilikua sehemu ndogo tu ya maelezo.
Pia "continental drift" na nguvu yake katika ushawishi wa mpangilio wa nchi karne hii unadhihirisha hakukua na ardhi ya ziada popote.
Mimi naona hakuwahi kuwepo na Atlantis na imejipatia umaarufu kutokana na watu kutokumuelewa Plato vizuri.
 
Ila Nimrod alikuwa black mkuu sababu ndio mtoto wa CUSH founder of kingdom of KUSH/ ethiopia..... So tunarudi kulekule ikimaanisha ancient sumerians were semitic-speaking negroids akiwemo Nimrod ama Enmekar kwa kisumeria
Israel walikuwa na operation Nimrod, ni wao huyo?
 
Nashkuru kwa maelezo yako murua nimekusoma kabisa mkuu
 
.
Israel walikuwa na operation Nimrod, ni wao huyo?
Nafkiri unaongelea Operation Nimrod ya SAS uingereza maana ndio walikuwa na operation Nimrod ya kuokoa mateka kwenye ubalozi wa iran nchini uingereza...... However sijafaham kwanni waliita operation nimrod hivyo siwezi kucomment chochote kuhusiana na jina hilo labda nimuite mtaalam wa intelijentsia
Malcom Lumumba Elungata
 
Mkuu Magonjwa Mtambuka kumbe ni great thinker hivi?? achana na jukwaa la siasa naona linatuficha ur bright side.
 
Natamani elimu hizi zingekuwa zinadadavuliwa kwa kina kwenye majumba yetu ya ibada, badala ya kinachoendelea hivi sasa..

Hii ishu ya Atlantis nilidhani ni story tu, lakini nimepitia scriptures kadhaa nikabaini kuna asilimia nyingi za ukweli. Siku nikipata wasaa nitashushia uzi wake ukiwa ni sehemu ya majibu ya uzi huu.

Kuhusu Wanefili

Hawa kwenye Biblia wameelezewa kuwa ni uzao wa Malaika waliozini na Binadamu. Kwenye Quran ni tofauti, kwa maana kwenye uislamu Malaika wanaelezwa kama viumbe visivyo na jinsia hivyo na havina matashi.. So ni ngumu kuingiliana na binadamu.. Badala yake, Quran na hadithi kadhaa zinakubali kwamba kuna kizazi cha majini (asili ya Ibilisi) waliwahi kuasi na kufanya matendo ya ngono na wanadamu hivyo kuangamizwa..

Maelezo ni mengi. Nimedaka haya kwa uchache yatuongezee maarifa. Bahati nzuri/mbaya yapo kwa kiingereza;

The holy Quran also speaks about the people of ‘Ad and Thamud. They were huge and powerful, and could uproot trees with their hands. They were also civilized and skilful. But because of their strength and wealth, they rejected the truth and caused a lot of havoc and mischief on the land. So Allah punished them. Allah wiped them off the surface and it was as though they never existed.

Mengine;

Allah says in the holy Quran in Surah 41:15: “As for ‘Ãd, they turned arrogant on earth, opposed the truth, and said, “Who is more powerful than we?” Did they not realize that GOD, who created them, is more powerful than they? They were unappreciative of our revelations.”
And Also in Surah 89:6-9: “Saw you not how your Lord dealt with the ‘Ad (people). Of the (city) of Iram, with lofty pillars, The like of which were not created in the land? And (with) the Thamud (people), who hewed out rocks in the valley?

Tusiache kusoma na kujifunza zaidi..
 
Kwani wewe si umeambiwa lilipotea tuu, shida nini
Ilizama baharini.... Ila shida yangu nijue kama liliexist na lilikuwa na uwezo gani maana nakumbuka nmeona documentary Hitler akituma makomandoo kwenda kutafuta hiyo nchi ili kujua watu walioishi mule na wawatumie kutawala mabara mengine

So it's important mkuu
 
Wewe unaeleza kikristo,mwenzako unaeleza kiislamu hakuna sababu ya wewe kumpinga Wala yeye kukupinga,swali hili hili ukimuuliza muumini Wa dini nyengine atakupa majibu ambayo huyategemei, ndio Dunia ilivyo mbaya zaidi hii midini yote tumeletewa na weupe!
Nalog off
 
"lililoongelewa na mwanafalsafa wa kigiriki Plato kwamba lilikuwa na teknolojia kubwa kuliko hata ya sasa "
Hapo tu ndo umezingua mkuu unajua kwa nn? Plato kazaliwa 427 na kufariki 347 sasa yeye alijuaje kuwa teknolojia ya atlantic ni kubwa kuliko ya miaka hii ya sasa ?
 
Kwa enzi zake mkuu.... Licha ya plato tu hata Hitler naye ambaye aliishi kipindi teknolojia ipo kubwa alituma kikosi cha makomandoo kwenda kusaka ilipo atlantis na watafute race iliyoishi pale ili iweze kuwasaidia wajerumani kwenye vita ya kuitawala dunia. So ipo common understanding kwamba hao Atlantis walikuwa na teknolojia kubwa kwa wakati wao.
 
Hebu acheni kupotosha watu kwanza malaika sio wanaume sio wanawake na Mungu amewaumba malaika kumtii na kumuabudu sio kwa namna nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…