Upepo wa Membe mtaani usipime

Upepo wa Membe mtaani usipime

Angalia asije akijakata mwenyewe maana anatakiwa ajibu trilion 2.4 ziko wapi
Watanzania tufike mahali tukubali kumpongeza anayeonyesha moyo angalau wa kutuvusha,
tusitegemee nchi hii iongozwe na malaika asiyekuwa na doa hata kidogo.
Binafsi naona hakuna haja ya kutoa maelezo ya hiyo trioni 2.4
mimi naweza kusema nchi hii ni kubwa kumtegemea mtu mmoja adhibiti mambo yote na pasiwepo upungufu
haiwezekani,huenda hilo pengo kama lipo limesababishwa na wasimamizi wake,maana tunashuhudia
kila mara watu wanatenguliwa na wengine kuwekwa.
 
Upinzani hautakaa ujipange maana aidha haupo kwa maana kuwa waliopo ni ccm kwa bendera za upinzani au upo ila haujui nini ufanye, kama BCM akianza joto la urais wajue ni ccm ktk camoufalege ili kupoteza muda upinzani kujipanga ushinde. Am sorry for you

Upinzani ni neno la kiswahili (lugha ya taifa) mbona wengi tunashindwa kuelewa linamaanisha nini?
 
Watanzania tufike mahali tukubali kumpongeza anayeonyesha moyo angalau wa kutuvusha,
tusitegemee nchi hii iongozwe na malaika asiyekuwa na doa hata kidogo.
Binafsi naona hakuna haja ya kutoa maelezo ya hiyo trioni 2.4
mimi naweza kusema nchi hii ni kubwa kumtegemea mtu mmoja adhibiti mambo yote na pasiwepo upungufu
haiwezekani,huenda hilo pengo kama lipo limesababishwa na wasimamizi wake,maana tunashuhudia
kila mara watu wanatenguliwa na wengine kuwekwa.

Trilioni 2.4 ni nyingi kushinda ufisadi wote uliotokea kwenye serikali ya BWM plus ya JK

Unataka tusamehe hivihivi tu mjomba?
 
Trilioni 2.4 ni nyingi kushinda ufisadi wote uliotokea kwenye serikali ya BWM plus ya JK

Unataka tusamehe hivihivi tu mjomba?
kati ya hao ni nani aliwahi hacha kutekeleza,tuongelee kuwaza
kuhamishia ikulu Dodoma,kujenga SGR,kujenga fly overs n.k?
Hatutegemei mtu alowane umande wakati amekaa chumbani kwake tena kwenye kochi.
kitendo cha JPM kuthubutu,kinanifanya nimuunge mkono.
 
Hayo Maji unayokunywa miundo mbinu ilijengwa na JPM?
Hiyo Mwendokasi unayopanda kwenda town/Muhimbili ilijengwa na JPM?
Chuo cha UDOM anachosoma mtoto wa mjomba wako alijenga JPM?
Daraja la Kigamboni wanalopita wauza madafu kutoka Kibada alijenga JPM
Huo umeme unaowasha nchi nzima aliuweka JPM?
Vipi Barabara unazotumia kwenda kwenu huko Bukoba, Mwanza, Kahama, Geita, Mtwara, Simiyu, Katavi?
Babu yako akishikwa ugonjwa wa moyo akatibiwa JK Health Institute, aliijenga JPM?
Hizo shule za kata anazosoma mtoto wa dada yako alizijenga JPM?

Mpaka mwaka wa nne wa utawala wake JK alishajenga shule za Kata nchi nzima na Chuo kikuu cha UDOM plus Kilometa kibao za barabara, Huyu wa sasa mwaka wa nne ndo kwanza anazindua ujenzi wa miradi yake ambayo ni "Legacy projects"

Miradi mingi Mikubwa kama Daraja la Kigamboni, Hospitali ya Mloganzila, Termina 3, Darala lile la Kilombero unayoona anazindua leo Ilianza wakati wa utawala wa JK, Pesa alitafuta JK ila sema tu kwa sababu alikuwa lazima astaafu kwa mujibu wa sheria na katiba imeendelea kujengwa na kumalizika katika utawala wa JPM, kwa hiyo ukiona JPM anazindua basi anazindua tu jasho la mwenzie.

Tungoje miradi ya JPM kama SGR na Stiglers ikamilke naye tumpe ujiko lakini so far mpaka sasa bado anatembelea nyota ya JK kwa sana
 
Benard Membe for presidency.. 2020. WanaCCM wenzangu tusiharibu tena kipenga kikipulizwa. Chama chetu lazima tukisimamishe tena.
 
Mlionaaccess ya kumpata mzee wetu huyu mfikishieni ujumbe wetu Watanzania. Hakuna wakati tunamuhitaji Mh Benard Membe kama 2020. Yeye ndie wakututoa kwenye shimo hili tulilopo sasa.
 
Hakuna siri tena,kwenye kile chama kuna kundi kubwa limeibuka likimtaka mh Membe kusimama 2020

Na kwa utafiti mfupi uliofanyika lakini sio rasmi unaonyesha kuwa Membe anakubalika zaidi na wanaccm wengi na wasio wanachama wa ccm

Eitha ,imeonyesha kuwa endapo Membe atasimama 2020 upinzani utakuwa na nguvu chache tofauti akisimama mzee mwenye nyumba ambapo upinzani unaweza ukawa na nguvu kuliko hata kipindi cha Lowasa na mabadiliko

Mikoa inayomuunga Membe kwa asilimia 100 ni Mtwara,Lindi,Ruvuma,Njombe,Iringa,Mbeya,Kigoma,Kagera,Mwanza jiji,Mara,Arusha,Kilimanjaro, Tanga,Pwani,Dar,Singida na mikoa yote ya Zanzibar

Mikoa inayomuunga Mzee mwenyewe wa chama ni Dodoma,Geita,wilaya za Mwanza(nje ya jiji),Simiyu, Katavi na Tabora

Mikoa ambayo wanagawana nusu kwa nusu ni Rukwa,Morogoro,Manyara na Shinyanga
Tunamtaka Lissu, weka Membe pembeni
 
Magufuli hahitaji CCM , ni CCM ndo ina muhitaji Magufuli, Magufuli hata akihamia chauma akampisha membe ccm na membe akaungana na wana cecm wote bado Magufuli atawashinda , huyu jamaa utendaji wake una mbeba sana mazuri ni mengi kuliko mabaya
Vizuri mkuu basi wekeni wagombea wawili katika kinyang'anyiro. Magu na Membe.
 
Ana weza fanya hivyo na bado akashinda, tena kwa 100%, kumbuka yeye ana mawaziri zaidi ya 20, wabunge ambao akihama wengi watamfuata, wabunge wengi wanataka guarantee ya kurudi tena bungeni, hivyo wana muhitaji Magufuli kuwa vusha, wakurugenzi ambao ni wakeleketwa wakuu wa uchaguzi ni wateule wakuu was Rais, vyombo vya ulinzi na usalama wakuu wake ni wateule wake, akitoka ccm hii advantage ccm itakuwa haina tena, huyu mtu unafikiri ccm watamshinda? ukweli kuwa ccm ndo ina muhitaji Magufuli wala sio vingine.
Mbona unawaza kawaida sana? Unafahamu nini kuhusu nguvu ya chama kwa raisi? Akiachana na chama ameachana na hiyo nguvu unayoiongelea mpaka atakapoipata tena kupitia chama kingine(kama ataipata). Raisi anafanya kazi lakini kumpandisha cheo kuliko chama unajidanganya. Halafu unatakiwa ufahamu pia kuna watu nchini wana nguvu na wafuasi mpaka kwenye majeshi na si maraisi. Ndo maana kuna nchi machafuko na uasi wa jeshi hutokea endapo watu wao wakiguswa.
 
Tunamtaka Lissu, weka Membe pembeni

Tangu mambo ya kutekana tekana, kuuawa kwa baadhi yetu, kuminywa uhuru wetu, etc.. yalipoanza, Watanzania tulishafanya maamuzi ya kumpa kiti cha uRais Mh Benard Membe. #tunamwagapombe
 
Watanzania tufike mahali tukubali kumpongeza anayeonyesha moyo angalau wa kutuvusha,
tusitegemee nchi hii iongozwe na malaika asiyekuwa na doa hata kidogo.
Binafsi naona hakuna haja ya kutoa maelezo ya hiyo trioni 2.4
mimi naweza kusema nchi hii ni kubwa kumtegemea mtu mmoja adhibiti mambo yote na pasiwepo upungufu
haiwezekani,huenda hilo pengo kama lipo limesababishwa na wasimamizi wake,maana tunashuhudia
kila mara watu wanatenguliwa na wengine kuwekwa.
Tetea kwa akili basi. Sema hakuna T2.4 iliyopotea, kama haipo kwenye ndege basi ipo kwenye reli au umeme kuna sehemu tu imetumika.
Yaani pengo la pesa yote hiyo ndani ya miaka minne unatetea kuwa ni wasimamizi? Yeye akiwa wapi? Anavyoogopeka nani wa kuchota zote hizo? Unajua hiyo figure ni kubwa kuliko pesa zote zilizopigwa miaka kumi ya aliyepita? Mayb even na ya wa nyuma yake.
 
Mbona unawaza kawaida sana? Unafahamu nini kuhusu nguvu ya chama kwa raisi? Akiachana na chama ameachana na hiyo nguvu unayoiongelea mpaka atakapoipata tena kupitia chama kingine(kama ataipata). Raisi anafanya kazi lakini kumpandisha cheo kuliko chama unajidanganya. Halafu unatakiwa ufahamu pia kuna watu nchini wana nguvu na wafuasi mpaka kwenye majeshi na si maraisi. Ndo maana kuna nchi machafuko na uasi wa jeshi hutokea endapo watu wao wakiguswa.
Anaweza badili katiba , chama kijitenge na serikali kabla ya uchaguzi, na akafanya kampeni kwa makada wote wa ccm kura za ndio zitashinda, nguvu aliyonayo ni kubwa kuliko kijani chenu, yuko hapo mtoeni muone effect yake.
 
Acha kabisa Mkuu hili likitokea la Bugirichato kupigwa chini furaha itakayokuwepo nchi nzima itakuwa haina mfano.

Watanzania wengi watalia machozi ya furaha na wengine walioathiriwa na huyo dhalimu kwa namna mbali mbali yatakuwa machozi ya huzuni.

Nina uhakika kabisa kuwa siku hiyo Bubu Atataka Kusema BAK
 
Tuliokuwepo enzi za azimio la Arusha,kulikuwa na misemo fulani
mmojawapo ni huu "Kukata mirija" na mheshimiwa Magufuli anachokifanya
ni kukata mirija,hayo mambo ya kupelekwa mahakamani ni upotevu wa fedha ya umma
mimi naona ni heri tukate mirija, wa kunyauka atanyauka mwenyewe bila hata kesi.
Ni kupambana kuziba nyufa zilizotumika kutunyonya mengine yafuate,na huwezi kuyafanya yote kwa wakati mmoja.
Mkuu mrija wa trilioni 2.4 mbona haujakatwa???...trioni 2.4 zipo wapi????
 
Wantanzania wengi hatujui thamani ya pesa, tril2.4 itoke wapi? miradi mingi ni makusanyo kidogo na wanatanguliza down payment, 2.4 ni accumulations ya projects zipi?
 
Back
Top Bottom