Upendo utawale, kuna watu wako radhi kuhairisha walichopanga kufanya ili kutatua changamoto zako

laii

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
834
1,060
Kwenye hii Dunia ya sasa, ni watu wachache sana watakupenda jinsi ulivyo, ni watu wachache watajua mapungufu (ujinga) wako na kuendelea kukupenda jinsi ulivyo, ukipata mtu au watu wa aina hii washikilie sana, waombee sana.

Ni watu wachache wataichukulia shida yako kama yao, kuna watu wapo radhi kukopa ili kukusaidia katika matatizo yako, wako radhi kuhairisha walichopanga kufanya ili kutatua changamoto zako, hakika ukimpata mtu wa aina hii mshikilie sana na muombee sana Kwa Mungu.

Ukiwa nao usiongee kupitiliza utajikuta umeongea hadi mambo yatakayomkera, chagua maneno ya kuongea na wakati sahihi ya kuyaongea, usilielie shida wala kuomba omba hela iwe kukupa bure au kumkopakopa, usijieleze sana kwake kuhusu changamoto zako na familia kwa ujumla, mkishaongea mara moja mwache, mara nyingi watu wa aina hii husukumwa na Upendo walio nao kusaidia na si mara ngapi umemwambia shida zako. Jitahidi kuficha madhaifu yako mbele yake, acha ayaone au ayasikie.

Dunia ya leo imejaa watu wanaojipenda wenyewe Wenye kujali vitu kuliko utu, akishiba yeye inatosha haangalii wengine, ni watu ambao wako radhi kuuzima uhai wa kiumbe chochote Kwa ajili ya mali. Kwa hiyo ukipata mtu wa aina hiyo hapo juu mshikilie sana, na wewe pia ujitoe Kwa watu ambao unaweza kuwasaidia na kurejesha tabasamu lao.

Mungu Awabariki Na Kuwalinda, Kwa Jina La Baba na La Mwana na La Roho Mtakatifu. Amina.
 
Kwanini usiwe hivi ulivyojieleza? Unadhani kwanini akusaidie wewe tu? Atasaidia wangapi kama wewe? Unadhani yeye hana shida? Kusema kwamba anaweza kuacha vyake ili akusaidie wewe, je hauoni kama huo ni ubinafsi wako?

Kila mwanaune apambane kivyake na ale kwa jasho lake.
 
Kwanini usiwe hivi ulivyojieleza? Unadhani kwanini akusaidie wewe tu? Atasaidia wangapi kama wewe? Unadhani yeye hana shida? Kusema kwamba anaweza kuacha vyake ili akusaidie wewe, je hauoni kama huo ni ubinafsi wako?

Kila mwanaune apambane kivyake na ale kwa jasho lake.
Hujaelewa topic, tafadhali rudia kusoma tena, ninaweza nikawa Mimi nasaidia, inawezekana Akawa yule, Anaweza kubwa mtu yeyote. Simaanishi mtu awe tegemezi, I mean If You have some one who knows Ur flushness and he/she still tolerate You, hold him or her tight ndugu.
 
 
Kwenye hii Dunia ya sasa,ni watu wachache sana watakupenda jinsi ulivyo,ni watu wachache watajua mapungufu (ujinga) wako na kuendelea kukupenda jinsi ulivyo,ukipata mtu au watu wa aina hii washikilie sana,waombee sana.
Ni watu wachache wataichukulia shida yako kama yao,Kuna watu wapo radhi kukopa ili kukusaidia katika matatizo yako,wako radhi kuhairisha walichopanga kufanya ili kutatua changamoto zako,hakika ukimpata mtu wa aina hii mshikilie sana na muombee sana Kwa Mungu.
Ukiwa nao usiongee kupitiliza utajikuta umeongea hadi mambo yatakayomkera chagua maneno ya kuongea na wakati sahihi ya kuyaongea, usilielie shida Wala kuomba omba hela iwe kukupa bure au kumkopakopa,usijieleze sana kwake kuhusu changamoto zako na familia kwa ujumla,mkishaongea mara moja mwache mara nyingi watu wa aina hii husukumwa na Upendo walio nao kusaidia na si mara ngapi umemwambia shida zako.
Jitahidi kuficha madhaifu yako mbele yake,acha ayaone au ayasikie.
Dunia ya leo imejaa watu wanaojipenda wenyewe Wenye kujali vitu kuliko utu,akishiba yeye inatosha haangalii wengine,ni watu ambao wako radhi kuuzima uhai wa kiumbe chochote Kwa ajili ya mali.Kwa hiyo ukipata mtu wa aina hiyo hapo juu mshikilie sana,na wewe pia ujitoe Kwa watu ambao unaweza kuwasaidia na kurejesha tabasamu lao.

Mungu Awabariki Na Kuwalinda, Kwa Jina La Baba na La Mwana na La Roho Mtakatifu.Amina.
Daaah.....hongera mkuu kwa hili ulilobarikiwa na kusukumwa na roho mtakatifu uliandike.🙏
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom