Update ya askari wa JWTZ aliyeshushiwa kipigo

Dogo G

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2018
Posts
1,052
Reaction score
440
Wandugu habari,

Juzi nilileta taarifa kuhusiana na mwanajeshi wa jwtZ kupewa kichapo kikali na vijana wa bodaboda punde baada ya kumdhulumu yule kijana 1500 tu ambayo ilikuwa ni kwaajili ya malipo ya huyo boda kwa hiyo huduma.

Sasa jana inasemekana kiongozi wa kambi ya mafinga mwenye cheo cha luteni(jina halijafahamika) alikwenda kituo cha polisi mafinga kwaajili ya kuzungumza na mkuu wa polisi mafinga(OCD) ambapo pia alimshukuru kamanda huyo kwa kuwa police waliwahi mapema kumuokoa huyo kijana kwasababu bila hivyo angekuwa ni hayati.

Katika mazungumzo hayo,inasemekana yule luteni amefedheheka sana na kitendo kilichotendwa na askari wake kwa kufanya utovu wa nidhamu kudhulumu shillingi 1500 kwa raia kwani kwa namna moja anachafua sifa ya jeshi la wananchi(JWTZ) lakini amesema askari huyo ambaye ni private atahojiwa zaidi hali yake kimwili ikitengemaa kwani bado yupo nyumbani akiugulia na uchunguzi unafanyika ikibainika kosa ni lake sheria za kiuaskari zitafwatwa.

Source:ebony

MY TAKE:sasa nimeamini hii awamu nyingine na zama zimebadilika,mimi nilifikiri wangekwenda kulipiza kisasi kwa bodaboda wote badala yake kaenda police kisheria Zaidi ndio kwanza anasema anafanya UCHUNGUZI.kweli sasa uonevu umekwisha
 
Wandugu habari,

Juzi nilileta taarifa kuhusiana na mwanajeshi wa jwtZ kupewa kichapo kikali na vijana wa bodaboda punde baada ya kumdhulumu yule kijana 1500 tu ambayo ilikuwa ni kwaajili ya malipo ya huyo boda kwa hiyo huduma.

Sasa jana inasemekana kiongozi wa kambi ya mafinga mwenye cheo cha luteni(jina halijafahamika) alikwenda kituo cha polisi mafinga kwaajili ya kuzungumza na mkuu wa polisi mafinga(OCD) ambapo pia alimshukuru kamanda huyo kwa kuwa police waliwahi mapema kumuokoa huyo kijana kwasababu bila hivyo angekuwa ni hayati.Katika mazungumzo hayo,inasemekana yule luteni amefedheheka sana na kitendo kilichotendwa na askari wake kwa kufanya utovu wa nidhamu kudhulumu shillingi 1500 kwa raia kwani kwa namna moja anachafua sifa ya jeshi la wananchi(JWTZ) lakini amesema askari huyo ambaye ni private atahojiwa zaidi hali yake kimwili ikitengemaa kwani bado yupo nyumbani akiugulia na uchunguzi unafanyika ikibainika kosa ni lake sheria za kiuaskari zitafwatwa.

kulikuwa hakuna jinsi ilibidi afanye hivyo. vinginevyo ingekuwa mmeingia kwenye timing zao tungesikia mengine
 
Huyo Kamanda Wa Jeshi Hakutaka Makubwa, Vinginevyo Bodaboda Wangeipata Fresh Maana Wanajifanya Wajanja Sana Kwa Kuchangia Mtu. Bodaboda Ni Wa Kuangalia Sana Kwa Jicho La Tatu Maana Ni Kikundi Sensitive Sana Kutekeleza Uhalifu Na Kujichukulia Sheria Mkononi
 
Siku hiz mambo ya kupiga raia hovyo yanapungua japo bado yapo ila sio kama zamani! Mambo yamebadilika kiasi, ila ingekuea zamani hao bodaboda wangepata tabu sana
 
Ameonyesha ukomavu katika utu. Anastahili pongezi na kuwa mfano wa kuigwa. Kubwa juu.
 
Wandugu habari,

Juzi nilileta taarifa kuhusiana na mwanajeshi wa jwtZ kupewa kichapo kikali na vijana wa bodaboda punde baada ya kumdhulumu yule kijana 1500 tu ambayo ilikuwa ni kwaajili ya malipo ya huyo boda kwa hiyo huduma.

Sasa jana inasemekana kiongozi wa kambi ya mafinga mwenye cheo cha luteni(jina halijafahamika) alikwenda kituo cha polisi mafinga kwaajili ya kuzungumza na mkuu wa polisi mafinga(OCD) ambapo pia alimshukuru kamanda huyo kwa kuwa police waliwahi mapema kumuokoa huyo kijana kwasababu bila hivyo angekuwa ni hayati.Katika mazungumzo hayo,inasemekana yule luteni amefedheheka sana na kitendo kilichotendwa na askari wake kwa kufanya utovu wa nidhamu kudhulumu shillingi 1500 kwa raia kwani kwa namna moja anachafua sifa ya jeshi la wananchi(JWTZ) lakini amesema askari huyo ambaye ni private atahojiwa zaidi hali yake kimwili ikitengemaa kwani bado yupo nyumbani akiugulia na uchunguzi unafanyika ikibainika kosa ni lake sheria za kiuaskari zitafwatwa.

Source:ebony

MY TAKE:sasa nimeamini hii awamu nyingine na zama zimebadilika,mimi nilifikiri wangekwenda kulipiza kisasi kwa bodaboda wote badala yake kaenda police kisheria Zaidi ndio kwanza anasema anafanya UCHUNGUZI.kweli sasa uonevu umekwisha
Awamu na uonevu wapi na wapi?
 
Bodaboda Ni Kikundi Tulivu Na Kinafanya Kazi Zao Kwa Amani Tu. Lakini Ni Vikundi Hatari Sana Kujichukulia Sheria Mkononi Na Kufanya Uhalifu. Wengi Wao Ama Walikuwa Vibaka Au Majambazi Au Shughuli Zingine Tata, Ndiyo Maana Huwa Hawana Huruma Kumfanyia Uhalifu Mtu Anayejiingiza Vibaya Kwenye Anga Zao. Akigongwa Bodaboda Kwa Bahati Mbaya Hawachelewi Kulipiza Kisasi Palepale Mara Mbili Yake. Wamekaa Mkao Wa Kihunihuni Tu. Bodaboda Ni Mojawapo Ya Biashara Ya Kihuni Mjini. Ina Mbilinge Nyingi Barabarani Kama Kuchomekeana Na Kuhatarisha Usalama Barabarani, Hawajali Zebra Na Alama Zingine Za Maonyo Barabarani. Ni Kero Tupu Barabarani
 
Hio nidhamu inatoka juu kushuka chini. Mambo yanabadilika taratibu.
 
Back
Top Bottom