Upande wa pili wa Igunga na mapacha watatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upande wa pili wa Igunga na mapacha watatu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Raia Fulani, Sep 22, 2011.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kwa ufupi na uchache yaliyojiri igunga
  1. Tindikali
  2. Dc 'kupigwa' na kuvuliwa hijabu
  3. Gharama. Zimefikia zaidi ya bil 1
  4. Uzinzi
  5. Uchomaji nyumba
  6. Kupigana
  7. Kambi za maninja huko iramba

  Katika hili la maninja, Mbowe alitoa kauli akasema, 'nawaapia safari hii hatuibiwi kura kama tulivyopoteza majimbo 80 mwaka jana. Nimewaambia makamanda wangu lazima tucheze nao' (MWANANCHI leo). Kauli hii si ya kubezwa, si ya kwanza kutolewa wala si ya mwisho, wala si cdm pekee waliotoa kauli kama hii.

  Ni wazi kabisa kuwa hadi uchaguzi uishe patakuwepo na majeruhi wa kila sampuli. Hadi mazingira. Nalo ni jimbo moja tu la igunga ambapo kutokana na sera ya ccm kujivua gamba, haya ndo matokeo yake.

  Hapo ni igunga tu. Natumai pia moyo wa rostam unashangilia kwa haya yanayotokea jimboni mwake. Ni matokeo ya siasa uchwara za ccm kiukweli. Haiwezekani mtumia bilioni za hela kwenye kampeni kwa ajili ya kutoa ahadi kwa wananchi kuwa mtawapelekea maji, umeme, barabara n.k. Si walikuwa na mbunge? Mbunge si alitoka ccm? Ccm si imetawala tanzania zaidi ya miaka 30? Kwani hawakupata muda wa kuwapelekea hao wana igunga hizo huduma?

  Chenge nae aseme anaachana na siasa uchwara. Itakuwaje jimboni mwake. Lowasa nae aseme anajivua gamba, si itakuwa vurugu sasa? Zitakuwa si kampeni za kawaida kwani zitakuwa ni zao la chuki na kukamiana na kusema, 'tuone sasa'. Tuutazame uchaguzi wa igunga kwa sasa na baadae, na athari za sera nusunusu za ccm kitaifa katika kujivua gamba
   
Loading...