Blood of Jesus
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 2,955
- 5,877
Mungu anajua yote (Omniscient). Alijua kuna malaika watamwasi, aliwaacha maana hakutaka kuingilia utashi wa viumbe wake kutokana na upendo mkuu alio nao. Pia alijua ni nini atakachokifanya baada ya uasi huo. Ndio maana akaandaa njia ya UKOMBOZI iliyo katika Kristo Yesu Bwana.1. Wakati Mungu anamuumba Lucifer, alijua au hakujua kwamba atakuja kumuasi?
2. Kama binadamu hakutakiwa kujua jema wala baya, angekua na tofauti gani na roboti?
3. Kama binadamu aliumbwa akiwa hajui jema wala baya, angejuaje kwamba kutokumtii Mungu ni vibaya ili asile tunda alilokatazwa?
Mungu alitaka tusijue jema na baya kwa sababu hakutaka tujiongoze wenyewe (katika nafsi) yaani kujitegemea. Alitaka tuishi kama malaika na viumbe wengine walioko mbinguni. Alitaka tuongozwe na roho, sio akili ambao Iko kwenye nafsi. Akili ya mwanadamu haina uwezo wa kumuongoza mtu kuyafanya mapenzi ya Mungu. Ndio maana mtu anajua kutenda jambo fulani ni makosa mbele za Mungu ila analitenda. Maana yake akili yake kujua jambo hilo ni dhambi haijamsaidia chochote. (ndio maana atahukumiwa)