Upendo wa kweli una sifa hizi...

Upendo wa kweli una sifa hizi...

StudentTeacher

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2019
Posts
6,555
Reaction score
7,699
Upendo ni Udhihirisho wa Thamani ya kile kinachopendwa.Mathalani,Unaposema unampenda mtu basi utadhihirisha waziwazi kwa kuonesha huyo mtu ni wa thamani kiasi gani kwako.

Hata hivyo kuna "Upendo wa uongo" ambao unaonekana kutamalaki sana hususani katika kizazi hiki na hakuna namna ya kuutambua "Upendo huo wa uongo" pasipo kuzijua sifa pambanuzi za Upendo wa Kweli ambazo baadhi yake ni;

1.HAUTOI KASORO WALA HAUHESABU MABAYA. Akupendae kwa dhati ukimchunguza vema utagundua ni kama vile hazioni kabisa kasoro zako wala mabaya yako.Anahesabu mazuri yako tu na kukusaidia kufix hizo "kasoro" ulizonazo.

2.HAUNA UBINAFSI(SELFLESS). Upendo huu adimu una asili ya kujitoa "Sadaka" kwa ajili ya ustawi wa mwingine.Tena hutoa bila kutarajia malipo(fadhila) yoyote.Yaani Upendo huu huwa unatoa mema bila kujali malipo yake yatakuwaje.Ukiona mtu yeyote mahali popote anakutendea "mema" huku anajipigia hesabu yeye kwanza katika hayo "mema" unayoona anakutendea,ndugu yangu weka mguno wenye kishindo kikuu...!.

3.HUVUMILIA NA KUSTAHIMILI. Hii pia ni miongoni mwa sifa adimu kabisa za Upendo wa kweli.Kuvumilia na Kustahimili!.Kama hujui Ustahimilivu ukoje kachunguze mimea ya jangwani.Upendo huu una kawaida ya kumshape mtu awe tayari kuukabili "Ukame".

4.HUSITIRI WINGI WA MAKOSA. Ukiona kila ukikosea kibinadamu(siyo makusudi) inaorodheshwa orodha ya makosa yako ya nyuma basi hapo rafiki,fungua macho kiukweli hakuna Upendo bali pana kitu kingine kabisa ambacho nadhani hata jina hakina au kina majina mengine mengine tu lakini hakina hadhi ya kuitwa Upendo.

5.SI MWEPESI WA HASIRA NA HAUNA TABIA YA KUTAFUTA KULIPA KISASI. Ukiona kukomoa au kisasi kinachukuliwa kama ndo "tiba" aisee hapo Upendo HAKUNA.Hapo kuna biashara nyingine kabisa...!.Mahali ambapo Upendo wa kweli upo huwezi kusikia habari za eti "MTU KAMCHINJA MPENZI WAKE NA SHOKA KISA AMEMSALITI AU BLA BLA NYINGINE ZINAZOFANANA NA HIZO".Haiingii akilini hata kidogo kwamba Mtu uliyekuwa unamuimbia wimbo wa "nakupenda" leo hii unaamua kwa hiyari yako kumchinja.Rafiki,Upendo na Kumchinja "umpendae" wapi na wapi?.Kumpenda Mtu hakumaanishi na yeye akupende hivyo hivyo.BIG NO.Kumtendea MTU mema sio sababu ya yeye kukurudishia mema pia.Ukiujua Ukweli huu hautakuja kujutia kamwe uwepo wako chini ya jua...! 6.UPENDO WA KWELI HAUFURAHII UDHALIMU.Udhalimu maana yake ni kwenda kinyume na HAKI.Haki ni jambo ambalo mtu anastahili kupewa au kufanyiwa.Upendo wa kweli kamwe hauungi mkono wala mguu Udhalimu na haijalishi nani anaufanya udhalimu huo.Siku zote Upendo wa kweli unasimama katika HAKI.Ukiona unafanya udhalimu halafu watu wanakuangalia tu,hawakuonyi,hawakukemei wala kukukosoa tambua wazi kwamba HAWAKUPENDI.Wanakuacha makusudi tu ili hatimaye ukija kuvuna matunda ya udhalimu ulioupanda washangilie,wakucheke,wakubeze ili mradi tu waoneshe kwamba HAWAKUPENDI. Kwa ujumla hakuna kinachoyafanya Maisha haya yawe na THAMANI kama UPENDO.Ndo maana kuna watu wakiukosa wapo tayari kuutafuta hata wa "kununua" au wa "kukodi" ili mradi tu wajione wanathaminiwa.

Mungu akipenda wakati mwingine nitaelezea DUKA linalogawa BURE Upendo huu wenye sifa tajwa hapo juu ikiwemo ni namna gani Upendo huu unaweza kupandwa,kuoteshwa na kustawishwa ndani ya "moyo" wa mtu na hatimaye matunda yake yakawafaa wanaomzunguka mtu huyo na kufanyika ushuhuda mwema.Kila la Kheri Ndugu Zangu....!
 
Huo unaohubiri upendo wa mshumaa na haupo

mtu anatongoza hadharani au unamfuma halafu tu ujifanye hujaona na usimuhesabie makosa ni unafiki wa kimataifa kwakweli
 
Nashukuru sana kwa kunialika kwenye mada yako na naunga mkono uliyoyasema maana yapo kwenye maandiko ya kikristo ila labda niseme tu kwamba hizo sifa za upendo wanaume wengi hawatakagi kuwa nazo au kuzionyesha kwa wanawake wao lakini hao hao wanaume wanataka wanawake wao wawe nazo au wazionyeshe kwao

Basi kuna vilaza watakuja hapa kusema kuwa wanaume hawajaumbiwa kupenda wameumbiwa kutamani
 
Upendo ni Udhihirisho wa Thamani ya kile kinachopendwa.Mathalani,Unaposema unampenda mtu basi utadhihirisha waziwazi kwa kuonesha huyo mtu ni wa thamani kiasi gani kwako.

Hata hivyo kuna "Upendo wa uongo" ambao unaonekana kutamalaki sana hususani katika kizazi hiki.Hakuna namna ya kuutambua "Upendo huo wa uongo" pasipo kujua sifa pambanuzi za Upendo wa Kweli ambazo baadhi yake ni. .

1.HAUTOI KASORO WALA HAUHESABU MABAYA.Akupendae kwa dhati ukimchunguza vema utagundua ni kama vile hazioni kabisa kasoro zako wala mabaya yako.Anahesabu mazuri yako tu na kukusaidia kufix hizo "kasoro" ulizonazo.

2.HAUNA UBINAFSI(SELFLESS).Upendo huu adimu una asili ya kujitoa "Sadaka" kwa ajili ya ustawi wa mwingine.Tena hutoa bila kutarajia malipo(fadhila) yoyote.Yaani Upendo huu huwa unatoa mema bila kujali malipo yake yatakuwaje.Ukiona mtu yeyote anakutendea "mema" huku anajipigia hesabu yeye kwanza katika hayo "mema" unayoona anakutendea,ndugu yangu weka mguno wenye kishindo kikuu...!

3.HUVUMILIA NA KUSTAHIMILI.Hii pia ni miongoni mwa sifa adimu kabisa za Upendo wa kweli.Kuvumilia na Kustahimili!.Kama hujui Ustahimilivu ukoje kachunguze mimea ya jangwani.Upendo huu una kawaida ya kumshape mtu awe tayari kuukabili "Ukame".

4.HUSITIRI WINGI WA MAKOSA.Ukiona kila ukikosea kibinadamu(siyo makusudi) inaorodheshwa orodha ya makosa yako ya nyuma basi hapo rafiki,fungua macho kiukweli hakuna Upendo bali pana kitu kingine kabisa ambacho nadhani hata jina hakina au kina majina mengine mengine tu lakini hakina hadhi ya kuitwa Upendo.

5.SI MWEPESI WA HASIRA NA HAUNA TABIA YA KUTAFUTA KULIPA KISASI.Ukiona kukomoa au kisasi kinachukuliwa kama ndo "tiba"aisee hapo Upendo hakuna.Hapo kuna biashara nyingine kabisa...!.Kwa ujumla hakuna kinachoyafanya Maisha haya yawe na THAMANI kama UPENDO.Ndo maana kuna watu wakiukosa wapo tayari kuutafuta hata wa "kununua" au wa "kukodi" ili mradi tu wajione wanathaminiwa.

Mungu akipenda wakati mwingine nitaelezea Duka linalogawa bure Upendo huu wenye sifa tajwa hapo juu.Kila la Kheri Ndugu Zangu....!
Mi naunga mkono hoja
 
Upendo ni Udhihirisho wa Thamani ya kile kinachopendwa.Mathalani,Unaposema unampenda mtu basi utadhihirisha waziwazi kwa kuonesha huyo mtu ni wa thamani kiasi gani kwako.

Hata hivyo kuna "Upendo wa uongo" ambao unaonekana kutamalaki sana hususani katika kizazi hiki ambapo hakuna namna ya kuutambua "Upendo huo wa uongo" pasipo kuzijua sifa pambanuzi za Upendo wa Kweli ambazo baadhi yake ni:

1.HAUTOI KASORO WALA HAUHESABU MABAYA.Akupendae kwa dhati ukimchunguza vema utagundua ni kama vile hazioni kabisa kasoro zako wala mabaya yako.Anahesabu mazuri yako tu na kukusaidia kufix hizo "kasoro" ulizonazo.

2.HAUNA UBINAFSI(SELFLESS).Upendo huu adimu una asili ya kujitoa "Sadaka" kwa ajili ya ustawi wa mwingine.Tena hutoa bila kutarajia malipo(fadhila) yoyote.Yaani Upendo huu huwa unatoa mema bila kujali malipo yake yatakuwaje.Ukiona mtu yeyote anakutendea "mema" huku anajipigia hesabu yeye kwanza katika hayo "mema" unayoona anakutendea,ndugu yangu weka mguno wenye kishindo kikuu...!

3.HUVUMILIA NA KUSTAHIMILI.Hii pia ni miongoni mwa sifa adimu kabisa za Upendo wa kweli.Kuvumilia na Kustahimili!.Kama hujui Ustahimilivu ukoje kachunguze mimea ya jangwani.Upendo huu una kawaida ya kumshape mtu awe tayari kuukabili "Ukame".

4.HUSITIRI WINGI WA MAKOSA.Ukiona kila ukikosea kibinadamu(siyo makusudi) inaorodheshwa orodha ya makosa yako ya nyuma basi hapo rafiki,fungua macho!.Kiukweli hakuna Upendo,bali pana kitu kingine kabisa ambacho nadhani hata jina hakina au kina majina mengine mengine tu lakini hakina hadhi ya kuitwa Upendo.

5.SI MWEPESI WA HASIRA NA HAUNA TABIA YA KUTAFUTA KULIPA KISASI.Ukiona kukomoa au kisasi kinachukuliwa kama ndo "tiba",aisee hapo Upendo hakuna.Hapo kuna biashara nyingine kabisa...!. 6.UPENDO WA KWELI HAUFURAHII UDHALIMU.Udhalimu maana yake ni Kinyume na HAKI.HAKI maana yake ni kile ambacho mtu anastahili kupewa au kutendewa.Hivyo kwa maana nyingine Udhalimu ni kutokutenda HAKI,yaani,
kutompa au kutomfanyia mtu jambo analostahili kupewa au kufanyiwa.Upendo wa Kweli KAMWE hauungi mkono wala mguu Udhalimu.Siku zote Upendo wa Kweli unasimama kwenye HAKI.Ukiona hutendi HAKI halafu watu hawakuonyi wala kukukemea wala kukukosoa ujue hawakupendi.Wanasubiri Uangamizwe na Udhalimu wako(ikumbukwe hakuna mavuno yaliyo kinyume na mbegu iliyopandwa) ili hatimaye wakukucheka akucheke,wakukuzomea akuzomeee,wakukubeza akubeze ili mradi tu wakuoneshe kwamba HAWAKUPENDI. Kwa ujumla hakuna kinachoyafanya Maisha haya yawe na THAMANI kama UPENDO.Ndo maana kuna watu wakiukosa wapo tayari kuutafuta hata wa "kununua" au wa "kukodi" ili mradi tu wajione wanathaminiwa.

Mungu akipenda wakati mwingine nitaelezea Duka linalogawa bure Upendo huu wenye sifa tajwa hapo juu ikiwemo namna gani Upendo huu unavyoweza kupandwa,kuoteshwa na kustawishwa ndani ya "moyo" wa mtu na kisha matunda yake yakaanza kujidhihirisha waziwazi na kushuhudiwa na wanaomzunguka mtu huyo.Kila la Kheri Ndugu Zangu....!
 
Back
Top Bottom