Upatu, DECI, Babu Loliondo na sasa Edward Lowassa!

Upatu, DECI, Babu Loliondo na sasa Edward Lowassa!

Geresha hizi zilianzishwa na ccm,huwezi amini pamoja na 40% ya ardhi yetu kufaa kwa kilimo still tunaimport kila kitu,Viongozi wetu wanafanya biashara za shule na vyuo na hivyo kuua vyuo na shule za umma,

Semeni msemavyo,danganyeni muwezavyo-Kama mpaka hapa hamjaona ubaya wa ccm kwa nchi yetu na wadanganyika basi lets go for Lowasa maana hatuna namna nyingine
Ubaya wa CCM tunauona, tatizo tu ni kwamba tukimpa Lowasa na kundi lake mambo yatakuwa mabaya zaidi (kumbuka wengine katika kundi lake wako CCM wanasubiri tu akiwa Rais waanze madili)
 
Naona umeandika kitabu,katika andiko lako hukujiandaa,ndio maana umeandika andiko reeefu mpaka likapoteza maana
 
Kwa mtizamo wangu, kuwa na mtazamo kinyume na unavyofikir sio uvivu wa kufikiru. Watu wanadhani lowasa ndio fisadi na wengine wote wasafi. Lakini tunaona, huyu lowasa ameondolewa miaka nane iliyipita, na bado tumeuona ufisadi wa kutisha. Mfumo wetu wa kiserikali ndio unaotengeneza mazingira rafiki ya ufisadi. Sidhani kama kwenye tz hii kuna mtu ambaye ana mamlaka, kuanzia wenyevit wa vijiji mpaka juu ambaye ambaye alicho nacho alikipata kwa halali, na hiyo ni pamoja na wewe na mimi. Shida uoo katika mfumo wa serikali, kwa sababu mtu hafanyi ufisadi kwa jina lake, bali kwa cheo chake. Kwa hiyo ni rahis rais kwa cheo chake akalazimisga jambo, na kwa sababu hao anaowaagiza ni wateule wake, itabidi wafanye kulinda kibarua chake. Vivyo hivyo wazri mkuu, mawaziri, wakurugenzi, wakuu wa taasisi, wakurugenzi wa hamashauri ambao nao hawapo nyuma kuchakachua, kila mmoja kwa uwigo wa mamlaka yake, wamefanya hayo. Nijuavyo mimi, jambo lolote linaoopekwa bungeni, ni lazima lijadiriwe kwanza na baraza la mawaziri. Na hata bunge letu nalo linekaa kuupalilia ufisadi, kwa sababu miradi yote ya kifisadi ilipitihwa humo ili kutekelezwa, na tunaona hongo wanayopewa naserikali, pale kunapokuwa na uzito(rjea jairo), na kwa sababu mfumo unasababishwa na katiba, na ccm haiwezi kutoa katiba ambayo itawadhibit, na kumbuka kuwa shera na katiba hii ipo kwa ajili ya kutudhibiti sisi, ukionekana unainua shingo na kuulizia wakudhibit, haipo kwa ajili ya kuwadhibiti wao, ili kuwaweka kwenye nidhamu ta utawala, na kwa sababu ccm haiwezi kuleta katiba itakayowaondolea udhbiti wao juu ya watu, tunatakiwa tuitoe kwanza, na ndipo tuanze katiba ya kuwadhibiti, ambayo itawafanya wezi walipie wizi wao. Hakuna mwizi hata mmoja aliyefungwa, akina mramba walifungwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, na ambayo nadhani pia, serikali yote, kama baraza la mawaziri walikubaliana.
 
Mkuu huo wote ni sehemu ya uchafu uliosababishwa na ccm na serikali yake ndo maana Tumedhamilia kuichinjilia ccm mbali mwaka huu

Sasa boss wangu mbona kama vile tulielimishwa sana tukakaidi tukalizwa. Sasa mbona mnanirejesha tena kwenye ukaidi ule ule jamani? Sasa nikilizwa tena nitamlilia nani jamani? Mbona mnanichanganya
 
Sasa unakataa au unakubali kuwa tunashida ya udogo wa IQ? Kama unajibu la zaidi ya ndiyo au hapana tuambie hapa acha story

Wewe kama IQ yako ndogo shauri yako, mie yangu kubwa na sihitaji kuambiwa na wala sihitaji utafiti wa kunijuza kwamba ni kubwa. Hiyo IQ inayoona watanzania wana IQ ndogo kwenje jambo moja si ihitaji hata kuisikia, IQ kubwa ingekuja na tufanye nini na kutoa suluhisho la kitu bora cha kufanya.
 
Duu kweli una bonge la IQ. Naomba tu iwe genetically non dominant vinginevyo itakuwa hatareee
 
....wabongo bana..maneno meengi!!....woote hao awe magufuli ...awe lowassa wote sawa tu....hata kimaadili hawana tofauti...na kama ni shutma za ufisadi wote wanazo....na hakuna anachoweza kufanya magufuli atashindwa lowassa..wote ni wale wale tu....na historia zao kiutendaji zinaonyesha hivyo pia....

....kama ni maamuzi magumu wote wana historia hiyo...magufuli mnampamba na ujenzi wa mibarabara(japo haikai sana inajaa mashimo)....nae lowassa alishughulikia shule za kata ccm wanazotamba nazo leo...na pia alisitisha kampuni feki ya maji dar...na pia alishiriki kupeleka maji ya ziwa victoria kule shinyanga...

...hivyo nawashangaa sana wabongo kwa kejeli zao dhidi ya lowassa...maana kwangu mimi kwanini lowassa aonekane upatu na si magufuli???...kama ni upatu... kwangu hata magufuli anaweza kuwa upatu...kama ambavyo wabongo mlichezewa upatu wa maisha bora kwa kila mtanzania kwa miaka 10 iliyopita.....

....ccm acheni kejeli sikilizeni hoja....hili msipoangalia litawagharimu....namwona lowassa akipata point sana juu ya hili....maana yeye kimya...japo anajua maovu tele ya utawala wa ccm...kwangu mimi aliyebadiilika ni lowassa...kwa kuhama chama kinacholea mafisi na kuhamia kwenye matumaini ya mabadiliko...
 
ila angalia kama hapo amesema ukweli au sivyo
nasikitika kuona wachumia tumbo wanahangaika na lowasa pasipo kujuiliza kwa nn mtu huyu mwenye tuhuma lukuki anazidi kujipatia mashabaiki wengi kila siku japo anatukanwa na kudhalilishwa kila kona...jibu ni fupi tu..lowasa kaonyesha kuthubutu kaonyesha kweli anataka kuleta mabadiliko na ndio mana katoka ccm..nyie wote wenye tuhuma dhidi yako hamna anayekwenda kumshtaki ili kudhihirisha uchafu wake bali mnabaki kumshambulia tu...mnataka kutuamnisha kwamba lowasa ndo chanzo cha matatizo ya taifa hili..hovyo kabisa..raia wanampemda sababu wana imani nae kwamba atabadilisha maisha yao ndo mana hata kashfa zake hawaziangalii tena..ccmm nzima inejaa wala rushwa na bado wanaongeza wapya lkn hamna mtu anaesema....na kwa vile mnaona watanzania ni wajinga wasio kua na akili basi watamchagua lowasa na atawafanyia yale ambayo ninyi hamuwezi kufanya...kwa maandishi yako ww umeonyesha ni cccm halisi na woga wako ni lowasa..poleni sana hao wenye iq ndogo ninwengi na wanakwenda kufanya msichokitaka
 
tumekusoma na tumekuelewa na tulifundishwa na DR SLAA kuwa katiba mpya ndio mkombozi wetu kwa hiyo tunaiitaji

tumekusoma, na tumekuelewa kuwa LOWASSA NI FISADI na ndiye aliyeifilisi nchi au SHETAN kama alivyoitwa na DR. slaa
MUHIMU NI KWAMBA SOMO LA KATIBA ALILOTUPA SLAA tuliliamini na kuliunganisha na imani zetu za dini kwa hiyo hututenganishi nalo kwa maandiko ya kidunia

hapa ni lowassa tu, msiyemtaka sasa ataishika IKULU na mtanyoosha maelezo

Mwandishi anaanza kwa kusema samahani nilikosea nikaandika chama cha Zitto ni ADC badala ya ATC halafu aanaandika maandishi mareeeeeeeeeeeeeeeeeeeefu na akategemea watu watasoma taarifa za mwandishi anayekosea hata kiongozi wa chama, huo muda naupata wapi wa kusoma makala ya mwandishi mmoja peke yake. Nimeihifadhi, nitasoma mara baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu, ngoja niweke vizuri zaidi, nitasoma baada ya Rais mpya kuapa rasmi. Kwa heri.
 
Kwa hiyo huyu jamaa anataka nini, kama watanzania ni watu wa kufuata mkumbo safari hii wamefuata mkumbo wa Lowassa!

Mbona hasemi tulivyoburuzwa kwenye EPA, Richmond, Esrcow, mikataba ya madini na gas? Kwa nini kuburuzwa au kufuata mkumbo iwe na uzito [ale tu linapokuja urais wa Lowassa?

yale yale. kwani weweulifuata mkumbo kwenye mambo ya EPA, Richmond, Esrcow, mikataba ya madini na gas?

makala hii inahusu watanzania kuwa na akili ndogo (IQ ndogo) kiasi cha kudandia kila kitu kijacho bila kupima na kutafakari. sasa lini wananchi wa kawaida wa nchi hii walidandia maufisadi?
 
kama vipi hata magufuli ahame ccm aje kwenye mabadiliko nje ya ccm maana ccm ni gunia la mavi halibebeki linanuka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
viva Lowasa mzee wa maamuzi magumu!
Uuuuwi. Ajinyee Lowassa hadharani, kinyesi usingizie ccm
 
Tumekusikia. Huyo fisadi, na genge lake la wahuni kama Mbowe, ma Zero kama Sumaye na vichaa kama Lissu na Lema hawaioni ikulu
 
yale yale. kwani weweulifuata mkumbo kwenye mambo ya EPA, Richmond, Esrcow, mikataba ya madini na gas?

makala hii inahusu watanzania kuwa na akili ndogo (IQ ndogo) kiasi cha kudandia kila kitu kijacho bila kupima na kutafakari. sasa lini wananchi wa kawaida wa nchi hii walidandia maufisadi?

Umeona makala imejikita kwenye mifano ipi? Umeona makala imeegemea wapi? Japo nakubaliana na mantiki na maudhui ya hoja ya watu wengi kutokufukiri napingana na namna mwandishi alivyoamua kuchukua upande kwenye kwenye makala yake.

Kwa mujibu wa makala hii kama nikiamua kubaki kwenye mada kama unavyotaka wewe kwamba watanzania kua na IQ ndogo, kwa nini nisikubali kwamba ni kweli kwa CCM kuendelea kuwepo madarakani hadi leo?

Sasa hauoni hata kutokuchukua hatua zenye tija kwenye hizo kashfa nilizozitaja bado ni palepale tatizo la IQ ndogo? Sijajua hasa unapinga kitu gani na unakubali nini.
 
Kwa mtizamo wangu, kuwa na mtazamo kinyume na unavyofikir sio uvivu wa kufikiru. Watu wanadhani lowasa ndio fisadi na wengine wote wasafi. Lakini tunaona, huyu lowasa ameondolewa miaka nane iliyipita, na bado tumeuona ufisadi wa kutisha. Mfumo wetu wa kiserikali ndio unaotengeneza mazingira rafiki ya ufisadi. Sidhani kama kwenye tz hii kuna mtu ambaye ana mamlaka, kuanzia wenyevit wa vijiji mpaka juu ambaye ambaye alicho nacho alikipata kwa halali, na hiyo ni pamoja na wewe na mimi. Shida uoo katika mfumo wa serikali, kwa sababu mtu hafanyi ufisadi kwa jina lake, bali kwa cheo chake. Kwa hiyo ni rahis rais kwa cheo chake akalazimisga jambo, na kwa sababu hao anaowaagiza ni wateule wake, itabidi wafanye kulinda kibarua chake. Vivyo hivyo wazri mkuu, mawaziri, wakurugenzi, wakuu wa taasisi, wakurugenzi wa hamashauri ambao nao hawapo nyuma kuchakachua, kila mmoja kwa uwigo wa mamlaka yake, wamefanya hayo. Nijuavyo mimi, jambo lolote linaoopekwa bungeni, ni lazima lijadiriwe kwanza na baraza la mawaziri. Na hata bunge letu nalo linekaa kuupalilia ufisadi, kwa sababu miradi yote ya kifisadi ilipitihwa humo ili kutekelezwa, na tunaona hongo wanayopewa naserikali, pale kunapokuwa na uzito(rjea jairo), na kwa sababu mfumo unasababishwa na katiba, na ccm haiwezi kutoa katiba ambayo itawadhibit, na kumbuka kuwa shera na katiba hii ipo kwa ajili ya kutudhibiti sisi, ukionekana unainua shingo na kuulizia wakudhibit, haipo kwa ajili ya kuwadhibiti wao, ili kuwaweka kwenye nidhamu ta utawala, na kwa sababu ccm haiwezi kuleta katiba itakayowaondolea udhbiti wao juu ya watu, tunatakiwa tuitoe kwanza, na ndipo tuanze katiba ya kuwadhibiti, ambayo itawafanya wezi walipie wizi wao. Hakuna mwizi hata mmoja aliyefungwa, akina mramba walifungwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, na ambayo nadhani pia, serikali yote, kama baraza la mawaziri walikubaliana.

kipindi cha mwinyi kodi zilikuwa hazikusanywi ipasavyo - pamoja na mengine mishahara ya wafanyakazi ikawa shida. alipokujwa mkapa tatizo hili alilitatua kwa kiasi kikubwa. kiujumla mapungufu mengi ya kipindi cha mwinyi yalitatuliwa kipindi cha mkapa japo nae alikuja na yake. ninachotaka kusema ni kuwa marais hutofautiana uwezo. pia inategemeana na timu gani ameitengeneza imsaidie kuendesha nchi. uwezo wa rais na timu ya watu anayoitengeneza inaamua ufanisi wa kipindi cha huyo rais. kila rais anajitengenezea 'mfumo' wake

magufuli hata kama ana nia ya kuja kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hii muda huu si muda muafaka kwake kusema hayo. akija kushika madaraka ndio atakuwa na nafas nzuri kuliongelea suala hili. kwasasa inaweza kuwa kutafuta kuvurugana na chama chake - hiki si kitu anachokitaka kwasasa

historia inambeba zaidi magufuli kuwa atafanya vizuri zaidi kuliko mwingine. usiniambie lowasa atabadilika na kuwa mcha mungu kwa raslimaliza nchi hii. kama tangia akiwa kijana mpaka amezeeka alikuwa wa mwennendo fulani ni vipi leo hii useme atatubu yote aliyoyafanya kujianza upya? lowasa atabaki yuleyule. na hata magufuli atabaki yuleyule. sasa anza kulinganisha nani ni mpigaji hatari.

kama unafikiri wezi hawatakuwa wanafungwa kipindi hata cha magufuli unajidanganya. tusubiri tuone
 
Wewe kama IQ yako ndogo shauri yako, mie yangu kubwa na sihitaji kuambiwa na wala sihitaji utafiti wa kunijuza kwamba ni kubwa. Hiyo IQ inayoona watanzania wana IQ ndogo kwenje jambo moja si ihitaji hata kuisikia, IQ kubwa ingekuja na tufanye nini na kutoa suluhisho la kitu bora cha kufanya.

mbona rahisi, wewe huoni hapo? cha kufanya ni kumpiga chini lowasa. magufuli for presidency,

hatujawahi kuiona ukawa/ chadema au lowasa wakishika ikulu. ndio maana inakuwa rahisi kwa wengine kufikiri ccm ni mbovu kuliko ukawa/chadema. lakini kwa wenye kuiangalia kwa ukaribu ukawa/ chadema na lowasa wao tunaona giza tupu mbele, hamna matumaini. tunaona watu wasio na mtizamo mmoja. tunaona watu waliojikusanya kwenda ikulu tu. na tunakumbuka timu ya kikwete ya kwenda ikulu na miguvu na mihela iliyotumia kwenda ikulu na walichokifanya baada ya kwenda ikulu. tunaona watu wanaosema ikulu kwanza mipango baadae.
 
makala kama hizi ni ndefu sana. wengi wetu habari kama hizi hatuzisomi. halafu kwanza haziambatani na picha
 
mbona rahisi, wewe huoni hapo? cha kufanya ni kumpiga chini lowasa. magufuli for presidency

Nafurahi kwamba umeelewa hili jarida lengo lake ni nini hasa, na hapo ndio ilikua shida yangu. Huwezi kuongelea ufinyu wa kuwaza/IQ ndogo ya watanzania kwa kujikita na jambo moja tena ukionyesha kabisa upande wako kwamba humtaki Lowassa.
 
Toeni Precise Solution Watanzania wafanye nini sio Mnaponda tu Ukawa.

watanzania hawatakiwi kusema chochote kinachokuja sawa eti tumechoka na ccm. kwa ukawa huu na lowasa walivyo itakuwa bora mara 1000 ccm ibaki madarakani kuliko ukawa na lowasa wao kuwa madarakani. ccm ina mapungufu. lakini chini ya magufuli ccm na serikali yake vitakuwa bora na imara.

msidanganyike na maneno eti 'mfumo'. watu hutengeneza mifumo. na mifumo haiibi hela. watu ndio wanaiba hela. rais asiye na tamaa, msafi, mchapakazi, mwenye kujali nchi yake hawezi wachekea wezi na wala yeye mwenyewe hawezi kuwa mwizi.

tumchague magufuli
 
Nafurahi kwamba umeelewa hili jarida lengo lake ni nini hasa, na hapo ndio ilikua shida yangu. Huwezi kuongelea ufinyu wa kuwaza/IQ ndogo ya watanzania kwa kujikita na jambo moja tena ukionyesha kabisa upande wako kwamba humtaki Lowassa.

mwandishi wa makala ametoa sababu. amesema alichowahi kusema lowasa na hata sumaye (kauli zinazopingana - watu vigeugeu) na ameonyesha sababu zotolewazo kumpigia upatu na wanaomshabikia (ushabiki zaidi kwa mambo mazito kwa uongozi wa nchi - kutotafakari kwa kina mambo ).
 
Wewe umeyatoa wapi ya Magufuli for presidency?
 
Back
Top Bottom