FT: Ligi Kuu Tanzania Bara | Mbeya City 1-1 Simba SC | Uwanja wa Sokoine 23/11/2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Kama si mbiringe bila shaka ni patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Novemba 23, 2022 ambapo aabishi Mbeya City wanawakabili wekundu wa Msimbazi Simba SC kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.

Hii ni zaidi ya mechi na ushindani wa kutosha ndani ya dimba, na kutokana na kumbukumbu ya mwisho kwa Simba kugusa nyasi katika Uwanja wa Sokoine alipoteza kwa bao 1-0 na kuwapa alama tatu Mbeya City.

Kocha Msaidizi wa Mbeya City Anthony Mwamlima amesema kuwa wamefanya maandalizi tofauti na mechi nyingine.

"Sisi kama Mbeya City tumejiandaa kucheza na timu kubwa ambayo inashiriki mashindano ya kimataifa na unapojiandaa kucheza na Simba SC ni tofauti na unapojiandaa kucheza na Polisi au Singida, hivyo tunaingia kwa tahadhari hiyo kwa kuwaheshimu huku tukiamini kupata matokeo ya ushindi". Amesema Kocha Mwamlima

Naye Kocha wa Simba SC Juma Mgunda amesema kuwa wamejiandaa vizuri kwa mapambano.

"Tunawaheshimu Mbeya City, ni timu nzuri na imejipanga vizuri, lakini sisi tumejipanga kuhakikisha tunashinda, tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani lakini tupo tayari kwa mapambano". Amesema Kocha Mgunda

Kauli ya Kocha wa Mbeya City kuwa maandalizi yao kwa Simba SC ni tofauti na mechi nyingine ina maana gani? Dakika 90 za jasho na damu kufahamika.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: 00 Alasiri. Usikose yatakayojiri kutoka kwa jopo zima la JF!

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

=======

00' Naaam mpira umeanza Uwanja wa Sokoine | Mbeya City 0-0 Simba SC.

03' Simba SC wamepata Kona ambayo haikuzaa bao, baada ya shuti la Mzamiru kutoka sentimita chache ya lango la City.

05' Golikipa Manula yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kupata rabsha, ameinuka mpira unaendelea.

10' Sabilo na Henock kwenye papatu papatu, lakini refa aliamuru faulo kuelekea City

14' Mzamiru Goooooooooooooaaal gooal, Mzamiru anaweka kambani bao la kwanza akipokea pasi murua kutoka kwa Bocco.

17' Tariq anafanya faulo kwa Okrah, inapigwa kulee lakini City wanazuia

22' Hassan wa City anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Phiri

Free Kick kuelekea City anapiga Okrah lakini mpira unababatiza mabeki

City wanamiliki mpira kwenye eneo lao, hata hivyo Simba wanafanya faulo, wakijaribu kuwazuia

29' Awadh anapiga kichwa lakini mpira unatoka nje na kuwa goal kick

Tariq almanusura afunge bao, kama si uimara wa golikipa Manula.

Sangija anatoa nje mpira na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao kwa Simba

35' Bocco anakosa nafasi nzuri ya kufunga baada ya kumlamba chenga beki wa City

39' Simba wamepata Kona ambayo haikuzaa bao, mpira wa Kichwa kutoka kwa Mkude unapaa nje ya lango la City.

41' Sabilo anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali kuelekea lango la Simba SC

43' Free Kick kuelekea City anapiga Chama lakini golikipa wa City anaruka na kupangua mpira na kuwa wa kurusha.

45+1' Kuelekea kuwa mapumziko ambapo Simba wapo mbele ya bao moja.

HT: Mbeya City 0-1 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Sokoine, hakuna mabadiliko kwa wachezaji.

Phiri anakosa nafasi nzuri ya kufunga, alizongwa na mabeki wa City

49' City wanapata Kona ambayo haikuzaa bao, Simba wanaokoa

53' Ameingia Kibu na ametoka Okrah, wakati huo anafanya jaribio la kwanza kwa City, ni Kona

57' Ameingia Mwaipasi kuchukua nafasi ya Ng'odya

City wanafanya shambulizi lakini, wanashindwa kumaliza mpira wa mwisho kwenye wavu.

Mzamiru anapiga Krosi hafifu na mpira unatoka nje na kuwa goal kick

Tariq anapiga Krosi lakini hakuna MTU wa kuunganisha mpira ule, ilikuwa nafasi nzuri

70' Hassan Nassor anaonyeshwa Kadi ya Njano upande wa City

Henock anapiga kichwa na mpira unagonga Mlingoti, ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga bao la pili.

City wanafanya shambulizi kali sana, lakini golikipa Manula anadaka, refa aliamuru Kona ambayo haikuzaa bao

76' Goooooooooooooaaal gooal |City wanasawazisha kupitia kwa Tariq Seif

Mbeya City 1-1 Simba SC

Free Kick kuelekea City anapiga Hussein lakini wanaokoa hatari ile

85' Ametoka Bocco na ameingia Kyombo upande wa Simba

89' Ametoka Phiri na ameingia Sakho upande wa Simba

90+4' kuelekea kumalizika kwa mchezo

Simba wanamiliki mpira, lakini City wanazuia kwa kuondosha hatari ile

Sabilo anaonyeshwa Kadi ya Njano dakika hizi za nyongeza

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo City na be Simba SC wametoshana nguvu kwa kufungana moja kwa moja

FT: Mbeya City 1-1 Simba SC
 
Hakuna sare kwenye mechi kumi kati ya Simba SC na Mbeya City katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
20221123_142720.jpg
 
Sixtus Sabilo anatakata sana msimu huu ndani ya kikosi cha Mbeya City

Ni wa kuchungwa mno ndani ya dimba
 
Captain fantastic baada ya kupata Hat-trick dhidi ya Ruvu Shooting, leo kuendeleza moto ule ule?
instagram_1669193985820.jpg
 
Hii timu ni yakuonea huruma.. hebu oneni wachezaji Wao wakutumainiwa wa first eleven Mkude, Onyango, Mzamiru, boco.. .....
kama mambo yakiwa magumu Kwa Hawa walioanza hebu tazama walioko hapo benchi wakuja kuokoa jahazi utacheka sana..
Eti Kuna Kibu, akpan,Nyoni,Gadiel,ouatara,kyombo,
Kennedy,...

Kweli Hawa ndugu zetu tuwaombee angalau wapate akili za kufanya usajili mzuri... Wamejaza lundo la wachezaji takataka ambao hata hawawezi pata namba kmc/kagera sugar/singida big stars
 
Back
Top Bottom