Upendo Nkone amuomba msahama Martha Mwaipaja

Upendo Nkone amuomba msahama Martha Mwaipaja

Lakini inaonekana Kuna ukweli ndani yake sema upendo kaamua kuomba radhi yaishe kwakua Sasa hawezi thibitisha kisheria.
 
Sakata hilo limeibuka leo katika mitandao ya kijamii, baada ya Martha Mwaipaja kuchapisha video akimtaka Upendo Nkone kueleza kwa ushahidi wa kisheria ni lini na wapi aliwahi kumtishia Maisha, pamoja na madai ya kuwasiliana naye kwa simu. Kauli hiyo ya Martha imeonekana kumlazimisha Upendo Nkone kujitokeza hadharani na kuomba msamaha.
Jela sio kuzuri kwa wakina mama km hawa waoneeni huruma ile ilikua ni content creation tu kupata viewers na alishalipwa na hii ya kuomba msamaha pia amelipwa tena Jela sio kuzuri kwa wakina mama km hawa sio km yule
 
Yaani wasani wa gospel wanatumia skendo za kipuuzi ili wapate "jina,wajulikane(umaarufu)" "kweli kiki mambo mbaya"
Oya Upendo Nkone hawezi kutafuta kick maana yeye mwenyewe ni kick tosha jina lake tu linamtambulisha kabla ya kazi zake emu tuacheni hizi basi aah sometimes mnaboa sana
 
Asiyekuwa na akili hapo ni huyo Upendo Nkone. Anastahili kuomba msamaha.
 
Asiyekuwa na akili hapo ni huyo Upendo Nkone. Anastahili kuomba msamaha.
 
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Upendo Nkone, amemuomba radhi Mwimbaji mwenzake Martha Mwaipaja kufuatia kauli aliyoitoa kwenye moja ya mahojiano, akidai kuwa aliwahi kutishiwa Maisha kupitia simu.

Sakata hilo limeibuka leo katika mitandao ya kijamii, baada ya Martha Mwaipaja kuchapisha video akimtaka Upendo Nkone kueleza kwa ushahidi wa kisheria ni lini na wapi aliwahi kumtishia Maisha, pamoja na madai ya kuwasiliana naye kwa simu. Kauli hiyo ya Martha imeonekana kumlazimisha Upendo Nkone kujitokeza hadharani na kuomba msamaha.

Akizungumza, Upendo Nkone amesema kuwa yeye ni Mkristo na anaamini katika msamaha, hivyo ameona ni vyema kuomba radhi kwa kauli aliyoitoa kwenye mahojiano aliyofanya na Lilian Mwasha.

Akizungumza na AyoTV, Nkone amesema “Kazi ya Shetani ni kugombanisha na kuchonganisha Watu. Inawezekana sikupaswa kulisema suala hili hadharani, nilipaswa kubaki nalo kimya. Lakini nilipohojiwa, nikajieleza, na sasa naona imeleta madhara.

Nipo hapa kumuomba msamaha Mwimbaji mwenzangu Martha Mwaipaja. Naomba anisamehe popote nilipomuumiza au kufanya jambo ambalo hakulipenda. Halikuwa lengo langu. Mungu hapendi mvutano, anapenda amani. Nilizungumza kama simulizi ya jambo lililopita, lakini kwa sasa nashusha moyo na kumuomba anisamehe.” Amesema Nkone.
Petty issues...
Mambo wayapendayo ccm
 
Back
Top Bottom