FANANI MTENZI
Senior Member
- Jul 4, 2017
- 106
- 95
UPEPO WA USIKU-25
BONIFACE BIRAGE
“Ni shushushu wa wapI?”
“Bado hatujajua lakini hii tattoo ni maalum kwa mashushushu wanaopandikizwa mataifa tofauti!Yupo ambaye aliwahi kukamatwa hapa miaka ya nyuma alikuwa na tattoo kama hii.Haina tofauti yoyote”
Alisema wakala au agent James.Hilo lilikuwa jipya kwa Linda aliyetamani kumaliza kitendawili hiki.
“Au ndo maana anasema Masua alikuwa mume wake?”
“Mume wake!Masua kaoa lini halafu huyu si mke wa Bario?”
Wote wakaangaliana kana kwamba wameelewa kitu Fulani!
“Ndiyo amesema hivyo na kabla sijamaliza kumuhoji alizimia!Alishindwa kustahimili adhabu tuliyompa!”Linda alisema akiendelea kukagua zile nyaraka!Moja ilimpa umakini sana ilikuwa bahasha imeandikwa Poliyandry test!Alitambua maana ya neno hilo kwamba ni kitendo cha mwanamke kuolewa zaidi na mume mmoja.Yaani anakuwa na waume halali wa ndoa wawili nakuendelea.Hili hufanyika kwa tamaduni kadhaa duniani na hufanywa hivyo kulingana na sababu kadhaa wa kadhaa!Tamaduni nyingine hutokea kwa kuwa na uhaba wa watoto wa kike au kutengeneza ukaribu nakumpa mwanamke kipaumbele katika swala zima la taasubi ya kike!Lakini kwa nchi za kiafrika hili halikuwepo kw asana na hata kama ilitokea basi mambo hayo hufanyika kwa siri sana!
Mwanamke kuwa na mume au mpenzi zaid ya mmoja hutafsirika kama uhuni!Na kama ikitokea basi wengi hufanya jambo hilo kwa njia ya usaliti yaani anakuwa anawachezea shere wapenzi hao pasipokujuana.Kikawaida mwanaume ndo huwa na mke zaidi ya mmoja kwenye jamii za kiafrika.Lakini kwa tafsiri ya neno lililo kwenye bahasha ni kuwa mwanamke anakuwa na mume zaidi ya mmoja na wote wanajua kwamba huyo ni mke wao!
“Unaona hiili neno?”alisema Linda akimuonesha James ambaye alithibitha kuona neno hilo nakujua tafsiri yake.Wakafungua bahasha ile nakukutana na nyaraka zimefungwa kwa pamoja walizifungua nakuona vitu vya ajabu!Vilikuwa vyeti cha kwanza kilikuwa cha kanisani kati ya Laredo na Bario ikionesha uhalali wa ndoa yao!Nyuma ya cheti kulikuwa na picha ya harusi yao!Cheti cha pili kilikuwa kati ya Masua na Laredo halali kabisa cha ndoa!Ndoa hii ilifungwa kwa DC!Ilikuwa yakiserikali na tena ina kila uhalali wa kisheria.Aliona hadi tarehe na kila kitu yaani haikuwa na miezi mingi.Hilo lilizidisha mshangao mkubwa kwa Linda ambaye aliona kasalatiwa na Masua.Ina maana Laredo alichosema ni ukweli mtupu?Alipoendelea kukagua zile nyaraka akaona picha kati ya Laredo na Masua wakiwa kwa DC!Hukuhitaji kuhoji zile picha zilikuwa za nini!Walifunga ndoa halai kweli!Hilo likamuogopesha sana mwanamke huyu!
Alipokagua zaidi akaona cheti cha tatu ambacho kilisajiliwa kwa shekhe!Kilikuwa cha kiislamu na ndoa halali ya Laredo na Hamza!Hapo hapo akaona na picha iliyoambatanishwa kwa nyuma ya kile cheti ikimuonesha Hamza na Laredo wakiwa wamejipamba vizuri kabisa siku ya ndoa yao!Linda alibaki mdomo wazi huku akimpa James nyaraka zile nay eye akathibitisha wote wajikuta wakimuogopa Laredo kwani kuweza kudanganya waume watatu nakufunga nao ndoa halikuwa jambo la akawaida!Na hivi wamekuta ana mchoro wa tattoo kwenye mwili wake.Mchoro ambao unathibitisha kwamba yeye ni shushushu wa kupandikizwa kwa kuwa tattoo ile iliwahi kukutwa kwa shushushu mwingine wa kupandikizwa miaka kadhaa iliyopita.
“Umeelewa kilichopo kwenye hivi vyeti?”
“Nimeelewa alikuwa kaolewa na wanaume wote watatu!Sasa swali aliwezaje kuwarubuni wote watatu?Na kama yeye ni shushushu yawezekana alifanya haya kumfikia shushushu wetu Masua nakumuingiza kwenye mtego huu?”
Walijiuliza maswali hayo bila kuwa na hitimisho.
“Inabidi tutoe taarifa.Huyu kama ni shushushu wa kupandikizwa lazima tujihadhari naye hatujui ni mangapi amejua kutoka kwa Masua!”
“Sidhani kama Masua ameweza kujitaja yeye ni shushushu.”alitetea Linda.
“Hapana kurubuniwa hadi kamuoa nakulishwa ujinga akaishi naye nyumbani muda wote huu hadi kafa kwa sumu ya panya atakuwa alivujisha siri nyingi.Hili ni tusi kwenye idara yetu kwa shushushu wa kupandikizwa kukutwa eneo alimokufa shushushu wetu!”alishauri James kwa ghadhabu kuu.
“Unadhani tufanyeje?”
“Lazima atuambie katumwa na nani na kwanini aliolewa na wanaume wa tatu je,walijua kuwa ni mke wao?”alisema James.
“Ok twende tuone hali yake.”alishauri Linda.Walitoka katika ofisi zao wakaenda hadi alipolazwa Laredo walimkuta kafunikwa na blanketi nzito huku chumba chake kikiwa na joto kali kudhibti baridi lililoganda mwilini mwake.Tayari alikuwa amehudumiwa.Walimkuta kapumzika.
Walimtikisa nakumuamsha!
“Unaweza kuongea?’’alianza Linda.Laredo alitikisa kichwa kuitikia.
“Eti uliniambia Masua ni mumeo?”
“Ndiyo.”
“Lakini siulikuwa mke wa Bario?”
“Walikuwa waume zangu wote.Bario,Masua na Hamza.Niliwashawishi hadi wakakubali nikaishi nao nyumba moja.Tulifanya kitu kinaitwa polyandry!”
Linda na James wakatumbua macho.Baada ya mateso Laredo anatoa kisa chote.Wamegundua ni shushushu!Ni mtu aliyemtaalam anaweza kufanya jambo hilo tu!