Uongozi wa Wizara ya Michezo, RC Dar es Salaam na TFF mmeonesha dharau kwa mkuu wa nchi

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,208
4,705
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani leo alikuwa mgeni rasmi kwenye Uzinduzi wa Kitabu cha Maisha ya Rais Mstaafu Mzee Ally Hassani Mwinyi

Viongozi Wakuu waliohudhuria ni Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, Jaji Mkuu, Mawaziri & Wabunge mbalimbali, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama & Mabalozi & Marais & Mawaziri Wakuu wastaafu n.k

Ieleweke kuwa tukio hilo la Kitaifa halikuja ghafla bali lilipangwa kitambo hivyo mechi ya watani ilitakiwa ipangwe siku tofauti na wala sio leo.

Uongozi wa Wizara, RC Dar es salaam & TFF tambueni matukio yanayomuhusisha Rais wa nchi ni matukio rasmi ya Kitaifa na yanawahusu moja kwa moja Wananchi wote

Uongozi wa Wizara ya Michezo, RC Dar es Salaam & TFF mmeonyesha dharau kwa kupanga mechi ya Simba & Yanga Watani sambamba na Uzinduzi wa kitabu cha Mzee Rhuksa!

Niwaombe wahusika wote kwa kuwa mmefanya mambo ya hovyo basi itapendeza mkijitengua wenyewe.
 
Kujipendekeza kumekuzidi Madelu. Kitabu cha maisha binafsi ya mtu kinasababishaje kuagirishwa mechi ya soka? Kwa hiyo ulitaka mechi zote nchini zisimame ili watanzania wote waangalie uzinduzi wa kitabu?
 
Kuharibu & kuvuruga afanye Bi Mkubwa halafu kulaumiwa walaumiwe TFF, Waziri na RC, Bi Mkubwa amebugi sana hapa; anataka kila tukio atokeee tuuu yeyee. ^Mtaka yote kwa pupa...^ Kwani mgeni rasmi asipokuwepo mpira hauchezeki!? Waseme tu walipanga kuwahujumu wananchi wanyonge pesa zao.

#Bi Mkubwa anaweka historia ya uongozi duni zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu. Hili liepushiwe mbali!!!
 
Kuharibu & kuvuruga afanye Bi Mkubwa halafu kulaumiwa walaumiwe TFF, Waziri na RC!? Bi Mkubwa amebugi sana hapa; anataka kila tukio atokeee tuuu yeyee. ^Mtaka yote kwa pupa...^ Kwani mgeni rasmi asipokuwepo mpira hauchezeki!? Waseme tu walipanga kuwahujumu wananchi wanyonge pesa zao.

#Bi Mkubwa anaweka historia ya uongozi duni zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu. Hili liepushiwe mbali!
Kama kuna mtu ataweza kumzidi kiongozi aliyepita kwa uongozi wa ajabu, ambaye alikuwa anaburuza watu na kuamua mwenyewe na kuvunja misingi yote basi itabidi afanye kazi ya ziada.
 
Izo hela za icho kitabu zina pelekwa kwenye maendeleo ya wananchi au ana kula uyo mzee.

Ficheni ujinga wenu .
 
"Uongozi wa Wizara ya Michezo, RC Dar es salaam & TFF mmeonyesha dharau kwa kupanga mechi ya Simba & Yanga Watani sambamba na Uzinduzi wa kitabu cha Mzee Rhuksa!"

Nini kilianza kupangwa kufanyika?
 
Kujipendekeza kumekuzidi Madelu. Kitabu cha maisha binafsi ya mtu kinasababishaje kuagirishwa mechi ya soka? Kwa hiyo ulitaka mechi zote nchini zisimame ili watanzania wote waangalie uzinduzi wa kitabu?
Madelu ndio nani mkuu
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani leo alikuwa mgeni rasmi kwenye Uzinduzi wa Kitabu cha Maisha ya Rais Mstaafu Mzee Ally Hassani Mwinyi

Viongozi Wakuu waliohudhuria ni Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, Jaji Mkuu, Mawaziri & Wabunge mbalimbali, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama & Mabalozi & Marais & Mawaziri Wakuu wastaafu n.k

Ieleweke kuwa tukio hilo la Kitaifa halikuja ghafla bali lilipangwa kitambo hivyo mechi ya watani ilitakiwa ipangwe siku tofauti na wala sio leo.

Uongozi wa Wizara, RC Dar es salaam & TFF tambueni matukio yanayomuhusisha Rais wa nchi ni matukio rasmi ya Kitaifa na yanawahusu moja kwa moja Wananchi wote

Uongozi wa Wizara ya Michezo, RC Dar es Salaam & TFF mmeonyesha dharau kwa kupanga mechi ya Simba & Yanga Watani sambamba na Uzinduzi wa kitabu cha Mzee Rhuksa!

Niwaombe wahusika wote kwa kuwa mmefanya mambo ya hovyo basi itapendeza mkijitengua wenyewe.
Ondokana na ukale uliojaa ujinga na kutojielewa. Zama za kulazimisha watu kuangalia unaowaita viongozi wa kitaifa zimekwisha. Waache watazamaji wachague cha kuangalia.
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani leo alikuwa mgeni rasmi kwenye Uzinduzi wa Kitabu cha Maisha ya Rais Mstaafu Mzee Ally Hassani Mwinyi

Viongozi Wakuu waliohudhuria ni Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, Jaji Mkuu, Mawaziri & Wabunge mbalimbali, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama & Mabalozi & Marais & Mawaziri Wakuu wastaafu n.k

Ieleweke kuwa tukio hilo la Kitaifa halikuja ghafla bali lilipangwa kitambo hivyo mechi ya watani ilitakiwa ipangwe siku tofauti na wala sio leo.

Uongozi wa Wizara, RC Dar es salaam & TFF tambueni matukio yanayomuhusisha Rais wa nchi ni matukio rasmi ya Kitaifa na yanawahusu moja kwa moja Wananchi wote

Uongozi wa Wizara ya Michezo, RC Dar es Salaam & TFF mmeonyesha dharau kwa kupanga mechi ya Simba & Yanga Watani sambamba na Uzinduzi wa kitabu cha Mzee Rhuksa!

Niwaombe wahusika wote kwa kuwa mmefanya mambo ya hovyo basi itapendeza mkijitengua wenyewe.
Kati ya mechi ya simba na yanga na tukio la kuzindua kitabu cha mwinyi ni kipi kilianza kupangwa? Tuanzie hapo
 
Back
Top Bottom