Upelelezi /uchunguzi unaohusisha mitandao ya kimataifa pamoja na computer . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upelelezi /uchunguzi unaohusisha mitandao ya kimataifa pamoja na computer .

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MziziMkavu, Oct 17, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Mafunzo yoyote na miongozo yoyote iliyokwepo kwenye nyaraka hii ni kwa ajili ya masomo ( kujifunza ) tumia miongozo na mafunzo mengine ndani ya nyaraka kwa ajili ya kujifunza wewe na wenzako .

  Matumizi ya computer na mitandao ya kimataifa yanazidi kukua kila siku ukuaji huu umefanya ukuaji wa uhalifu kwa njia ya mtandao na mitandao nao kukua kwa kasi , vitendo vya uhalifu vinaweza kufanyika kwa njia ya mtandao sasa kuliko wakati wowote wa historia ya binadamu .

  Wahalifu wanaweza kuendesha vitendo vya vya kuhalifu kwa njia ya mtandao bila kujulikana kwa urahisi zaidi vinavyohusiana na biashara , wizi na njia zingine mbali mbali , kwa kujificha kutumia njia mbali mbali ndani ya mitandao hii .

  Tovuti , vyumba vya kulonga , barua pepe vinaweza kutumika kama vyombo vya kutafuta ushahidi katika upelelezi wa uhalifu unaohusiana na mitandao ya mawasiliano ya computer .  Mafunzo yaliyomo ndani ya nyaraka hii ni kwa ajili ya watu wanaohusika na upelelezi kwa njia ya mtandao au wale wanaopenda kujifunza zaidi mambo haya , ingawa haiwezi kujibu maswali yote yanayohusiana na mitandao hii kwa sababu tekilologia na mbinu hubadilika wakati mwingine kutegemeana na kitu ulichokutana nacho .

  Utumiaji wa Mtandao na aina nyingine za mitandao ya computer imekuwa kwa kiasi kikubwa sana , na matokeo yake aina yoyote ya uhalifu inaweza kufanyika kutumia vifaa hivi vinavyowasiliana kutumia njia ya mitandao ya kimataifa .

  Msomaji unatakiwa ujue kwamba mhalifu anaweza kutumia mitandao ya kimataifa kwa sababu mbali mbali .

  - Kufanya biashara , kubadilishana vitu na wahalifu wenzake ( kama nyaraka , picha , video hata programu za computer )

  - Kufuta taarifa zao au za wengine kwa njia ya mtandao au hata kuharibu na kuchafua

  - Kutumia Taarifa ambazo sio zao au za wengine kwa shuguli za kihalifu

  - Kutafuta au kuchunguza taarifa za wanaowafanyia uhalifu

  - Kuwasiliana na wahalifu wenzake

  - Kuchapicha , sambaza taarifa ambazo sio za kweli

  - Kuandaa Mikutano , kuisimamia tovuti za jamii na kufuatilia taarifa za watu kutumia mitandao hiyo haswa mambo yao ya fedha .


  Upelelezi wa aina hii ni mgumu na mrefu sana wakati mwingine , ushahidi wa matukio haya unaweza kupatikana kwenye vifaa vyenyewe vinavyotumika kwenye kuwasiliana , ukiwahusisha wahalifu wengi , pamoja na watu wengi ambao wamefanyiwa uhalifu huo .

  Vyanzo vya Taarifa vinaweza kupatikana sehemu yoyote ile duniani lakini kuwa tabu kwa mpelelezi kuvifikia kwa urahisi zaidi kutokana na mahala vilipo vyanzo hivyo kwa namna moja au nyingine .

  Vyanzo hivi ni kama

  - Wahalifu , wale waliofanyiwa uhalifu na wanaohisiwa kuendesha uhalifu huo

  - Taarifa zilizokwepo kwenye Computer au router za wengine kama biashara , taasisi za kiserikali au za kimasomo .

  - Recodi za ISP ( Mtoaji wa huduma za Internet )

  Wakati mwingine Taarifa zilizo kwenye mfumo wa Electroniki zinaweza kupotea kwa urahisi zaidi kwa mfano

  - Zinaweza kubadilika kutokana na matumizi

  - Zinaweza kuharibiwa au kuharibika

  - Zinaweza kuharibika kutokana na Udhibiti mbovu

  Kutokana na sababu hizo Ushahidi unatakiwa uhifadhiwe vizuri na kutunzwa kwa njia nzuri zaidi na salama , pia kumbuka unapochunguza masuala yanayohusiana na mitandao , muda , tarehe vinaweza kuwa muhimu sana , muda wa computer au server unaweza kuwa sio sawa na muda wa sehemu ambapo uhalifu huo unafanyika au unaendelea mpelelezi anatakiwa atumie taarifa zingine kuhakikisha muda na tarehe ni sawa kama inavyotakiwa kuwa .

  Pia kwenye upelelezi itategemea sana ujuzi wa mtu husika pamoja na vifaa anavyotumia katika kufanya upelelezi au uchunguzi huo , anatakiwa atambue kwamba chochote anachofanya kinaweza kusababisha computer na vifaa vyake kuharibika au kupata hitilafu na kuharibu ushahidi Fulani ambao ni muhimu sana .

  Kama mpelelezi anataka kushugulika na computer hizo na vifaa vyake lazima ahakikishe vinahifadhiwa kwa njia ya maandishi .

  Kabla ya yote haya kumbuka Mlalamikaji lazima awepo , Mashahidi watambulike na wawe wameshafanyiwa usahili , Njia zilizotumika kwenye upelelezi ziandikwe pamoja na masuala mengine ya kisheria kutokana na eneo husika ambapo uhalifu umetendeka . Mpelelezi anatakiwa ajue mambo yafuatayo

  - Ni kweli uhalifu umetendeka ?

  - Nani ana haki Kisheria ?

  - Vitu gani vinahitajika katika upelelezi na uchunguzi ?

  - Je vifaa hivyo vinatosha na vinafaa kuendesha uchunguzi ?

  - Kuna Taarifa zipi za nyongeza

  - Je kuna mambo mengine ya kisheria ya kujadiliana na Vyombo vingine ?

  SOMO LA 1 – KUCHUNGUZA VYANZO VYA BARUA PEPE

  Kama tunavyojua Kila nyumba au eneo lina Anuani na kila computer iliyounganishwa kwenye mtandao ina anuani inaitwa IP au Internet Protocol . Sehemu hii itaonyesha jinsi Anuani hizi zinavyopewa computer na kuchunguza mwanzo wake .  YONA F MARO
   
Loading...