Tayana-wog
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 30,108
- 41,777
Asee kweli Waafrika wengi asa wabongo washakuwa addicted na kumtaja Mungu ata Kwa kitu ambacho hausiki nacho
Sent using Jamii Forums mobile app
Watu 200 kwa siku? Hebu muulize mwandishi tenaBarua kutoka Italia
___________________
Amani kwa wote,
Tunaishi Italia - Milan,
Nitashiriki nawe na kukuelezea
"Vipi maisha hapa Milan" wakati wa siku hizi ngumu, nadhani unapaswa kujifunza kutokana na makosa na matokeo ambayo tunaishi hapa.
Hivi sasa tumetengwa. Hatuwezi kwenda barabarani, polisi wanasimama kila wakati na kumkamata mtu yeyote nje ya nyumba yake.
Kila kitu kimefungwa! ... biashara, maduka makubwa, maduka madogo, mitaa yote bila mtu yoyote kutembea.
Tunahisi ndiyo mwisho wa ulimwengu !!
Italia, nchi nzuri ya kuishi, inabadilishwa kutoka wakati mmoja hadi mwingine kana kwamba ni nchi iliyo kwenye giza la vita.
Ni ukweli kwamba sikuwahi kufikiria kwamba ningeweza kuishi!
Watu wamechanganyikiwa, huzuni, wasiwasi na hawana msaada, na mara nyingi hawaelewi jinsi ukweli huu ulivyowekwa kwao na wakati gani hali hii ya usiku itamalizika.
Kosa kubwa ni kwamba mwanzoni mwa watu wa kwanza kupata ugonjwa, watu waliendelea kuishi maisha yao kama kawaida na waliingia mitaani kwa kazi, burudani na kuhisi ni kama kipindi cha likizo, kwa hivyo mikusanyiko na marafiki na karamu ziliongezeka.
Kila mtu alikosea na ndivyo pia ulivyokuwa!
Ninakuomba, kuwa mwangalifu, hii sio kichekesho wala utani.
Kinga wapendwa wako, wazazi wako, na wazee wako! Ugonjwa huo ni hatari kwao.
Karibu watu 200 hufa hapa kila siku, sio kwa sababu dawa huko Milan sio nzuri (ni moja wapo bora ulimwenguni), lakini ni kwa sababu hakuna mahali kwa kila mtu!
Madaktari huchagua nani atakufa! Hii ni kwa sababu ya utelezi wa wananchi hapo mwanzoni, ambao waliamua kuendelea na maisha yao kama kawaida, bila kujali hali mpya!
Tafadhali, jifunze kutoka kwa makosa, sisi ni nchi ndogo ambayo inaweza kuishia na janga kubwa.
Sikiliza vizuri sasa ,,, [emoji120]
Usitoke kwenda kwenye sehemu zenye watu.
Usijaribu kula mahali pa umma. Kaa muda mrefu nyumbani wakati huu!
Sikiliza miongozo ya Wizara ya Afya (usichezee!).
Ongea umbali wa mita kutoka kwa kila mtu, usikaribie karibu, usichanganye au ukubali.
Pata matibabu ya ziada na ya kuzuia na ujifunze kutoka kwa makosa ya wengine.
Tunapendekeza kuchukua vitamini C kuongeza mfumo wako wa kinga.( Tumia matunda jamii ya machungwa, na limao katika chakula chako )
Kusaidia wataalamu kuzuia kuenea kwa janga ...
Huko Italia, nchi nzima imetengwa, ikimaanisha watu milioni 60 wametengwa!
Hii ingezuiwa ikiwa watu wangesikia maagizo tangu mwanzo.
Jitunze na maisha ya yule umpendaye [emoji173][emoji173]
___________________________________
Ujumbe huu unafaa kushiriki ikiwa unajali wengine
Jr[emoji769]
Serikali imefanya uzembe, kuruhusu safari na kutofunga mipaka.Bandiko nyingi humu, hata iliyoanzisha mjadala huu, ni kulaumu tu. Hata Mshana Jr, nguli ya JF, naye anashadidia lawama hizo.
Tutambue kuwa kinga thabiti ya maradhi, yoyote yale, ni ya mtu binafsi, kaya na jamii kwa ujumla. Isitoshe, wakati Serikali kwa ufinyu wa "resources", ikikabiliwa na majanga mengi, hasa wakati huu wa masika ambapo miundo mbinu ya barabara inaharibika, kutaka kuwepo na vituo vya kukagua na kuhudumia walioambikizwa kila sehemu, ni kukosa uelewa.
Hivyo basi, kusisitiza kila mwananchi kuchukua tahadhari, ni jambo la msingi katika kuthibiti kuenea kwa ugonjwa nchini.
Forewarned is forearmed
Watu 200 kwa siku? Hebu muulize mwandishi tena
Naona imetolewa
Mmhh chanzo cha hii taarifa?
Nimeona juzi Muhimbili watu wanapanga foleni kunawa mikono kwa maji na sabauni. Nikajiuliza kwa foleni zilizopangwa hapo, akitokea mgonjwa mmoja akapiga chafya au kukohoa wataambukizwa wangapi? Kama Muhimbili wenye dhamana ya kulinda afya hawako makini kiasi hicho, vipi wanasiasa na viongozi wengine wa kisiasa?Natambua umahiri wetu wa kuvifanya vitu serious kuwa mizaha. Natambua ujuzi wetu wa kuyageuza majanga kuwa manufaa ya kisiasa.
Hivi ni kipi kikubwa tumekifanya kama taifa cha serious kujikinga na hili gonjwa linalotaka kuwa janga la dunia?
Nimemsikia Waziri wa Afya akikutangazia umuhimu wa kutoshikana mikono wala kukumbatiana wakati wa kusalimiana kama ilivyo jadi yetu. Wanasiasa wakalibeba hili mzobe mzobe. Mengine yote sidhani kama yamepewa kipaumbele.
Waziri katangaza kila mkoa utenge maeneo maalum ya kuchunguza wenye dalili na viashiria vya huu ugonjwa.
Je, hili limetekelezwa?
Je, kuna vifaa ya kutosha kwenye hili?
Je, bajeti imetoka wapi?
Je, kuna wahudumu wa dharura wenye uelewa na huu ugonjwa wameandaliwa?
Je, sahihi ni kutenga vituo kila mkoa ama kila wilaya?
Je, mpaka sasa ni mikoa mingapi imelitekeleza hili?
Je, kuna changamoto yoyote?
Je, kuna kipindi maalum kwenye vyombo vya habari kutoa mapya ya kila siku kuhusiana na huu ugonjwa?
Hakika maswali ni mengi sana. Lakini nilichokiona kwenye huu ugonjwa ni mizaha na kukosa umakini. Hatuna takwimu rasmi zozote mpaka sasa za chochote kuhusiana na huu ugonjwa. Hatujaona umakini wowote kwenye maandalizi ya dharura. Chukulia mfano mkoa wa Pwani kutoka Mkuranga mpaka Bagamoyo utenge kituo kimoja tu cha ukaguzi wa corona, inawezekana kweli!?
Kinachopigiwa chepuo sasa ni kusalimiana bila kushikana mikono, eti kugongesha miguu. Mmh! Tumeiona kwa viongozi, lakini nyie msioshikana mikono sasa si mlikaa chumba kimoja kwa madakika mengi tu? Je, mlitumia viziba midomo na pua?
Hivi kwani corona ni ugonjwa wa ngozi? Iweje wachezaji uwanjani wazuiwe kusalimiana kwa kushikana mikono eti ni mojawapo ya kampeni ya kupambana na corona wakati huo huo wachezaji haohao watakuwa pamoja uwanjani kwa dakika 90+ wakishikana, wakivutana, wakiangukiana wakipumuliana? Vipi na wale mashabiki watazamani kwa maelfu walio majukwaani? Tuna abiria kwa maelfu wanasongana kwenye vyombo vya usafiri. Kwenye masoko. Kila mahali.
Bado hatuko serious na mizaha ndio imetawala kupitia siasa. Mungu pekee ndio anatubeba. Kitengo cha dharura kitaifa hakijasema chochote. Kipo kimya kabisa. Vyombo vyetu vya habari ni siasa na wanasiasa mwanzo mwisho. Viziba pua na midomo vimepanda bei maradufu. Box lilikokuwa linauzwa elfu 10 piece 50 sasa hivi linauzwa elfu 40 na hapo ugonjwa haujachanganya. Ukithibitika upo nchini na tukatakiwa kutumia hivyo vifaa tutafanyaje?
Jr[emoji769]
Hii nayo ni habari ya kutuletea hapa ?.
Hii nayo ni habari ya kutuletea hapa ?.