Upendo wa Mama katika Klabu ya AC Milani

Upendo wa Mama katika Klabu ya AC Milani

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Katika kuungana na dunia kusherehekea Siku ya Mama Duniani Jumapili hii Mei 11, 2025, klabu ya AC Milan imeendeleza utaratibu wa wachezaji wake kuvaa jezi zenye majina ya Mama zao mgongoni badala ya majina yao kama ilivyozoeleka.
1746862002748.jpg

Wachezaji wa AC Milan kwa mara nyingine walivaa jezi hizo dhidi ya Bologna jana wakishinda mabao 3-1 kama ilivyokuwa msimu uliopita kwenye mchezo dhidi ya Cagliari walioshinda kwa mabao 5-1.
1746861998797.jpg

AC Milan wamelazimika kuvaa jezi hizo jana Mei 09, kwa sababu hawatakuwa na mchezo wa ligi Mei 11, ambapo ndio maadhimisho ya siku hiyo Ulaya na kwingineko duniani.
1746861943918.jpg

Wameweka utaratibu mzuri wa kuadhimisha siku ya kina Mama duniani. Klabu zingine zifuate utaratibu kama huu.
 
Nzuri sana hii.

Mzazi anajivunia sana mwanae kumtambulisha duniani.
 
Sawa Sisi wababa tunaendelea kupambana ili muendelee kuimba nani kama mama.
 
Ikifika Siku Ya Upendo Wa Baba Naamini Kama Si Maji Maji Fc Ya Songea Basi Ni Simba Sports Club Watatimiza Sawa Na Hilo La Ac Milan....Tuombe Duah Inshallahh......!!!
 
Back
Top Bottom