Upande wa Giza: Kila binadamu ana siri zake za kuficha

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Tunapozungumzia Dark Side, tunazungumzia upande wa giza. Kila unayemuona kwenye ulimwengu huu ana upande wake wa giza ambao hataki watu wengine waufahamu.

Hata wewe unayesoma hapa una upande wako wa giza ambao hutaki watu waufahamu. Ndiyo! Ipo hivyo. Na ndiyo maana huwa ninawaambieni hakuna kumuamini mtu yeyote yule.

Kuna wengine mnawachukulia binadamu kama Mungu kwamba hawezi kufanya dhambi, hawawezi kuua ama kumuabudu shetani, sijajua huwa mnauchukuliaje huu ulimwengu na binadamu wake.

Mimi simuamini hata mchungaji wangu kuhusu masuala ya Mungu, bali najiamini mimi mwenyewe. Leo ukisema yule mkuu wa dhehebu lile anafanyaga ibada za kishetani, watu watakukatalia, ukiwaambia kwamba naye huwa anaongozwa na watu wanaomfuatilia shetani na kumwambia nini cha kufanya, utakuja juu sana, kwa nini? Kwa kuwa ushamchukulia yeye ni Mungu, hatendi dhambi wala nini.

Ukisikia upande wa giza wa watu wengi utalia. Mimi huwa sipendi kusikia mambo ya upande wa giza wa watu na ndiyo maana hata mimi najitahidi sitaki watu waujua upande wangu wa giza.

Kuna jamaa yangu aliniambia bosi wao ni mtu fea sana, yaani anawapenda wafanyakazi wake, dereva wa bosi huyo akamuuliza mchizi, unaujua upande wa giza wa bosi wako? Hakika ukiujua, utasema jamaa amekaa karibu na shetani wanapiga stori kila siku.

Jitahidi sana usimtetee binadamu kwamba ni mwema. Umeletewa mashitaka yake, usitake kukaa upande wake na kusema hakuna, yule hawezi kufanya hivi na vile.

Kila binadamu ana upande wake wa giza, acha kuamini watu ni watakatifu. Hata mchungaji ama imamu wako hutakiwi kumwamini kwamba ni mtakatifu, wewe jua tu naye ana upande wake wa giza ambao hataki mtu yeyote aufahamu zaidi yake.

So shut up ukisikia unaambiwa kiongozi fulani wa dini anafanya hivi na vile, usiibuke na kuanza kumtetea, kuna watu wanajua sana pande za giza za watu katika ulimwengu huu.
 
Yin and Yang.

Dark and Light complement each other.
Esoteric_Taijitu-5c85cc7b46e0fb00014319cd.png
 
Back
Top Bottom