Uovu unatawala...... Leo kuna moto makanisani balaa

Uovu unatawala...... Leo kuna moto makanisani balaa

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
9,751
Reaction score
15,545
Wakatoliki wote wanakemea uovu unaondelea kwenye nchi yetu..

Walutheri na sisi hatujabaki nyuma, kukemea japo huko juu viongozi wetu hawalushi makemeo wazi wazi, lakini waumini wote tunapewa neno la kutufungua fikra zaidi.

Mchungaji wangu leo kanisani kafundisha Mambo mengi kwa ufupi.

1. Tujue haki zetu kama Raia.
Alitoa mfano mmoja kuwa kuna police alikwenda kumkamata mtu yule mtu akamchoma na na kisu, sasa police wakamfungulia kesi ya kufanya shambulio kwa siraha...
Akajitetea kuwa ilikuwa ni self defence na akashinda kesi.

2. Aina mbili za Mamlaka
i. Mamlaka ya Mungu Mbinguni
ii. Mamlaka za watawala duniani.

kwahiyo tusikubali kupuuza juhudi za kupata viongozi Wanao litakia mema taifa letu kwa vitendo bila kupotosha haki.

3. Cha tatu kikubwa ni madhara ya taifa kukosa haki.
Leo katekwa jirani yako kesho atatekwa mke wako au mzazi wako.

leo kaibiwa jirani yako kesho watavunja geti lako.

4. nne mwisho mchungaji katufundisha Madhara ya Uchawa,

Swala la uchawa linapelekea Watu wasomi wenye sifa kuachwa na kupewa uongozi watu wajinga na wenye uwezo mdogo.


# UKOMBOZI UNAKUJA.
 
nimetoka kumsikiliza Mange kwenye page yake daaah, Kweli Wahuni sio watu wazuri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom