mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,793
- 7,165
Hawa sio Dagaa ila walitumia njia mbaya, wangetumia kama ya ile ya KAGODA mambo yangekuwa shwari
Mambo ya sinema hayapo hapa, angalia wenzako wameanza na Mubarak then wasaidizi wake ndio wamefuata, mwendo ndio huo.Ni lazima usafishe mtandao kwa kuanza na dagaa. Hata sinema huwa tunaona kwanza wanamalizwa maadui halafu ndio anasakwa kubwa la maadui. Uliona sinema ipi "gang leader" akamalizwa mwanzo, si sinema itakwisha kabla haijaanza.
Pesa iliyoibwa EPA ni zaidi bil 40 tunahangaika na 2bil. wako wapi walioiba bil 20?
Asalamaleku walah
Aliyekulamba billion mbili unamwita kidagaa? kwi kwi kwi teh teh teh!
Aliyekulamba billion mbili unamwita kidagaa? kwi kwi kwi teh teh teh!
Tatizo lako unashindwa kuelewa kuwa mabunge yetu ndio yanayoweka hizi sheria na si mimi wala wewe. Labda mwenzangu ni mbunge.
Sheria zetu na nyingine nyingi duniani, zinazotungwa na watu (wabunge) zimejaa kulindana, hapo bungeni wale unaowaona usifikiri kuwa wako pale kwa maslahi yako wewe zaidi, wako pale kwa maslahi yao na kujilinda wao kwa wao, si wa upinzani wala wa chama tawala.
Hivi, umeshajiuliza ni kwanini wanaowaua waiba simu hawachukuliwi hatua? nini kinachowalinda? utakuta ni wewe mmoja wapo unaowalinda hao wauaji wa mitaani, akitokea mwizi akauliwa na wewe upo kwenye eneo, unajuwa kabisa ni fulani na fulani ndio waliomuuwa, lakini unakaa kimya huendi kuwashitaki wala kupeleka ushahidi. Halafu leo uozo huohuo unautolea mfano?
Wizi upo, haukuanza leo Tanzania hii, cha kutia moyo ni kuwa angalau kwa sasa tunaona hao wizi wa "EPA" wakifikishwa mahakamani. Kumbuka kuwa hii EPA ni madudu ya awamu iliyopita na walikuwepo watunga sheria pia, walikuwa wapi? mpaka aje Kikwete ndiyo ayaibuwe na kuisuka PCCB upya?, hivi kabla ya PCCB kulikuwa hakuna hivi vyombo vya kuzuwia rushwa? vilikuwa wapi? vilifanya nini? vilimfikisha nani mahakamani? majibu ni rahisi kabisa. Hakuna.
Leo hii yule anaechapa kazi na kuyaibuwa yote haya na kuchukuwa hatua stahiki za kubadilisha sheria za kulindana na kufumuwa mitandao ya huu wizi na mwingine ndiye anaonekana hafai. Ajabu sana.
Kumbuka kuwa sheria zimebadilishwa sana kipindi cha Kikwete zimeziba mianya mingi iliyopo awali na pia ukumbuke kuwa hivyo ni vita endelevu, ni uozo ulioota mizizi na kuuvunja na kuuondoa huo uozo kwa siku moja ni ndoto. Lakini matumaini yapo na ni mema sana na tumeona nia safi ya Kikwete katika awamu yake ya uongozi.
Walio husika ni CCM sema hao ndiyo walio tumika....
....Na wanaogopa kumtaja MWIGULU NCHEMBA kama mhusika mwenzao
kwani hao ndo walihusika na EPA?
EPA ilikuwa na wezi wa aina mbili yaani mwizi msafi na mwizi mchafu,msafi u huru kwa usafi wake ila mchafu jela.Eh nyinyiemu na hukumu zenu za macho.
kwani hao ndo walihusika na EPA?