Updates mpambano wa Mbeya city na Simba

Updates mpambano wa Mbeya city na Simba

Nilikuwepo sokoine kuangalia mechi. mcc wanabebwa sana na refa, hususani kipindi cha kwanza refa wa kati alikuwa anaachia rafu za mcc, ile penalti haikuwa ya halali, mshika kibendera mmoja alikuwa anatoa offside dhidi ya simba zisizokuwa za halali.

Maneno ya mkosaji. Umeandika kishabiki mno kiasi kwamba sipati taabu kufahamu wewe ni wa timu gani.
 
Nilikuwepo sokoine kuangalia mechi. mcc wanabebwa sana na refa, hususani kipindi cha kwanza refa wa kati alikuwa anaachia rafu za mcc, ile penalti haikuwa ya halali, mshika kibendera mmoja alikuwa anatoa offside dhidi ya simba zisizokuwa za halali.
Maneno yako tu yanaonesha wewe ni Simba....
Mtalalamika sana mwaka huu...

Mbina round ya kwanza mmefunga magoli mengi tu ya penati...Nazo mlikuwa mnapewa?

Dakika 15 za mwisho mlikuwa na hali mbaya kweli....
 
Mechi ya wiki iliyopita kati ya mcc na mtibwa, maamuzi ya utata kutoka kwa mwamuzi kuipendelea mcc yalikuwepo kama ilivyokuwa jana. Michezo inayofuatia (itakayochezwa sokoine) kati ya mcc dhidi ya oljoro, rhino, prisons, azam na mgambo ikiwezekana nitaenda kuiangalia, nawe pia uifuatilie utaona.

Huku mbeya kuna hamasa kubwa ya kuishabikia hii timu kimkumbo. Hata uwanjani mashabiki wa mcc walikuwa wanashangilia pale tu timu yao ilipofunga au ilipokuwa inashambulia, muda mwingi walikuwa kimya.

kuhusu dakika 15 za mwisho ni kwamba mcc wanaonekana wana mazoezi/pumzi na kuna muda kipindi cha pili walikuwa wanategemea mashambulizi ya kushtukiza, hivyo baada ya ssc kuchoka nao wakawa wanaogopa kushambulia wakichelea kushtukizwa..................

Hata hivyo mcc inabidi waimarishe mawinga wao wawe wanarudi kusaidia full backs. Kwa mfano kipindi cha kwanza winga wa kushoto alikuwa harudi haraka kumsaidia beki tatu kumzuia singano. Pia kipa wa mcc siyo mzuri kwenye mipira ya juu na vilevile ana kimo kifupi kwa kuwa kipa ni kama 5ft7ins-5ft8ins
 
Back
Top Bottom