Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Upelelezi wazidi kukwamisha kesi ya Kitilya na wenzake
Upelelezi wa kesi inayomkabili Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya, mshindi wa Mashindano ya Urembo (Miss Tanzania), mwaka 1996, Shose Sinare na Sioi Solomon katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bado haujakamili.
Dar es Salaam.Upelelezi wa kesi inayomkabili Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya, mshindi wa Mashindano ya Urembo (Miss Tanzania), mwaka 1996, Shose Sinare na Sioi Solomon katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bado haujakamilika.
Wakili wa Serikali, Hellen Moshi aliyaeleza hayo leo kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Hata hivyo Hakimu Nongwa aliutaka upande wa mashtaka Juni 2, 2017 kueleza upelelezi umefikia katika hatua ipi.
Katika kesi hiyo washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani 550 milioni kwa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Uingereza.
Wanadaiwa kula njama na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, Kwa upande wa mshtakiwa.
Chanzo: Mwananchi