Upi ni mtazamo sahihi juu ya maisha

doppla2

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
1,314
1,366
Salaam JF

Ebu leo tusaidiane katika hili, upi ni mtazamo sahihi juu ya

1. Pre destination Life (hatima iliokwisha kupangwa)

2. Worked out destination ( hatima inayotafutwa)


Katika mtazamo wa kwanza, unalenga kutuonyesha kuwa kabla ya kuzaliwa hatima zetu zimeshapangwa, no matter what! Alichokipanga Mungu lazima kitokee maishani mwetu.

Dhana hii uondoa uwajibikaji kwa mtu na kumuonyesha mtu kuwa victim wa nguvu za asili. Watu wengi wa dini uamini sana mtadhamo huu....


Mtazamo wa pili unasisitiza hatima inatengenezwa kwa maamuzi na hatua unazozichukua kila siku.
Dhana hii inampa mtu kuwajibika juu ya hatima yake, hata hivyo dhana hii ushindwa kutoa majibu ya mambo yanayowakabili watu ambayo hawana uwezo nayo kuyacontrol lakini yanatokea .


Je wewe mdau unaamini dhana ipi kati ya izi juu ya maisha.

Uswazi usema kama ipo ipo tu....

Washua usema you got to prepare your Future.....

Karibuni wadau mchangie
 
Mie naona 2 ndo sawa. Wa 1 mungu zngekuw anapanga kabla ya kuumbwa. Nadhani kuna watu wasingekuja hapa duniani.
 
Back
Top Bottom