Update:KUANDAMA KWA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.

Status
Not open for further replies.
Wanawazuona hugawanya saumu (kufunga) katika mafungu matatu:

1-Kufunga kiujumla:
Kujizuia (kufunga) kwa kuacha chakula,vinywaji na kumuingilia mke ; hii ni aina ya fungo (saumu) ambayo kila
mwenye kufunga huitekeleza na ndiyo ambayo inajulikana sana.

2 -Kufunga maalum:
Ni kujizuia kimacho (mfungaji hatazami maovu kama vile wanawake n.k), masikio (hasikizi uovu kama
usengenyaji ) miguu (haendi kwa miguu yake kwenye maovu kama vile wizi n.k), mikono (haibi), mdomo (hasemi uongo) n.k
Kama ilivyopokewa katika hadith na Imam al-Bukhari, Tirmidhee, Nasaee kuwa Mtume salalhu alayhi wasallam anasema (tafsiri ya harakaharaka) "Allah hahitaji saumu ya mtu asieacha uongo na kutenda kutokana na uongo wake"

3-Kufunga kuliko maalum na khasakhasa:
Huu ni ufungaji wa mtu ambaye anafunga kimoyo, yaani moyo wake anauepusha na mambo yote ya kidunia, hafikirii isipokuwa
yale tu yanayompendeza Allah; kama vile kuzitafakari aya za Quran, dhikri (nyiradi) huku anayatafakari maneno yale ya nyiradi.

Tujitahidini Waislamu tufunge aina zote hizo tatu kiasi cha uwezo wetu "Basi mcheni Mwenyezi Mungu kiasi muwezavyo...(Quran 64:16)

Jazakallah kheir ustadh Sideeq kwa darasa muhimu!
 
Last edited by a moderator:
Mwezi mtukufu ukoje?mbona naona ndoa nyingi sana au ndo mwezi mtukufu?
Mkuu imani ni kuamini, wewe sio wanaoamini waachie wenyewe. Mbona wapo wanaoamini ijumaa kuu nini tofauti na ijumaa zingine?
 
Naam,
Ramadhani imeshaingia alhamdulilah kubwa tujitahidi kuzidisha ibada ili kufikia lengo lake ambalo ni uchamungu.
 
Wanawazuona hugawanya saumu (kufunga) katika mafungu matatu:

1-Kufunga kiujumla:
Kujizuia (kufunga) kwa kuacha chakula,vinywaji na kumuingilia mke ; hii ni aina ya fungo (saumu) ambayo kila
mwenye kufunga huitekeleza na ndiyo ambayo inajulikana sana.

2 -Kufunga maalum:
Ni kujizuia kimacho (mfungaji hatazami maovu kama vile wanawake n.k), masikio (hasikizi uovu kama
usengenyaji ) miguu (haendi kwa miguu yake kwenye maovu kama vile wizi n.k), mikono (haibi), mdomo (hasemi uongo) n.k
Kama ilivyopokewa katika hadith na Imam al-Bukhari, Tirmidhee, Nasaee kuwa Mtume salalhu alayhi wasallam anasema (tafsiri ya harakaharaka) "Allah hahitaji saumu ya mtu asieacha uongo na kutenda kutokana na uongo wake"

3-Kufunga kuliko maalum na khasakhasa:
Huu ni ufungaji wa mtu ambaye anafunga kimoyo, yaani moyo wake anauepusha na mambo yote ya kidunia, hafikirii isipokuwa
yale tu yanayompendeza Allah; kama vile kuzitafakari aya za Quran, dhikri (nyiradi) huku anayatafakari maneno yale ya nyiradi.

Tujitahidini Waislamu tufunge aina zote hizo tatu kiasi cha uwezo wetu "Basi mcheni Mwenyezi Mungu kiasi muwezavyo...(Quran 64:16)

Mungu akubariki na akulipe kila la kheri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom