Update: Lema kufikishwa Mahakamani Jumatatu

Bramo

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Posts
13,242
Reaction score
10,227
MAMBO yamezidi kumwendea kombo Mbunge wa Arusha Mjini, (Chadema) Godbless Lema baada ya Jeshi la Polisi kutangaza rasmi kwamba itamfikisha Mahakamani, siku ya Juma tatu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amema kwamba Mbunge huyo hawezi kuachilia huru kwa sababu mashtaka dhidi yake yameshakamilika na atafikishwa Mahakamani siku ya Juma tatau.

"Hatuwezi kumwachia kwa sababu anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili"alisema Sabas.

Wakati Kamanda huyo akitoa msimamo huo, taarifa za ndani ya Jeshi hilo zinaeleza kwamba Mbunge huyo amehojiwa kwa zaidi ya saa nane sasa na bado yuko katika chumba maalum kwa mahojiano zaidi na maofsa wa Polisi huku akitakiwa kuonyesha ujumbe mfupi wa vitisho aliyodaiwa kuwa ametumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.

Katika hatua nyingine Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Arusha, kimekuwa na kikao kirefu kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo na kwamba ajenda kubwa inayojadiliwa ni tukio zima la vurugu zilizotokea katika Chuo cha Uhasibu mkoani humo.

Lema alikamatwa usiku wa kuamkia leo baada ya Askari wa Jeshi la Polisi kumfuata nyumbani kwake na kuzingira nyumba yake kabla ya zoezi la kumchomoa ndani ya nyumba hiyo kufanyika.

Mbune huyo anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuchochea vurugu katika chuo hicho baada ya kutokea mauaji ya Mwanafunzi Henry Koga aliye uawa kwa kuchomwa kisu juzi akirejea chuoni hapo kutoka kwenye matembezi yake, hata hivyo haijajulikana mara moja sababu za kuawa kwa mwanafunzi huyo wala watuhumiwa hawajakamatwa.

My Out Look:
Nazidi kuyasadiki Maneno ya Rafiki yangu SSP Chuwa kuwa Tatizo sio Mulongo.

Yeye ana execute to Matakwa ya Mkulu Dhidi ya Lema.

Ile Issue ya Lema kumpa Live Mkulu kuwa analea Udini imemchoma sana Mkulu.

Rafiki Yangu SSP Chuwa Akaongeza, "CCM ni Wepesi Mno na Weupe Suala linapofika Mahakani"

Wao wana Mamlaka na Fedha, Lema ana Mungu

===================
Kinachojiri Mahabusu
===================

 
Hivi kwanini watanzania tusifuate mfano wa wananchi wa Misri,Tunisia na Libya?

Kuna haja gani ya kuendelea kuwavumilia hawa watawala wanaofanana na madikteta?

Badala ya mimi kutafuta hela niisaidie familia yangu eti nikaandamane . Huu ni upuuzii uliotukuka . Wajinga ndio wafuate mawazo yako .
 
Hii nayo picha nyingine tena kiingilio ni masikio yako na macho tu siasa mchezo mchafu
 
Hivi kwanini watanzania tusifuate mfano wa wananchi wa Misri,Tunisia na Libya?

Kuna haja gani ya kuendelea kuwavumilia hawa watawala wanaofanana na madikteta?

jaribu uone watakavyosigina guu lako na hapo lema na chalema yake hawatokusaidia lolote..
 
Badala ya mimi kutafuta hela niisaidie familia yangu eti nikaandamane . Huu ni upuuzii uliotukuka . Wajinga ndio wafuate mawazo yako .
thinking apacity yako imeishia hapo.tafuta hela.
 
Badala ya mimi kutafuta hela niisaidie familia yangu eti nikaandamane . Huu ni upuuzii uliotukuka . Wajinga ndio wafuate mawazo yako .

Hujui kuwa kama system ikiwa nzuri hata hauitaji kutoa jasho ili kufanikiwa? . Jiunge na wenzako uboreshe maisha yako na ya kizazi chako.Hii ni kama uko sincere na wewe siyo imposter!
 
Kuna kipindi magereza nyingi zilikarabatiwa na kutiwa mbwembwe za ajabu na magari mazuri,kumbe issue ilikuwa kwa ajiri ya watu wa EPA na kina LIYUMBA,sasa basi waandae mengine bila hata kuyapamba sana kwa ajiri ya sisi wafuasi wa cdm na wananchi wasiopenda kuonewa hovyo....fikiria Lema katoa simu yake nakumpigia mkuu wa mkoa kuwa njoo chuoni kuna tatizo, leo yeye ndio anapelekwa mahakamani? na je yule aliefika pale na kutumia kauli mbovu za mabavu na badae kumtumia lema ujumbe wa vitisho nani mwenye makosa?
 
Mungu ni mwema. Yanamwisho haya hata kama yataexist kwa miaka 2000, mubaraka chali, osama chali, gadafi chali, sadam hussein chali, charles teilor chali..........
 
mwisho wa ubaya ni aibu the hague ipo kwa ajili ya watu kama JK na Said Mwema.hivi tangu lini mkuu wa mkoa anakuwa mpelelezi,jaani watu kama wakina RAMA walio husika na utekaji wa kina kibanda bado wapo huru,mtetezi wa raia anaswekwa rumande,hata mandela ali wekwa kizuizini miaka 27 kwa makosa ya ugaidi wa kubambikwa,yote yana mwisho watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…