Upendo ni Udhihirisho wa Thamani ya kile kinachopendwa.Mathalani,Unaposema unampenda mtu basi utadhihirisha waziwazi kwa kuonesha huyo mtu ni wa thamani kiasi gani kwako.
Hata hivyo kuna "Upendo wa uongo" ambao unaonekana kutamalaki sana hususani katika kizazi hiki.Hakuna namna ya kuutambua "Upendo huo wa uongo" pasipo kujua sifa pambanuzi za Upendo wa Kweli ambazo baadhi yake ni. .
1.HAUTOI KASORO WALA HAUHESABU MABAYA.Akupendae kwa dhati ukimchunguza vema utagundua ni kama vile hazioni kabisa kasoro zako wala mabaya yako.Anahesabu mazuri yako tu na kukusaidia kufix hizo "kasoro" ulizonazo.
2.HAUNA UBINAFSI(SELFLESS).Upendo huu adimu una asili ya kujitoa "Sadaka" kwa ajili ya ustawi wa mwingine.Tena hutoa bila kutarajia malipo(fadhila) yoyote.Yaani Upendo huu huwa unatoa mema bila kujali malipo yake yatakuwaje.Ukiona mtu yeyote anakutendea "mema" huku anajipigia hesabu yeye kwanza katika hayo "mema" unayoona anakutendea,ndugu yangu weka mguno wenye kishindo kikuu...!
3.HUVUMILIA NA KUSTAHIMILI.Hii pia ni miongoni mwa sifa adimu kabisa za Upendo wa kweli.Kuvumilia na Kustahimili!.Kama hujui Ustahimilivu ukoje kachunguze mimea ya jangwani.Upendo huu una kawaida ya kumshape mtu awe tayari kuukabili "Ukame".
4.HUSITIRI WINGI WA MAKOSA.Ukiona kila ukikosea kibinadamu(siyo makusudi) inaorodheshwa orodha ya makosa yako ya nyuma basi hapo rafiki,fungua macho kiukweli hakuna Upendo bali pana kitu kingine kabisa ambacho nadhani hata jina hakina au kina majina mengine mengine tu lakini hakina hadhi ya kuitwa Upendo.
5.SI MWEPESI WA HASIRA NA HAUNA TABIA YA KUTAFUTA KULIPA KISASI.Ukiona kukomoa au kisasi kinachukuliwa kama ndo "tiba"aisee hapo Upendo hakuna.Hapo kuna biashara nyingine kabisa...!.Kwa ujumla hakuna kinachoyafanya Maisha haya yawe na THAMANI kama UPENDO.Ndo maana kuna watu wakiukosa wapo tayari kuutafuta hata wa "kununua" au wa "kukodi" ili mradi tu wajione wanathaminiwa.
Mungu akipenda wakati mwingine nitaelezea Duka linalogawa bure Upendo huu wenye sifa tajwa hapo juu.Kila la Kheri Ndugu Zangu....!