mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,219
- 6,650
Salaam wanaJF!
Wengi wetu huishi kwa kusema uwongo. Uwongo ndiyo chakula chetu kikuu. Uongo ndiyo taaluma yetu. Ukiingia kwenye siasa unafuzu na kuwa profesa wa uongo.
Dr Daniel Langleben wa Chuo Kikuu cha Pennsylvania (limeandika gazeti la JamboLeo, Alhamisi Septemba 26, 2016)katika utafiti wake amegundua kwamba ubongo unalazimika kufanya kazi kubwa na kwa bidii zaidi unaposema uongo kuliko unaposema ukweli.
Dr Daniel, kwa kutumia mashine ya MRI (Magnetic Resonance Imaging)amegundua kwamba mtu anaposema uongo, ubongo unahitaji kuanza kazi ya uchakataji, kisha kwa kutumia silika (mazoea)msema uongo uanza kufikiria jibu la kweli kwanza kabla hajafikiria kusema uongo.
Anaongeza "katika ubongo huwezi kupata kitu cha bure. Mchakato wa kusema uongo ubongoni ni mgumu zaidi kuliko mchakato wa kusema ukweli, kiasi unasababisha matumizi nakubwa zaidi ya nyuroni (seli za neva)".
Huku kwetu tuna msemo "ukiwa mwongo, basi uwe na kumbukumbu ya kile ulichosema". Kitendo hicho hugharimu uwezo wa ubongo kiasi unashindwa kufanya mambo mengine ya msingi. Lakini kila unaposema ukweli huitaji kukumbuka chochote. Kwa maana hiyo MWONGO anaupa ubongo wake mzigo mkubwa.
TUISHI KWA KUSEMA UKWELI SIKU ZOTE ILI UBONGO USILAZIMIKE KUKUMBUKA UONGO TUNAO UTUNGA
Wikiendi njema nawatakia kwa kuambizana ukweli tu.