Upendo Peneza (CHADEMA) awalaumu Wabunge wanaohama vyama. Asema chaguzi za marudio ni kucheza pesa za wananchi!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Mbunge wa Viti Maalum wa CHADEMA, Upendo Peneza ameitisha mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar na huenda akatangaza uamuzi mgumu.

More to follow
============

UPDATES:



=> Upendo Peneza: Anasema tunaenda kupoteza pesa za marudio ya uchaguzi kwa wabunge waliojiuzulu kwani gharama za uchaguzi ni za wananchi.

=> Anasema yeye haondoki Chadema, habari zilizotolewa ni kuwa anaenda CCM ni uzushi.
pene1.jpg

=> Amesema anachukizwa na tabia ya wabunge wanaohama kwa sababu wanawaumiza wananchi kwa kutumia gharama kubwa katika uchaguzi. Fedha hizi zingeenda kujenga shule na hospitali. "Tumeendelea kuona wabunge wakihama vyama. Taifa linaingizwa kwenye pressure ya uchaguzi hata kabla ya muda. Tulidhani ingekuwa ni mda wa sisi wabunge kufanya kazi za maendeleo lakini tumekuwa tukipoteza mda wa kuhama vyama"
pene2.jpg

=> Anasema wanaondoka upinzani wamehongwa na kununuliwa na CCM. Anasema kulikuwa na rumors za yeye kwenda CCM sasa amekuja kukanusha.

=> Anasema wabunge hao waliohama wangempongeza Rais Magufuli wakiwa katika vyama vyao.

=> Anaangalia namna ya kupitia Katiba kama wanaweza kuzuia uchaguzi wa marudio kwa wabunge waliohahama. Anaongea na wanasheria kumsaidia kufikia azma yake ya kuzuia Marudio ya Uchaguzi kwa Waliojiuzulu.

=> Anasema alichokisema ni msimamo binafsi sio wa chama chake.

=> Nimehusishwa kuhama Chadema,Mimi sihami chadema kwa sababu nina amini katika Chadema.Nimekuja kuwaambia watanzania kuhusu utapeli wa hawa wanaohamahama vyama kwa sababu tu ya kumuunga mkono Rais.

=> CCM iache kurubuni na kuhonga watu ili kuwanunua wahamie chama Cha mapinduzi

=> Nakubaliana kuwa Kwenye vyama vya siasa kuna changamoto, Hata ndani ya Chadema kuna changamoto lakini nitavumilia sitahama chama
 
Kumekua na hali ya Stofahamu ndani ya Chadema ikiwemo kutokuaminiani Baada yakujiuzulu kwa Dr.Godwin Moleli aliyekua Mbunge wa Siha haijulikani nani atafuata,Dr.Mollel amerejea kwnye Chama chake cha Zamani alikuja kwa Mafuriko ya Lowasa mda huo huo akaaminiwa nakuteuliwa Kua mgombea kisha akashinda ipo haja yakua na Utaratibu maalum kwa watu wanaohama vyama vyao wakati wa Uchaguzi,Je nani atafuatia baada ya Dr.Mollel hii ndio swali linalobaki bila majibu ya moja kwa moja
 
Kutoka upinzani kwenda CCM kwa kununuliwa siku yamekuwa maamuzi magumu?Hivi viti maalumu vinatakiwa kufutwa kama ilivyopendekezwa kwenye katiba mpya.
Upendo Peneza yule ana akili sana sidhani kama anaweza kujiunga CCM.
Peneza asema mwanzoni mwa utawala wa MagufuliJP alikuwa na matumaini mengi lakini kadri siku zinavyosonga amekuwa akivunjwa moyo kuona uhuru wa mawazo, mikusanyiko ya kisiasa na kuikosoa serikali ukiminywa.
 
Kumekua na hali ya Stofahamu ndani ya Chadema ikiwemo kutokuaminiani Baada yakujiuzulu kwa Dr.Godwin Moleli aliyekua Mbunge wa Siha haijulikani nani atafuata,Dr.Mollel amerejea kwnye Chama chake cha Zamani alikuja kwa Mafuriko ya Lowasa mda huo huo akaaminiwa nakuteuliwa Kua mgombea kisha akashinda ipo haja yakua na Utaratibu maalum kwa watu wanaohama vyama vyao wakati wa Uchaguzi,Je nani atafuatia baada ya Dr.Mollel hii ndio swali linalobaki bila majibu ya moja kwa moja
Mfumo ukiingiliwa na adui kutoka nje, adui anatengenezewa mazingira mabaya na hatimaye kutolewa nje. Kinachoendelea ni mfumo kujisafisha, kama vile kutapika na kuharisha. Uchafu ukiisha, mwili huendelea na taratibu zake za kujiimarisha tena. Na kwa bahati nzuri mwili ukiisha shambuliwa na ugonjwa fulani na kiinga ya ugonjwa huo huanza kujengeka. Hatutababaishwa na wageni hasa wanaotoka CCM.
 
CHADEMA na UKAWA kwa ujumla ikae kwa ujumla na wabunge wao wawaulize wabunge hao kua wangapi wanataka kuondoka kwenda CCM kuungana na mh Rais kwaajiri ya kuunga mkono juhudi za Rais( wao wanavyosema)wawaruhusu waende tuendelee na mambo mengine.
UKAWA haipo, hivi huwa MNA akili kweli nyie??? ni lini uliona ukawa imekaa pamoja toka 2015??
 
Back
Top Bottom