Kipangaspecial
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 19,408
- 25,932
Ndugu yangu unasumbuliwa na tatizo la kujiona unajua kila kitu. Ukifanikiwa ku deal na hilo tatizo perpendicularly utakuwa umefanikiwa pakuwa sana maishani.Una ufahamu mdogo wa mambo ya siasa. Hayo makundi uliyotaja leo hii vyama vya siasa vilivyopo ukiachia ccm, vikijaribu kuonyesha ukaribu tu na makundi hayo, utasikia yanajihusisha na siasa. Yaani ni makosa hayo makundi kuonyesha mahusiano yoyote na chama cha siasa cha upinzani, na yanaweza kukutana na hujuma za wazi dhidi ya ccm kupitia taasisi za kimamlaka, na mifano ipo wazi.
Tuje kwa Nyerere ambaye ni mfano wako. Nyerere alikuwa na mahusiano na hiyo Govenor Turnbull sio kwa sababu Huyo gavana alitaka, bali Tanganyika haikuwa koloni la Uingereza, ila ilikabidhiwa kwa Uingereza na Umoja wa mataifa, mpaka tutakapokuwa tayari kujitawala yenyewe. Nyerere ndio aliyekuwa na chuki ya wazi dhidi ya mfumo wa vyama vingi ili aburuze watu kwa mtazamo wake. Na kwa taarifa yako Nyerere ndio muasisi wa viongozi kukaa madarakani wapendavyo, na hakuna mwenyekiti yoyote wa chama cha siasa aliyejimilikisha chama cha siasa muda mrefu kama yeye. Alikuwa mwenyekiti wa TANU na Ccm zaidi ya 20yrs,na kama sio sera zake kuingiza nchi hii kwenye umasikini mkubwa, asingetoka madarakani kwenye ccm na urais.
Punguza u much know