johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 94,182
- 164,688
Prof Lipumba amekiri mara kadhaa kwamba aliridhia Dr Slaa awe mgombea urais kupitia Ukawa.Kielimu Prof amemuacha mbali sana Slaa lakini kiuongozi ni kinyume chake.Tuna mifano mingi ya watu waliojaliwa vipawa vya uongozi bila kujali elimu walizopitia.Mtu mwenye talanta ya uongozi huwa ni mwenye kuthubutu na wakati wote hujiamini ktk yale ayatendayo, ukiwaangalia kwa umakini Lipumba na Slaa utanielewa.Lakini pia yupo RC wa Dar es salaam aliyejaaliwa talanta hii ya uongozi, yeye husema na kutenda.Tuliaminishwa huko nyuma kwamba kuna baadhi ya mafisadi na wauza ngada wakiguswa tu au kutajwa nchi itatikisika lakini Makonda amewagusa na kuwataja na nchi iko shwari.Hakika tusome kwa ajili ya kuwa matabibu, wachumi, wahasibu nk lakini ili tuwe viongozi tunapaswa kuwa na hofu ya Mungu na kumuomba na kumtukuza yeye kila siku.