Updates za Mazao ya msimu wa 2022

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,012
1,627
Habari wakulima na wafugaji wenzangu, kutokana na hali ya hewa kubadilika na mvua kuwa chache nimeona ni bora tupeane updates za maendeleo ya Mazao hapa nchini ili watu wajipange kwa kununua Mazao sehemu yatakapopatikana kwa wingi

Huku maeneo ya Tanga hasa maeneo ya Muheza naona kama mvua ishakimbia na Mahindi yameachwa stages ambayo si Rafiki, yameachwa mengi yakiwa na umri wa mwezi mmoja na wakulima wengi wamepanda Mbegu za kienyeji ambazo zinachukua mpaka siku 120 mpaka kukomaa

Vip eneo lako Mazao yanaendaje?
 
Mkoa wa pwani pia hali ni hiyo maeneo ya mkuranga, mvua mwaka huu ni kidogo na zimekwisha mapema.
 
Afadhali ya nyie kama mtavuna kidogo wengne kwenye mpunga tumekula za kichwa mazima aisee... alaf ndio bei ya mpunga kubwa hatar.
Ngoja tukanunue tu alzeti ili tufidie hasara japo nao mwaka huu wameanza na bei kubwa balaa.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom