Upangaji wa bei elekezi kwenye sukari una mapungufu makubwa

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,305
3,327
Leo serikali kupitia bodi ya sukari nchini imetangaza bei ya sukari kwa rejareja iuzwe Tsh1800/kg kote nchini,hili ni jambo jema kwani huu ni mkakati wakumlinda mlaji.

Lakini kwa mujibu wa bei hii elekezi ni dhahiri kuna mapungufu makubwa kwani aliewekewa mipaka ya bei ya uuzaji wa sukari ni mfanya biashara wa rejareja pekee wakati wafanya biashara wa jumla hawajawekewa mipaka mfuko mmoja wa sukari wawauzie bei gani wafanyabiashara wa rejareja.

Hapa panaweza leta mkanganyiko kwani kama serikali haitawawekea wafanyabiashara wa jumla bei elekezi kwa mfuko wa sukari, inawezekana kabisa wakawauzia wafanyabiashara wa rejareja kwa bei ambayo kama wao watauza sukari kwa tsh1800/kg wasipate faida.

Ni vema jambo hili likatizamwa vizuri.
 
Hii nchi inashangaza sana
kwamba serikali imeamua kuwalinda wenye viwanda kwa kuzuia sukari ya nje
lakini hao wenye viwanda wao wenyewe hawana mfumo mzuri wa kusambaza sukari yao
na ni wao wenyewe wanahifadhi sukari yao ili ipande bei

sasa serikali inabidi ipange bei na kutoa vitisho

serikali haijiulizi mbona hakuna bei elekezi ya beer?
 
Serikali ya CCM haipo kwa ajili ya wananchi, kwani mjui hilo?
Inaezekana kabisa mkurugenzi wa bodi ya sukari akawa ni CDM,kadi ya chama haipo kwenye viambatanisho vya CV wakati wa ajira,tutoe mawazo ili kama itawezekana kutatua tatizo sio habari ya siasa
 
Hilo na
Leo serikali kupitia bodi ya sukari nchini imetangaza bei ya sukari kwa rejareja iuzwe Tsh1800/kg kote nchini,hili ni jambo jema kwani huu ni mkakati wakumlinda mlaji.
Lakini kwa mujibu wa bei hii elekezi ni dhahiri kuna mapungufu makubwa kwani aliewekewa mipaka ya bei ya uuzaji wa sukari ni mfanya biashara wa rejareja pekee wakati wafanya biashara wa jumla hawajawekewa mipaka mfuko mmoja wa sukari wawauzie bei gani wafanya biashara wa rejareja.
Hapa panaweza leta mkanganyiko kwani kama serikali haitawawekea wafanya biashara wa jumla bei elekezi kwa mfuko wa sukari, inawezekana kabisa wakawauzia wafanyabiashara wa rejareja kwa bei ambayo kama wao watauza sukari kwa tsh1800/kg wasipate faida,
Ni vema jambo hili likatizamwa vizuri.

Hilo nalo linahitaji kuelekezwa jamani. Wewe umeshaambiwa bidhaa hii iuzwe reja-reja sh 1800/- unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unamuuzia mfanyabiashara bei chini ya hiyo. Mf, 1500 na kiwandani inabidi iwe chini ya 1500 mf 1200/- nk. Bei itajiseti tu.
 
Hii ni tanzania hakuna aliemgeni,
tunaona hata mijini kwenye foleni za barabarani jambo dogo sana lakutumia busara lakini kutatengenezwa foleni gari zitasimama mpaka trafiki aje asimamie
 
Nahisi watakuwa wamefanya analysis yao vizur mpaka kufikia kutoa uamuz wa kuiuza 1800 per kg inamaanisha wamewasiliana na provider ambao ni whole saler although tatizo halipo kwa hawa wauzaji wadog. Wadogo maana wao wanauza kulingana na bei walionunulia mfuko mmoja ili mwisho wa siku wapatepo chochote sasa bas ni vema pia mkurugenz angekuja na bei elekez kwa wananunuZ wa jumla kwa sabab hawa wawil wote wanahusik ktk kupanda kwa bei ya sukari so ukibana upande mmoja alafu upande wa pil huongelei kunatufanya tujiulize kuwa je na yy ni jibu kwenye inshu hii ya sukari?

Inaezekana kabisa mkurugenzi wa bodi ya sukari akawa ni CDM,kadi ya chama haipo kwenye viambatanisho vya CV wakati wa ajira,tutoe mawazo ili kama itawezekana kutatua tatizo sio habari ya siasa
Mkuu bei ishaelekezwa tayari 1800 ndo imetoka hiyo, kwa sababu hawa watu hawana rekodi ya kusikiliza mawazo ya wengine, binafsi nimevunjika moyo
 
Ak

Akili za Nguliw.e km hizi ndo zitatufanya tusifikir Malengo yetu.Binadam hamna shukran,kila kitu kukosoa tu....
Toka lini serikali ya Ccm ipo kwa ajili ya wananchi?
Labda tuanzie na mfano mdogo wa ununuzi wa magari ya washawasha wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.
 
Yupo kwa kazi hiyo, Leo unamwambia ajenge hoja?
Sio kila mada ni ya kuleta siasa, huu upumbavu wenu wa vyama unawapa faida gani? Kadi ya ccm au cdm haikusaidii kupata huduma bora.
When it comes to e economic issues, wawekeni siasa pembeni. Idiots!!
 
Ingawa hili suala limewekwa kwa ajili ya kumlinda mwananchi wa kawaida ambaye ni mlaji....lakini kama halijafanikiwa upembuzi yakinifu inaweza kuleta mkanganyiko baina ya wafanyabiashara na wananchi.......
 
Sio kila mada ni ya kuleta siasa, huu upumbavu wenu wa vyama unawapa faida gani? Kadi ya ccm au cdm haikusaidii kupata huduma bora.
When it comes to e economic issues, wawekeni siasa pembeni. Idiots!!
Mkuu ndio ambao huwa tunawaita MATEJA WA KISIASA.....
 
Nadhani watakuwa wamezingatia vigezo vyote japo siyo rahisi kufafanua kila kitu siamini kama wanaweza kusahau kufanyia kazi hilo.
 
Hivi Ile Tume Ya Bei Iliyokuwepo Miaka Ya 80, Ambayo Ilikuwa Ikiratibu Bei Za Bidhaa Zote Ambazo Zinazozalishwa Nchini Ktk Viwanda Vyetu!! Sasa Sijui Serikali Hivi Sasa Wanaoingia Vp Ktk Kupanga Bei Za Bidhaa, Ambazo Haizizalishi!! Ktk Sera Ya Soko Huria Na Ushindani Wa Kibiashara, Ambapo Kazi Kubwa Ya Serikali, Ni Kuandaa Mazingira Bora Ya Uwekezaji Na Kukusanya Kodi!! Sasa Sijui Kama Serikali Inaondoa Au Kupunguza KODI Zake!!! SERIKALI Ikumbuke Kuwa Sera Yake Ya Ubinafsishaji Ktk Soko Huria, Hivyo Haihusiki Na Uendesheji Wa Biashara!! Tunapenda Mno Bei Za Bidhaa Zishuke, Tupate Unafuu Wa Maisha, Ila Isitumike Siasa Ktk Hilo, Serikali Isimamie Kwa Kuweka Sera Ya Kudhibiti Hilo!!!
 
Back
Top Bottom