Uongozi wa chadema morogoro mjini haufai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uongozi wa chadema morogoro mjini haufai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Inkognito, May 10, 2012.

 1. I

  Inkognito Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati umefika sasa kwa Viongozi wa kitaifa wa Chadema kutupia jicho uongozi wa Chadema jimbo la Morogoro Mjini kufuatia hali mbaya ya kisiasa inayoendelea ndani ya Jimbo la Morogoro Mjini.

  Nikiwa kama mjumbe wa Kamati tendaji ya Chadema Wilaya nimekuwa nikishuhudia namna viongozi wa Chadema jimbo la Morogoro Mjini wanavyopoteza muda wao mwingi kujadili watu badala ya kupanga mikakati ya kukiendeleza chama.Moja ya mapungufu makubwa ya Viongozi hao ni haya:

  Wanapinga kila mipango mizuri inayofanywa na baadhi ya viongozi wenzao
  wanapinga mawazo mazuri yenye malengo ya kujenga chama kwa mfano, katika mkutano uliofanyika tarehe 5/5/2012 katiuka kata ya Kichangani viongozi hao wakiongozwa na Katibu wa Chadema wilaya, Mercy, Inocent Zawadi pamoja na Mwenyekiti Mzee Kiroka walisusa kuhudhuria mkutano huo uliondaliwa na uongozi wa kata ya kichangani na kuhutubiwa na Benson Kigaila-Mkurugenzi wa Mafunzo na Organization, Mheshimiwa Amani Mwaipaja-Mbunge Kivuri wa Chadema Morgoro, Renatus Nzemo-Mwnyekiti wa BAVICHA-shinyanga pamoja na makamanda kibao wa Chadema.

  Mtu pekee anayatajwa kukivuruga chama ni MERCY-Katibu wa BAWACHA ambaye badala ya kufanya shughuli za chama ana kazi kubwa ya kuendesha kazi ya majungu na kuzusha mambo yasiyo na ukweli kuhusu viongozi wenzake.

  Mercy ndiye anayetajwa kuendeleza siasa za chuki dhidi ya aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Morogoro mjini kupitia Chadema Mheshimiwa Amani Mwaipaja, kijana mdogo, makini na msomi na mwenye msimamo wa kweli katika siasa.
  Imefikia hatua Mercy anajiita kuwa yeye Mbunge mtarajiwa kwa baadhi ya wanachama ambao wapo upande wake, tafadhalini viongozi wa Chadema, tunawaomba mshughulikie jimbo la Morogoro Mjini kabla mambo hayajawa mabaya
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikijiuliza sana Morogoro mjini kuna matatizo gani mbona hawaamki? Nini kinawaridhisha?
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Inabidi Viongozi na wanachama hapo mkoani CDM waanze kupangua hiyo safu mapema ili mambo yaende sawa!!
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Gombea wewe tunakukubali sana achana ila kwanza urudi Morogoro,kwanza umetembea mikoa mingi sana hapa Tanzania,unajuana na watui wengi sana ukitaja tu lile jina lAko lilizoeleka kila mtu atakuambia Gombea, hii ni nafasi yako maana wakati ni huu
   
 5. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  Wasiliana na uongozi taifa kwa maandishi kwa haraka kama unaipenda chadema
   
 6. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inabidi Benson Chigaila atoe taarifa ya alichokigundua makao makuu.Ili hatua stahiki zichukuliwe.
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwani hauna mawasiliano na uongozi wa chama taifa?
   
 8. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  fanya mawasiliano na makao makuu kwa msisitizo zaidi
   
 9. I

  Inkognito Member

  #9
  May 10, 2012
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa walilonalo viongozi hao ni uelewa mdogo walionao katika kuendesha chama makini kama chadema kwa wakati huu, chadema inazidi kukua, wananchi wanazidi kukiamini lakini viongozi waliopo Morogoro Mjini bado hawajatambua hilo,

  Matatizo ya viongozi hao hata mwenyekiti wa chadema mkoa wa Morogoro ambaye pia ni mbunge wa viti maalum mama susan Kiwanga anayajua lakini kinachoonekana ameshindwa kutumia nafasi yake katika kuwaweka sawa viongozi hao,kwa taarifa tu baada ya mkutano wa tarehe 5/5/2012 pale kichangani viongozi wa wilaya-kamati tendaji waliamua kuwaita viiongozi wa Kata ua kichangani na kuwahoji kwanini katika Mkutano huo walimwalika Mheshimiwa Amani Mwaipaja-Mbunge Kivuri wa Chadema,Renatus Nzemo-Mwenyekiti BAVICHA-Shyinyanga pamoja na Katibu wa Mbunge wa viti maalum mama susan Kiwanga, yote hayo wanayafanya kwa maslahi yao binafsi kwakuwa hata katika kikao hicho walitamka wazi kuwa kwanini viongozi wa kichangani waliwaita watu ambao hawawataki,
  Mheshimiwa Benson hawezi kujua hayo kwakuwa alikuja kwa ajili ya kuhutubia tu baada ya jitihada za kualikwa zilizofanywa na viongozi wa kICHANGANI kuzaa matunda,

  Tatizo la Morogoro mjini likiachwa litazua utata mkubwa kama ule uliojitokeza ifakara na Kilombero kwa marehemu Regia Mtema
  Viongozi wa Morogoro Mjini kwa sasa wapo bize kuendeleza siasa sa makundi....wamepitwa na wakati
   
 10. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  walugulu ni watu wamaneno maneno tuu ...action ni zero .... afadhali hata wakagulu
   
Loading...