kuku dume
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 414
- 62
Ndugu wakuu!
Ni dhahiri kwamba ukikaa na kujadiliana na watu utajua mengi.
Nikiwa katika wilaya ya Moshi leo nimejaribu kufika katika kata ya Kirua Magharibi na nikapata taarifa zilizonisikitisha.
Mosi ni kwamba inaonekana kwamba serikali ni dhaifu kiasi cha kuwaambia wananchi wachague ni kijiji gani wanachotaka kuwepo kati ya Kanji na Marua. Kumbuka kwamba hili linafanyika bila kujali mipaka ya kijografia.
Pili ni kuwepo kwa vijiji likuki visivyokuwa na watendaji ambapo inakadiriwa kwamba takribani vijiji 15 katika jimbo la Vunjo havina Watendaji.
Tatu ni kwamba wamekuwa wakiteuliwa watendaji wakorofi katika vijiji vinavyoshikiliwa na upinzani.
Nne ni kwamba zipo tuhuma za ufisadi dhidi ya mtendaji wa kijiji cha Nduoni kinachoshikiliwa na upinzani kiasi cha kusababisha mtafaruku katika uongozi wa kijiji. Pia nimedokezwa kwamba huyu mtendaji aliomba uhamisho kutoka kata moja kwenda nyingine bila malipo kutokana na uchafu uliozidi.
Chanzo: wananchi na viongozi wa maeneo husika.