Upandaji wa miti aina ya pain

Dec 8, 2013
94
70
Haya jamani 2014 ndo hiyo. Timiza malengo yako ya upandaji miti ili uboreshe mazingira na ukuze uchumi wako na uchumi wa nchi kwa ujumla. Miche ya miti aina ya pain inapatikana kwa Badian kinwiko aliyeko wilayani Mufindi, Iringa, kwa bei ya sh.100@mche. Kwa wakazi wa Mufindi na maeneo jirani mnakaribishwa. Kama una swali tupia hapahapa au email hii badiankinwiko@gmail.com
 
CYBERTEQ

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
7,359
0

Huwa wanatoa maelezo mkuu, hiyo miti ina manufaa gani, ukuaji wake hata na kapicha kidogo mkuu!
 
Nanren

JF-Expert Member
May 11, 2009
1,877
2,000
PAIN ndiyo miti gani?

Bila shaka anamaanisha "pine" ambayo ikitamkwa kwa kiingereza inasikika kwa kiswahili kama "paini"

Kiswahili cha PINE ni "msonobari"

Tuvumiliane tu ndugu yangu. Ndio maana kuna watu wanasema "elementi" wakimaanisha "helmet"; "rejeta" wakimaanisha "radiator"; "dip" wakimaanisha "beep"... na mengine mengi.
 
Dec 8, 2013
94
70
Pain(pine) ni mti wa mbao, ambao hukua kwa muda wa miaka 8-10 tangu kupandwa shambani, ndipo hupasuliwa na kutoa mbao zenye ukubwa wa inchi 2kwa 8, 2kwa6(2 by 6 inch) na kushuka mpaka 2 kwa 4(2 by 4). Na ni miti inayotoa mbao zenye matumizi mengi na wateja wake ni wengi sana ikishapandwa shambani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom