Nyakwec's Bro
JF-Expert Member
- Apr 27, 2012
- 820
- 174
Nimesikia sana hizi tetesi za timu kama Azam naYanga kutoa mzigo katika mechi zao za mwisho,lakini hivi ni kweli
unaweza kutoa pesa timu yenye uwezo mdogo iifunge timu yenye uwezo mkubwa?..Nadhani mwenye nafasi ni yule
anaetoa dau ili timu yake ishinde Yanga haina sababu ya kupoteza pesa ilichemka yenyewe kushindwa kumfunga Azam na
kufungwa na mgambo imuache tu Azam achukue ubingwa kama kwa halali au kwa kuhonga shauli yake ijipange msimu
ujao.
Kwa namna hongo inavyotembea sitoshangaa Mbeya City akifungwa kiurahisi na Azam.
Sitashangaa MCC akipigwa 3 kesho.
Yawezekana kabisa ! Maana Azam wapo tayari kwa lolote.
Any way mkuu,angalau msimu huu umekuwa na ushindani wa ubingwa.
azam msimu huu wapo sawa sana na hii idea ya kuhonga inaonekana ndio janja ya simba na yanga hata kipindi cha nyuma azam wakikaza gemu ya kwanza ya pili unasikia kafungwa ila toka omog kaingia upuuzi huo haupo kabisa..
acheni tubebe ndoo na sherehe itakuwa tamu sana kesho.. ila mcc wapo poa sana
Ni kweli kabisa ila kwa ulaya leo barca kagongwa na granada , ligi zote naona zinafanana tu , kila timu inaombea mwenzie afungwe , wadhamini wajitokeze kwa hz timu ndogo pia , ili ziwe na nguvu ligi itakuwa na ushindani sana.
Zamu ya azam kubeba ndooo! Mie mbeya city damu lakini hatuna cha kupoteza biti la nafasi ya tatu linatosha msimu huu. Chukua mpunga wa azam manake simba na yanga mwaka huu likizo time!!!
Kusema azam haitwai ubingwa leo,ni sawa na kubet eti mzee akilimali hatoropoka tena.
Gemu inayotolewa macho sana ni hii ya azam fc na mcc pale sokoine mbeya ni noma sana..
MSIMAMO LIGI KUU BARA
# Team. MP P
1 Azam 24 56
2 Young Africans 24 52
3 Mbeya City. 24 46
4 Simba 24 37
5 Kagera Sugar 24 34
UFUNGAJI.
1. Amis Tambwe magoli 19
2 . Kipre Tchetche magoli 14 3.Mrisho Ngassa magoli 12
Hamis Kizza magoli 12
4 . Didier Kavumbagu magoli 11
more updates to follow.
gemu ya leo ni ushindi tu hakuna jinsi yoyote..