Jiwe limerushwa gizani.Wenye maamuzi wanafanya kama vile hawaoni ukweli.!!
Mfumo kuanzia elimu ya msingi ni shida tupu,wao wanawapeleka watoto wao katika za 'english medium',huku wakifahamu kuwa kila mwananchi anataka elimu bora kwa mtoto wake.
Tujiulize,ni gharama kiasi gani inahitajika ili kubadilisha mfumo wa elimu ya msingi kuwa 'english medium' .
Tena,tujiulize kwanini shule za 'english medium' zinazidi kuongezeka.
Majibu ya maswali hapo juu,ni kwamba bado wenye maamuzi hawajawa tayari kutatua 'KIU YA MWANANCHI' katika kuwapatia watoto elimu yenye usawa katika jamii.
Ngazi ya vyuo,bado tumeendelea kukariri mifùmo iliyopitwa na wakati,na hivyo kuathiri ubora na umahiri wa mwanafunzi anaporudi kuishi na jamii.
Jamii inamuona mwanafunzi hana msaada kwa jamii