Ni vilaza na wenye chuki binafsi pekee ndio wanaona hii serikali imefeli,lakini kiukweli serikali ya awamu ya nne imefanya vizuri sana kuliko serikali zote zilizopita.Kwanza imeondoa ubaguzi wa maendeleo.Tulishuhudia serikali zilizopita zilikuwa na mpango mahususi wa kudunisha baadhi ya maeneo katika nchi mf.Rukwa,Ruvuma,Kigoma,Lindi na Mtwara,Tabora,Tanga,Pwani,Singida nk huku wakitoa kipaumbele kwa mikoa ya Arusha,kilimanjaro,Dar,mwanza na Mbeya kana kwamba wengine hawalipi kodi.
Kama sasa hivi unazunguka nchini utashuhudia mabadiliko makubwa kwa maendeleo hasa ile mikoa iliyotelekezwa hapo awali.Ruvuma ,kigoma ,Rukwa na sehemu zingine wananchi wanafuraha sana.Kiukweli tutakukumbuka JK kama bwana maendeleo hilo halina ubishi,umekuwa mkombozi wa watanzania,ni mzalendo hasa wa nchi yako.Mungu akubaliki sana na akulinde!