Update:KUANDAMA KWA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.

Update:KUANDAMA KWA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.

Status
Not open for further replies.
Wanawazuona hugawanya saumu (kufunga) katika mafungu matatu:

1-Kufunga kiujumla:
Kujizuia (kufunga) kwa kuacha chakula,vinywaji na kumuingilia mke ; hii ni aina ya fungo (saumu) ambayo kila
mwenye kufunga huitekeleza na ndiyo ambayo inajulikana sana.

2 -Kufunga maalum:
Ni kujizuia kimacho (mfungaji hatazami maovu kama vile wanawake n.k), masikio (hasikizi uovu kama
usengenyaji ) miguu (haendi kwa miguu yake kwenye maovu kama vile wizi n.k), mikono (haibi), mdomo (hasemi uongo) n.k
Kama ilivyopokewa katika hadith na Imam al-Bukhari, Tirmidhee, Nasaee kuwa Mtume salalhu alayhi wasallam anasema (tafsiri ya harakaharaka) "Allah hahitaji saumu ya mtu asieacha uongo na kutenda kutokana na uongo wake"

3-Kufunga kuliko maalum na khasakhasa:
Huu ni ufungaji wa mtu ambaye anafunga kimoyo, yaani moyo wake anauepusha na mambo yote ya kidunia, hafikirii isipokuwa
yale tu yanayompendeza Allah; kama vile kuzitafakari aya za Quran, dhikri (nyiradi) huku anayatafakari maneno yale ya nyiradi.

Tujitahidini Waislamu tufunge aina zote hizo tatu kiasi cha uwezo wetu "Basi mcheni Mwenyezi Mungu kiasi muwezavyo...(Quran 64:16)
 
Ijuma5 Inshallah is the first Ramadhan dei

Nimejaribu kuweka dondoo kadhaa tujadili kama watu wenye upeo wa kujifunza na kuuelewa vema uislamu, lakini wale wenye kuzoea mipasho naona wanakimbia maana wangependa tuendelee na mipasho badala ya mambo muhimu ya kuujua uislamu. Jamani tuwe tunajiweka mazingira ya kujua zaidi mambo muhimu ya dini zetu badala ya mtindo wa mipasho ya vijiweni.

Kuna kila dalili ya wengi kushabikia bila kuujua vema uislamu, ukisoma kwa makini mambo mhimu utakuja kugundua mengi mazuri ambayo hayaongelewi na hawa wapiga vuvuze wa kushabikia kama mpira wa mguu.
 
The Islamic year has twelve months that are based on a lunar cycle. Allah says in the Qur'an:"The number of months in the sight of Allah is twelve (in a year) - so ordained by Him the day He created the heavens and the earth...." (9:36).
"It is He Who made the sun to be a shining glory, and the moon to be a light of beauty, and measured out stages for it, that you might know the number of years and the count of time. Allah did not create this except in truth and righteousness. And He explains His signs in detail, for those who understand" (10:5).
And in his final sermon before his death, the Prophet Muhammad said, among other things, "With Allah the months are twelve; four of them are holy; three of these are successive and one occurs singly between the months of Jumaada and Sha'ban."
Islamic months begin at sunset of the first day, the day when the lunar crescent is visually sighted. The lunar year is approximately 354 days long, so the months rotate backward through the seasons and are not fixed to the Gregorian calendar. The months of the Islamic year are:
1. Muharram ("Forbidden" - it is one of the four months during which it is forbidden to wage war or fight)
2. Safar ("Empty" or "Yellow")
3. Rabia Awal ("First spring")
4. Rabia Thani ("Second spring")
5. Jumaada Awal ("First freeze")
6. Jumaada Thani ("Second freeze")
7. Rajab ("To respect" - this is another holy month when fighting is prohibited)
8. Sha'ban ("To spread and distribute")
9. Ramadan ("Parched thirst" - this is the month of daytime fasting)
10. Shawwal ("To be light and vigorous")
11. Dhul-Qi'dah ("The month of rest" - another month when no warfare or fighting is allowed)
12. Dhul-Hijjah ("The month of Hajj" - this is the month of the annual pilgrimage to Makkah, again when no warfare or fighting is allowed)



Ngoja watakuja weledi litajadiliwa.
 
Kuna taarifa Bakwata wanasema leo ni tarehe 29 shabani sasa tuweni makini na hii taasisi msijeacha kufunga kesho kwa sababu yao.
 
muslim-care1-450x337.jpg


Tunahitaji kupata ilmu ya uislamu tuelimike, wataalamu tujuzeni jamani.

teh teh hapa ulikuwa unamaanisha nini?
 
Kuna taarifa Bakwata wanasema leo ni tarehe 29 shabani sasa tuweni makini na hii taasisi msijeacha kufunga kesho kwa sababu yao.

lakin BAKWATA c ndio source nzuri zaid kwa waislam? Au inakuaje hapo, nauliza tu
 
Nimejaribu kuweka dondoo kadhaa tujadili kama watu wenye upeo wa kujifunza na kuuelewa vema uislamu, lakini wale wenye kuzoea mipasho naona wanakimbia maana wangependa tuendelee na mipasho badala ya mambo muhimu ya kuujua uislamu. Jamani tuwe tunajiweka mazingira ya kujua zaidi mambo muhimu ya dini zetu badala ya mtindo wa mipasho ya vijiweni.

Kuna kila dalili ya wengi kushabikia bila kuujua vema uislamu, ukisoma kwa makini mambo mhimu utakuja kugundua mengi mazuri ambayo hayaongelewi na hawa wapiga vuvuze wa kushabikia kama mpira wa mguu.

Nimejaribu kupitia posts zako zote zinazohusiana na kalenda na matukio mbalimbali ya kiislamu sijaelewa unataka kijadiliwe nini?
 
lakin BAKWATA c ndio source nzuri zaid kwa waislam? Au inakuaje hapo, nauliza tu

Muislamu yeyote popote duniani akitoa taarifa za kuonekana kwa mwezi tunatakiwa kufunga au kufungua. Kinachotakiwa ni kuhakikisha taarifa zake na hii ndio ilikuwa desturi ya mtume Muhammad s.a.w na maswahaba zake. Tunawaheshimu na kuwatii viongozi wetu wakituamrisha yaliokuwa mema na kutukataza mabaya na siyo wakituamrisha maovu na kutukataza mema likiwemo hili la funga ya mwezi wa ramadhani. Kwasasa Bakwata inakosa uaminifu kwa waislamu wengi kwa kuwa imekuwa inababaisha waislamu kati mambo mengi. Mtume asema fungeni/fungueni kwa kuonekana kwa mwezi. Na sio kuamrishwa na mwanadamu kwa matashi yake.
 
Mashalah, ramadhan imeingia, Alhamdulilah. Mwezi umeonekana nami nimeuona.
 
Alhamdulillah ala kulli Hal. Ramadhan Kareem
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1373367108576.jpg
    uploadfromtaptalk1373367108576.jpg
    37.8 KB · Views: 83
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom