Uongozi wa Nyerere na haja ya Katiba mpya

Sio kwamba Nyerere aliongoza nchi bila katiba ya wananchi. La hasha bali kama unakumbuka wakati nchi inapata uhuru ilikuwa ni vigumu kuandaa mchakato wa katiba ambayo ingefaa kwa wakati ule. Na kama unakumbuka katiba ile ilifanyiwa marekisho kadhaa kuendana na wakati na nini wananchi walikuwa wanahitaji.
Sasa kiongozi bora anatawala bila ya katiba ya wananchi????????????
 
Mzee wangu hakuvunja miiko yoyote ila nilimsikia akisema huu ujama umefeli duniani kote kwa hiyo haoni uhakika kama ungefaulu Tanganyika. Ni kweli

Wazee ambao hawakuvunja miiko ya uongozi ni wa kukumbukwa sana, ulimjumuisha na kina Kasanga Tumbo pamoja na Kambona ndo maana nikasema hivyo, Maana wale jamaa ni kweli walikuwa hawakubaliani na Nyerere lakini walidhaniwa pia wangeweza kupindua serikali.
 
well ndiyo haya haya ya "Waziri apigwa rungu".... unaweza kabisa ukajishawishi kuwa nimewahi kusema hivyo lakini ukitafuta hutapata mahali popote. Ni sawasawa na watu ambao hudai "Nyerere aliwahi kusikika kusema" au "Inadaiwa Nyerere alisema"... ukiuwaliza lini na wapi wanaenda kutafuta nukuu za mtu ambaye naye anadai kuwa Nyerere "aliwahi kusema". Tatizo huwezi kuyapata hayo maneno yenyewe ya Nyerere.

sio lazima useme moja kwa moja.....
but thru maandiko yako..

kuna vitu viwili unavisimamia ambavyo ni

1.umuhimu na haja ya katiba mpya...

2.nyerere alikuwa kiongozi bora aliekuja kabla ya wakati wake....

sasa we huoni unajichanganya hapo....?????????

angekuwa bora kihivyo leo tungehitaji katiba mpya?????????????

yeye hakuona umuhimu wa katiba yenye uhali tunaouzungumzia leo?????????

sisemi katiba haziihitaji mabadiliko...

ninachosema mabadiliko na kudai katiba mpya ni vitu viwili tofauti.....

katiba mpya maana yake nyerere hakuwa kiongozi bora full stop.
 
Wazee ambao hawakuvunja miiko ya uongozi ni wa kukumbukwa sana, ulimjumuisha na kina Kasanga Tumbo pamoja na Kambona ndo maana nikasema hivyo, Maana wale jamaa ni kweli walikuwa hawakubaliani na Nyerere lakini walidhaniwa pia wangeweza kupindua serikali.

Kutokukubaliana na serikali iliopo ama rais aliyeko madarakani haimaanishi mtu anataka kupindua nchi.
 
THE BOSS

si tu kwamba watu wanamsifia Nyerere and, at the same time wanaponda aliyofanya bila wao kujua hivyo.

kumbuka pia wanasema pia CCM haijawahi kutufanyia kitu cha maana tangu tupate uhuru, wanasahau wakishasema hivyo tayari Nyerere hajatufanyia kitu kizuri kwa muda aliokaa madarakani.

tataizo wanasahau kwamba kuku ni yai na yai ni kuku,

tatizo lingine bado ule mzimu wa zidumu fikra za mwenyekiti umeharibu vichwa vya watu, yale mabaya yalifichwa kwa ustadi kiasi cha kuchanganya sana watu,

with time wataelewa tu, pole pole ndio mwendo,

hawa watu wa ajabu sana
watamponda mwinyi wakati hata huyo mwinyi aliwekwa na nyerere....
na uyo mkapa ni product ya nyerere....its funny
 
Duh....Man you are right,ila nimecheka sasa.Buried here is the lacuna of ill-concieved political abracadabra that interred our forlon hopes in the six-foot-deep tomb of dispair, fending off the great minds and excited from the public sit-and-speak citizenry

So,case dismissed?

Case dismissed without costs? lol
 
Pamoja na ubovu wa katba ambayo aliisimamia, kamwe nyerere did not misuse. Kwa matendo na ubora wa uongozi wake, ndio uliwafanya watz wasidai nyingine. Kwa katba ambayo leo ni mbovu, mwl aliweza kujibana na kuwabana manyau na mambwa walafi wa taifa, kinyume na sasa. Mafisi wamenenepa, panya wanashangilia wakat paka yupo na hata wanasubutu kushka sharub za paka, paka anacheka tu, na wakat mwingine anakimbia yeye. Hii ni hatar.
 
Kweli hujafa hujaumbika ! Hata hivyo wengine wetu hatushangai sana. Kikwete kaingia madarakani mwaka 2005 iwe kihalali au hapana lakini ni ukweli Watanzania walikuwa na matumaini makubwa naye wakati huo. Ili kuwaondoa hofu waliokuwa bado wana wasi wasi naye, katika hotuba yake ya kwanza alikuwa na haya ya kusema kuhusu Baba wa Taifa;
Tangu tupate Uhuru, kila awamu ya uongozi wa taifa imekuwa na majukumu yake ya msingi. Awamu ya Kwanza iliunda na kujenga taifa. Wakoloni hawakujenga hisia za utaifa, maana mkakati wao wa kututawala ulikuwa kutudhoofisha kwa kutugawa ili tutawalike kwa urahisi. Mwalimu Nyerere hakurithishwa taifa na wakoloni. Alirithishwa mkusanyiko wa makabila mbalimbali, na watu wa dini na rangi mbalimbali. Akatambua kuwa hata uchumi wa Tanzania ungekua kwa kasi kubwa kiasi gani, iwapo hakuna misingi imara na hisia za dhati za utaifa, baada ya muda tutasambaratika na uchumi huo utakuwa hauna maana. Kwa kushirikiana na hayati Mzee Karume wakatujengea Taifa la Tanzania lenye umoja, pamoja na watu wake kuwa wa makabila 120, rangi na dini mbalimbali.
Mwalimu aliongoza vita dhidi ya ujinga, umaskini na maradhi. Mtandao mkubwa wa huduma za jamii tunaojivunia leo ulianza na falsafa ya maendeleo ya Baba wa Taifa. Wengi wetu tuliomo humu ndani, wa makamo yangu, tusingesoma na kufika hapa tulipo kama si kuona mbali na sera nzuri za Baba wa Taifa.

Hayo aliyasema wakati huo, lakini leo hii anasita hata kumwita Mwalimu Baba wa Taifa. Badala yake baada ya kutambua kuwa kumbe uongozi wa taifa si lelemama na kwamba hana uwezo wa kusimamia utawala wa sheria, kaamua kwa makusudi kuzitikisa zile nguzo alizozisifia wakati anaingia madarakani. Kwa makusudi ameamua kuunda mtandao ambao kwa kukosa busara anaamini utamnusuru kumbe una hatari ya kuusambaratisha umoja wetu ambao tumejivunia tangu uhuru. Anafikiri anaweza kufunika mapungufu yake kwa kumtupia lawama Baba wa Taifa ambaye siyo tu aling'atuka miaka 26 iliyopita bali kwa sasa ni marehemu asiyeweza kujitetea.

Huu mtandao ambao hivi sasa tunaushuhudia kila leo hadi hapa JF, ni mtandao ambao kwa vyovyote vile hauwezi kufanikiwa kwani ni za kutapatapa kama za mtu anayezama huku kasi ya maji ikizidi. Mitandao yenye malengo maovu ya aina hii huwa haidumu na Kikwete mwenyewe ni shahidi kwani anashuhudia jinsi mtandao uliomwingiza madarakani mwaka 2005 kwa hila unavyomtafuna bila huruma. Amejaribu kuwagawa Watanzania kikabila ameshindwa, amejaribu kidini hakufanikiwa na sasa anajaribu kutugawa kuhistoria. Kama alivyowahi kukiri yeye mwenyewe asithubutu kujaribu kuvaa viatu vya Mwalimu, haviwezi na asipoangalia vitamwangusha chali !

Utafiti kidogo tu unaonesha kuwa wote wanaojaribu kumdhihaki Mwalimu (RIP) ni hao hao wanamtetea huyu Kiongozi aliyekimbilia Ikulu bila kujua atafanya nini akifika hapo. Shuhudia katika hii hotuba yake ya kwanza kabisa Bungeni baada ya kuchaguliwa mwaka 2005 kuhusu Nishati;
Mheshimiwa Spika:
Nishati ni sawa na chembe za damu mwilini. Tutapanua wigo na aina ya vyanzo vya umeme na nishati kwa jumla ili kuwa na nishati ya kutosha na yenye gharama nafuu kukidhi mahitaji ya uzalishaji viwandani, utoaji wa huduma za kijamii, na matumizi ya nyumbani. Tutayashughulikia kwa kipaumbele cha juu matatizo ya sasa yahusuyo upatikanaji wa umeme nchini.
Mheshimiwa Spika:
Ilani ya CCM ya Uchaguzi wa Oktoba 2005 inasema wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itaharakisha mradi wa kupata umeme kutoka makaa ya mawe ya Mchuchuma. Na hivyo ndivyo tutakavyofanya. Aidha, Serikali ya Awamu ya Nne itafufua mipango ya umeme wa Mto Rusumo na Stigler's Gorge. Vile vile tutaharakisha upatikanaji wa umeme kutoka gesi asilia ya Mnazi Bay.
Mheshimiwa Spika:
Lengo la Serikali ya Awamu ya Nne pia ni kuendeleza kazi ya kufikisha umeme katika miji mikuu ya wilaya isiyo na umeme hivi sasa, kuongeza kasi ya kupeleka umeme vijijini kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini, na kuiunganisha Mikoa ya Kigoma na Ruvuma katika gridi ya Taifa.

Baada ya hotuba hiyo tukaingia mkataba na Richmond na leo hii miaka sita baadaye, ndio hali inakuwa ngumu zaidi na mgao wa umeme ndio hivo tena. Halafu kuna watu wanathubutu kumtetea Kikwete kwa kujaribu kuuandika upya historia ya taifa kwa simulizi za uwongo na zilizojaa chuki. Hapana, mapungufu ya Kikwete yawe ni mzigo wake na awe tayari kuubeba bila kukwepa na bila kumsingizia Baba wa Taifa. Je yawezekana hii yote inasababishwa na Mwalimu mwaka 1995 kuzima mbio za Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumsoma sawa na kuuona udhaifu wake ? Sifa anazopewa Mwalimu iwe ndani au nje ya taifa letu hazitapungua eti kwa sababu ya wivu na chuki za watu wachache wanaotafuta umaarufu bila sifa.
 
katiba mpya maana yake nyerere hakuwa kiongozi bora full stop.

duh.. haya kama unaweza kutengeneza correlation ya namna hiyo. Kama kutaka kuwa na Katiba Mpya maana yake ni uongozi mbaya wa Nyerere na ndicho kipimo pekee unachotumia kuamua basi hakuna namna nyingine isipokuwa msimamo wako huo.
 
nimesema hakuwa kiongozi bora,sijasema alikuwa kiongozi mbaya...
kuna tofauti hapo..

unaweza sema alikuwa kiongozi mzuri lakini sio bora.....
 
Kuna vitu viwili vinaendelea hapa tanzania
na jf pia..............

Watu wengi wanazungumzia haja na madai ya kuwepo kwa katiba
mpya...
Ambayo itakuwa ya watanzania,ya wananchi.
Itakayowapa uhuru wao na mambo mengi kwa ujumla...

Watu wengi akiwemo issa shivji,mwanakijiji na wengineo

wamedriki kusema kusema au kuunga mkono kuwa

katiba iliyopo sio tu haifai,lakini haijawahi kuwa ya wananchi......

Wakati huo huo,kuna mjadala wa kumkosoa nyerere na utawala wake

mjadala ambao cha kushangaza wale wengi wanaomtetea nyerere kuwa

alikuwa kiongozi bora na wa mfano,
na ambae alikuja kabla ya wakati wake ndio hao hao wanaodai katiba hii tuliyonayo

haifai na haijawahi kuwa ya wananchi......
Ni katiba mbovu,inayowakandamiza wananchi,haiwapi nguvu na uhuru wa kutosha
na kadhalika......

Sasa hapa swali ninalouliza ni hili.............

Inawezekanaje nyerere huyo huyo ambae alikuwa

kiongozi bora sana,na wengine mkimwita ni nabii na mtakatifu aliyekuja kabla

ya muda wake.......lakini leo katiba ile ile aliyoitumia kutawala na kuitengeneza

tuseme haifai kabisa na haina uhalali na sasa tunahitaji mpya?????????????????????????????

Mind you kuwa hatuzungumzii mabadiliko ya katiba tu
tunazungumzia katiba mpya,katiba nyingine inayofaa na sio hii ya nyerere...

Boss siamini kabisa kuwa MKJJ na wenzake hawalioni hili. Umesema logically, na sidhani kama logic hii inabishika.

Ila Logic yako umeiweka very strict kana kwamba kwa sababu Nyerere alivurunda hapo basi hawezi kupendwa!!!!

MKJJ simply anampenda Nyerere sometime I can feel how he feels when someone despises Nyerere! I think it is nature,and that called LOVE! love is blind mkuu we sema mabaya yote ya Nyerere atampenda tu!

If we say because Nyerere did not install good constitution then he was bad leader .....we are judging logically and in REALITY is TRUE! incontrovertably

If we say because Nyerere did not install good consitution then he is not supposed to be loved.....we can not judge this, because we are free to love anybody THIS IS ALSO TRUE.Incontrovertably!!

Nyerere anapendwa simply kwa sababu alikuwa anawapenda watu, alikuwa hana tamaa ya fedha, alilipenda taifa..In other words kwa katiba hii alikuwa mfalme mzuri sana, na waflame waliokuja baadae wameharibu sana!!!

Potelea pote, zama hizi, siku hizi, nyakati hizi, na muda huu, bora kuwa na katiba hii hii na kiongozi akiwa wa aina ya Nyerere!!! Lakini watu wa sasa hawafai kuwa na katiba hii ya Nyerere!!

Look here, another piece of thought.

Kwa sababu katiba hiii hii inatumiwa na watu wengine na kuweza kufanya madudu mengi, katiba hii hii coincidently imekuwa kama chujio la kuchuja wazalendo na wasio wazalendo, la kuchuja kati ya warafi na wasio warafi. In other words katiba hii si kuwa haikuwa ya wananchi tu, bali imefanyika msaada wa kumtofautisha Nyerere na viongozi wengine!! Hili pia ni sifa kwa upande mmoja wa Nyerere lakini ni kosa la karne ka kufikiri kila mmoja atakuwa kama wewe!!

Can I defend Nyerere about this..Yes I can

1. Society zinakua, we did that simply because we were who we were at that time!!!!
2. Tulitoka kwenye ujima, kwa kufikiri kila mtu anapenda jamii
3. Hatukupita kwenye kizazi cha ufisadi kama hiki, laiti tungepitia hiki kizazi mwaka huu 2011 na kurudi 1961 definitely Katiba ingekuwa tofauti, this said, I am corroborating the first point.
 
sio lazima useme moja kwa moja.....but thru maandiko yako..kuna vitu viwili unavisimamia ambavyo ni 1.umuhimu na haja ya katiba mpya...2.nyerere alikuwa kiongozi bora aliekuja kabla ya wakati wake....sasa we huoni unajichanganya hapo....?????????angekuwa bora kihivyo leo tungehitaji katiba mpya?????????????yeye hakuona umuhimu wa katiba yenye uhali tunaouzungumzia leo?????????sisemi katiba haziihitaji mabadiliko...ninachosema mabadiliko na kudai katiba mpya ni vitu viwili tofauti.....katiba mpya maana yake nyerere hakuwa kiongozi bora full stop.
Hata Mungu (Jehovah , Allah) naye ni dictator ! Period ..!Na Mungu si mwenye Haki , kwani yeye kama muumbaji na mgawaji na mmiliki ..hagawi kwa usawa. Tena ni mbinafsi. Unabisha?
 
Boss siamini kabisa kuwa MKJJ na wenzake hawalioni hili. Umesema logically, na sidhani kama logic hii inabishika.

Ila Logic yako umeiweka very strict kana kwamba kwa sababu Nyerere alivurunda hapo basi hawezi kupendwa!!!!

MKJJ simply anampenda Nyerere sometime I can feel how he feels when someone despises Nyerere! I think it is nature,and that called LOVE! love is blind mkuu we sema mabaya yote ya Nyerere atampenda tu!

If we say because Nyerere did not install good constitution then he was bad leader .....we are judging logically and in REALITY is TRUE! incontrovertably

If we say because Nyerere did not install good consitution then he is not supposed to be loved.....we can not judge this, because we are free to love anybody THIS IS ALSO TRUE.Incontrovertably!!

Nyerere anapendwa simply kwa sababu alikuwa anawapenda watu, alikuwa hana tamaa ya fedha, alilipenda taifa..In other words kwa katiba hii alikuwa mfalme mzuri sana, na waflame waliokuja baadae wameharibu sana!!!

Potelea pote, zama hizi, siku hizi, nyakati hizi, na muda huu, bora kuwa na katiba hii hii na kiongozi akiwa wa aina ya Nyerere!!! Lakini watu wa sasa hawafai kuwa na katiba hii ya Nyerere!!

Look here, another piece of thought.

Kwa sababu katiba hiii hii inatumiwa na watu wengine na kuweza kufanya madudu mengi, katiba hii hii coincidently imekuwa kama chujio la kuchuja wazalendo na wasio wazalendo, la kuchuja kati ya warafi na wasio warafi. In other words katiba hii si kuwa haikuwa ya wananchi tu, bali imefanyika msaada wa kumtofautisha Nyerere na viongozi wengine!! Hili pia ni sifa kwa upande mmoja wa Nyerere lakini ni kosa la karne ka kufikiri kila mmoja atakuwa kama wewe!!

Can I defend Nyerere about this..Yes I can

1. Society zinakua, we did that simply because we were who we were at that time!!!!
2. Tulitoka kwenye ujima, kwa kufikiri kila mtu anapenda jamii
3. Hatukupita kwenye kizazi cha ufisadi kama hiki, laiti tungepitia hiki kizazi mwaka huu 2011 na kurudi 1961 definitely Katiba ingekuwa tofauti, this said, I am corroborating the first point.

ha haaaaaaaaaaa love is blind sio lol
 
Kuna vitu viwili vinaendelea hapa tanzania
na jf pia..............

Watu wengi wanazungumzia haja na madai ya kuwepo kwa katiba
mpya...
Ambayo itakuwa ya watanzania,ya wananchi.
Itakayowapa uhuru wao na mambo mengi kwa ujumla...

Watu wengi akiwemo issa shivji,mwanakijiji na wengineo

wamedriki kusema kusema au kuunga mkono kuwa

katiba iliyopo sio tu haifai,lakini haijawahi kuwa ya wananchi......

Wakati huo huo,kuna mjadala wa kumkosoa nyerere na utawala wake

mjadala ambao cha kushangaza wale wengi wanaomtetea nyerere kuwa

alikuwa kiongozi bora na wa mfano,
na ambae alikuja kabla ya wakati wake ndio hao hao wanaodai katiba hii tuliyonayo

haifai na haijawahi kuwa ya wananchi......
Ni katiba mbovu,inayowakandamiza wananchi,haiwapi nguvu na uhuru wa kutosha
na kadhalika......

Sasa hapa swali ninalouliza ni hili.............

Inawezekanaje nyerere huyo huyo ambae alikuwa

kiongozi bora sana,na wengine mkimwita ni nabii na mtakatifu aliyekuja kabla

ya muda wake.......lakini leo katiba ile ile aliyoitumia kutawala na kuitengeneza

tuseme haifai kabisa na haina uhalali na sasa tunahitaji mpya?????????????????????????????

Mind you kuwa hatuzungumzii mabadiliko ya katiba tu
tunazungumzia katiba mpya,katiba nyingine inayofaa na sio hii ya nyerere...
Hili swali zuri kama hutazingatia mabadiliko yaliyokwisha tokea.

Labda nikuulize wewe kulikuwa na makosa gani kusifia aliyevumbua Typeletter machine, kisha leo tunatumia PC na tukazungumzia mapungufu ya Typelletter wakati bado tunatumia keyboard yenye mpangilio wa herufi wa Typeletter!. Kwa maana hii nina maana kwamba Katiba mpya inahitajika kulingana na mahitaji yanayotakiwa leo hii, lakini haina maana utunzi wa katiba ya kwanza ulikuwa na makosa wala sifa za mwalimu zitaondoka kwa sababu tu katiba hiyo haihitajiki tena.

Na hakika mkuu wangu ktk makuzi ya kiumri, Tanzania haiwezi kuendelea kuvaa nepi, tukilishwa na kuwa chini ya amri ya wazazi hata baada ya kuvunja ungo na kuingia ktk dunia ya Utandawazi..
 
THE BOSSsi tu kwamba watu wanamsifia Nyerere and, at the same time wanaponda aliyofanya bila wao kujua hivyo.kumbuka pia wanasema pia CCM haijawahi kutufanyia kitu cha maana tangu tupate uhuru, wanasahau wakishasema hivyo tayari Nyerere hajatufanyia kitu kizuri kwa muda aliokaa madarakani.tataizo wanasahau kwamba kuku ni yai na yai ni kuku, tatizo lingine bado ule mzimu wa zidumu fikra za mwenyekiti umeharibu vichwa vya watu, yale mabaya yalifichwa kwa ustadi kiasi cha kuchanganya sana watu,with time wataelewa tu, pole pole ndio mwendo,
alichokijenga jkn, ndio hivyo leo tunaviharibu, madn tunayaiba na viwanda chuma chakavu, ndio maana tuna generalize, lakn babu did best.
 
Hili swali zuri kama hutazingatia mabadiliko yaliyokwisha tokea.

Labda nikuulize wewe kulikuwa na makosa gani kusifia aliyevumbua Typeletter machine, kisha leo tunatumia PC na tukazungumzia mapungufu ya Typelletter wakati bado tunatumia keyboard yenye mpangilio wa herufi wa Typeletter!. Kwa maana hii nina maana kwamba Katiba mpya inahitajika kulingana na mahitaji yanayotakiwa leo hii, lakini haina maana utunzi wa katiba ya kwanza ulikuwa na makosa wala sifa za mwalimu zitaondoka kwa sababu tu katiba hiyo haihitajiki tena.

Na hakika mkuu wangu ktk makuzi ya kiumri, Tanzania haiwezi huwezi kuendelea kutumia mari za kuvaa nepi na kuwa chini ya amri ya wazazi hata baada ya kuvunja ungo na kuingia ktk dunia ya Utandawazi..

mkandara nakuheshimu sana
lakini naona hujaelewa maana ya katiba mpya......

unayoyasema nafikiri una maanisha mabadiliko ya katiba......

katiba mpya ni kitu kikubwa mno.kina ondoa uhalali wa katiba iliyopo...

nimesema hapo juu

kuifanyia mabadiliko katiba,ni kitu kingine kabisa
na kudai katiba mpya......

ni vitu viwili tofauti mno..........

wamarekani hawajawahi kudai katiba mpya,
lakini wameifanyia mabadiliko katiba yao mara nyingi mno...
 
Watanzania tukizidi kumtukuza nyerere hakika hatuta jenga nchi kamwe. Huyu Nyerer si aliwahi kutawala nchi mpaka watu wakatembea uchi mtwara au ni mwingine? Si ni yuel raisi aliwawanyima haki ya kutawala nchi watu wengine wenye mawazo tofauti na yeye kisiasa? Mfumo wa chama kimoja maana yake ni nini kama sio kinyume cha haki za wanadamu? SI ni raisi aliyetunyima haki ya kuwa na TV kwa miaka 27 ya utawala wake huku tukizomewa na africa nzima? Kumbuka Tanzania ndio nchi pekee africa iliwahi kukosa kuona world cup toka 1970 mpaka 1986 kwa sababu za siasa zake nyerere za kutunyima haki za kuwasiliana na dunia. Akatufutia kiingereza pia si kwa mapenzi yetu bali mapenzi yake na na ya wachina! Ni kweli mtu huyu anastahili kuitwa kiongozi bora jamani? Au hao baraza la maskofu katoliki hawakuyaona haya yote mpaka leo wamwite eti ni mtakatifu? Pelekeni jina Vatican halafu muone majibu yake mnajibiwa mara baada ya miaka 500!
 
On top of that ametuachia legacy ya wananchi walio wengi kuwa waoga kudali haki zao, wanyenyekevu kwa wageni, wasiojiamini, wanaoamini kupata shida za maisha ni haki yao etc....The ghost and legacy of Nyerere!!!
 
Shamba la kijiji-lazima ukalime n'gwe yako la sivy utaishia rumande
Vyama vya kilimo na ushirika
magari kutembea jumapili mwisho saa 8 mchana
Mchele, ngano, sukari na sabuni hupati hadi kibali cha RTC ama uende duka la kaya
Marufuku kumiliki TV
Marufuku kumiliki mashamba
Marufuku kumiliki nyumba yenye kuzidi thamani ya laki moja
Magazeti ya nje marufuku
Ukikutwa na Colgate ama Palmolive, basi unahujumu uchumi utaenda jela
Marufuku kuanzisha radio stations. RTD tu iwe hewani

Ujamaa ni ujinga!!

Du! Hii ni kali mlikuwa mnaishije sasa?
 
Back
Top Bottom