Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,869
- 828,403
Jumanne tulimchangia Catherine (mdogo wake Baraka) kiasi cha TZS 15.6M ili kimsaidie kumalizia elimu yake CBE na pia kiweze kusaidia familia yake na kumsaidia Baraka mwenyewe ambaye alivunjwa miguu yote miwili na kupewa kesi ya Uhaini. Tunamshukuru Mungu kesho yake Baraka akaachiwa huru.
Hata hivyo kukawa na maoni mengi ya watu wakitaka kijana aliyekua akimbeba Baraka gerezani na Mahakamani Kisutu nae achangiwe. Kijana huyo anaitwa Jovin Kaaya mkazi wa Kimara jijini DSM alijitolea kumbeba Baraka kwa kipindi chote wakiwa gerezani. Jana tukaweka mkeka na kwa neema ya Mungu tumeweza kumchangia Jovin kiasi cha TZS 10.9M.
Mungu awabariki sana wote mlioshiriki sadaka hii. Kiasi hiki alichopata Jovin atatoa kiasi kidogo kusaidia familia ya Nyapara aliyekua akiwahudumia gerezani. Kwahiyo tumeweza kurudisha tabasamu kwa familia ya Baraka na Jovin kwa kuwachangia jumla ya TZS 26.5M. Kwa niaba ya familia hizi mbili tunawashukuru sana. Utukufu kwa Mungu 🙏🏽