Nimesoma thread humu ndani kuhusu mgombea ubunge wa UPDP, kwa bahati nzuri nilifanikiwa kupata picha zake baada ya kufukuzia msafara wake kwa baiskeli, ulinipita nikiwa katika baa ya Kibo nikipata msosi. Alipofika aliuliza hapa ndio stendi yenu akajibiwa ndio, akauliza maliwatoni ni wapi, akaelekea huko akidai anakwenda kukagua, lakini nadhani alikwenda kuchimba dawa maana alikuwa chicha mbaya.
Nimewaletea picha hizo ili wale ambao kwa sababu moja ama nyingine hamkuweza kuziona msipitwe.
View attachment 37882
Msafara wa Ali Kabaka, mgombea Ubunge kwa tiketi ya UPDP ukielekea kwenye viwanja vya kampeni eneo la stendi mjini Igunga tarehe 25/09/2011. Gari inayoonekana nyuma sio sehemu ya msafara huo.
Kwa kweli niliona habari ya Mh.Ali Kabaka mgombea wa UDDP ilirushwa TBC a.k.a TV ya chama, jamaa alikua anaongea kwa sauti ya kilevi na alikua anaulizwa maswali na baadhi ya wapambe wake alikua nao kwenye msafara wake. Alizidi kudhihirisha kuwa amelewa pale aliposema kuwa atawawezesha vijana wawe wanalipwa 'dollar pound'ambapo sikuelewa anamaanisha nini. Akazidi kuwaambia kuwa anajua vijana wanateseka kwa kukaa vijiweni na kuchomwa na jua kama solar pannel na atawawezesha wawe na maisha mazuri na kuacha kukaa vijiweni kupigwa na jua kutwa nzima kama solar pannel. Pia alitanngaza sera yake ya kilimo kwa kusema yeye ataanzisha programme itakayoitwa ardhi kwanza na kilimo baadae.Mgombea alikua anongea kwa nmana ya kilevi na kihuni na kushangiliwa na kundi la watu walioonekana wamelewa chakari.Katikati ya mkutano MC alitangaza kuwa hou ni mkutano wa kipekee kwa kuwa kuna vinywaji na wahudhuriaji wanakaribishwa ila wanunue kwa hela yao na akasema zipo bia, soda na chips Kwa kweli UDDP wametia aibu ni kama mgombea wao alikua anaigiaza FUTUHI
Hi ni aibu kubwa kabisa kwa Taifa letu kama wagombea ndio hawa hatuwezi kabisa kuleta mabadiliko yoyote,hii ni sawa na comedy ya akina masanja tena hii haina kiwango