Tetesi: Uongo juu ya JKT

contask

JF-Expert Member
Jan 3, 2021
266
450
Habari wana Jf
nisiwachoshe tuende moja kwa moja kwenye uzi.
katika mitaa yetu tunayoishi kumekua na tetesi nyingi zinazosambaa zikihusisha na kuelezea maisha ya jeshini(JKT) na kuonekana ni tishio kwa vijana ambao wanatarajia kwenda jeshini.
Utafiti ambao nimefanikiwa kuufanya katika kipindi kifupi mtaani nimefanikiwa kugundua kwamba wengi wao wanaosambaza taarifa hizo asilimia 80 wakati asilimia 20 ni watu ambao wameenda jeshini na kama ilivyo sifa ya fasihi simulizi ya kukosa uhalisia kutokana na kuongeza na kupunguza taarifa hizo

. Mfano wa uzushi huo ni kama;
📌kula kwa kuhesabiana dakika
Ambapo kijana atatakiwa kula kwa haraka ndani ya muda ambao amepangiwa,muda huo ni kama vile dakika 5 au 10

📌mafunzo ya jeshini(jkt) ni magumu kiasi kupelekea vifo vya vijana

📌jeshini ni sehemu ya mateso na sio mafunzo kama wasemavyo

Huo ni baadhi ya uzushi kuhusu maisha ya jeshini pia kama mdau wa Jf naamini utakua umekutana na uzushi na tetesi nyingi zaidi kuhusu maisha ya jeshini ukiachana na machache ya hapo juu

✅️niendelee kwa kuelezea kwa ufupi maisha ambayo niliexperience nikiwa jeshin.
Mnamo mwaka 2022 nilifanikiwa kwenda kambi X ya jeshi ya jkt kwa ajiri ya mafunzo

ilikua mnamo saa 12 niliwasilini kambini hapo,nilikutana na vijana wenzangu ambao wamewasili kambini hapo wakiwa wamekaa chini wakisubiri muda waongezeke na wengine ambao tunawasili ili tuweze kuondoka kwa pamoja
Baada ya kama nusu saa tuliambiwa tusimame na kutembea single line tayari kwenda kuacha vitu vyetu na rasmi kuanza maisha ya kambiani hapo wengi wetu walikua wamevaa full track suit na vipara
Tulifika maeneo ya mbwenini ambapo jeshini tunaita anga tulikabidhiwa vitanda vjzuri tukalala hadi asubuhi

Katika kipindi hicho unakua na cheo cha uzalendo maisha yalikua simple sana zaidi zaidi ni kukimbia kimbia na kuimba nyimbo za hamasa maarufu kama chenja

. 💥MUDA WA KULALA
Wakati tupo wazalendo muda wa kulala haukua constant kutokana na mfumo uliopo kwa maana tulikua tukihesabu namba na kuitwa majina ndipo unaenda kulala,siku zingine tulikua tunalala saa nne ,nyingine saa tano zingine saa tatu na nusu

💥 MUDA WA KUAMKA
muda wa kuamka ulikua saa tisa alfajiri tunafoleni tunahesabiwa namba tunaenda kwenye majukumu kama vile kufanya usafi maeneo ya kambi na wengine kwenda bwawani kwa ajiri ya maji ya bustani,sasa hapa wengi wao wanaanza kuona maisha magumu kutokana na muda ambao wamezoea kuamka wakiwa kwao na hapa wengi wao wale wa MABASI YA NJANO😁 utawaona wanalalamika zaidi kutokana na ulaini walionano
💥MUDA WA CHAI
muda wa chai ni pale watu washafanya shughuri tofaut tofauti kama vile walioenda shamba na kazi zingine wanarudi kikosini na kujumuika wote kwa ajiri ya chai ilikua ni saa nne kamili,unapatiwa mkate na chai ambayo tulikua tunakunywa kwa ndani ya saa moja na sio kwa dakika kama wasemavyo walimwengu.
Baada ya chai tunafoleni tena then wanatugawa kwa vitengo mfano shamba ,ujenzi na usafi na ingine zaidi kwa idadi

💥 CHAKULA CHA MCHANA
Ilikua ni saa saba kamili,wakati huo watu wote waliokua kwenye vitengo wanarudi wanakusanyika kwa ajiri ya chakula cha mchana,tulikua tunakula ugali,maharage na mboga zingine,pia nyama ilikua mara tatu kwa wiki.
Kama ilivyo jeshi"JESHINI KILA KITU NI KIPINDI PIA KULA NAKO NI KIPINDI,KULA NI LAZIMA HAUTAKIWI KUKUTWA NJE YA ENEO LA CHAKULA MUDA WA KULA" ,Baada ya kumaliza kula tunakusanyika tena na kuendelea na shughuri ndogo ndogo
Hapo muda wako wa kupumzika ni wakati wa kula na kulala sasa kama ilivyojesshi. "JESHINI SIO NYUMBANI" hapa sas magari ya njano wanalialia maisha magumu😁,jeshini kuna muda ulikua unapewa upumzike ukiwa kitengoni ukiwa umemaliza kazi kwa wakati maarufu kama "kula tano"

💥CHAKULA CHA USIKU
TUlikua tunakula saa 12 hadi saa moja,wakati wa kula ukifika kazi zote zinasitishwa.
Chakula kilikua wali maharage na chai kila siku pia kulikua na pilau na nyama baada ya hapo tunafoleni kwa ajir ya kuita majina tayar kwa kulala

🤔🤔🤔🤔🤔🤔
Kuna watu walikua wanatoroka kwa kuona maisha magumu has MABASI YA NJANO ni walaini sana
💥 BAADA YA KUFUNGUA KOZI
hapa unakua unepandishwa cheo na kuitwa KURUTI na sio mzapendo tena hapa sas kulala ni saa 6 kuamka saa tisa
Hapa ndo kunamazoezi madogo madogo ya jeshi
Hapa wengi hutoroka hasa walain

Kutoroka kupo unaweza kutoroka ukarudi jiona ni wewe tu hapa kuna kitu tunaita "SIFA WEPESI" ukiwa mzito kila kitu utashiriki ila ukiwa mwepesi unatoroka hadi siku ya posho😁 unahisi kuna mazoezi

Jeshini ni kwa kiasina sio kama wasemavyo mwalimwengu 📌🔨🔨
 
Mtanzania yoyote yule anayekataa kwenda Mafunzo ya JKT au Kumkata Mwanae kwenda Mafunzoni huko hana Akili.
 
Kwani kuna mtu anategemea kwenda JKT kula maisha, kama mtu anataka mtoto wale ale maisha si kuna sehemu nyingi za vacation anaweza kumpeleka,
Ukakamavu hauwezi kufundishwa kwa kubembeleza mtoto.

BTW mzazi yeyote mwenye akili timamu hawezi kumzuia mtoto wake asiende jkt kisa atateseka, wakati kila mwaka watoto wengi tu wanaenda na wanarudi salama kabisa.
 
Tatizo ni imani potofu na ujinga ulipo katika familia zetu
 
Mkuu, mbona wengi sana wanasema ivo kwamba Jeshi shoo shoo.
kazi ipo ila sio kama watu wanavyovumisha mkuu.
Mimi jkt nimeenda nimeona kawaida mara nyingi watu ambao wanasema hivyo washazoea ulaini
 
Siyo kugumu kweli kama usemavyo na siyo kuna urahisi huo kuna machaka ukiingia unagangamala kweli ukiwazia kurudi nyumbani unarudi kweli. Kuna chaka la miyala hapo pwani oya mzee siyo kinyonge.
Sijasema kugumu sana mkuu ila ni kawada kikubwa ni "KUFUNGUA MOYO"
 
Yaah ni kweli unajua binadamu tunatofautiana mitazamo katika mambo tofauti, ila ni kweli kabisa ukizingatia na nature ya mafunzo ni jambo la kawaida. Mfano uende tisa mbili alafu unataka kulala mpaka saa 2 asubuhi itakuwa utani Sasa.
 
Tatizo watu wanadanganyana sasa mtaani kuhusu jeshini.
✅️mfano wakat nipo kambi X kuna watu wawili walifariki
Nilivyorudi mtaani watu walikua wanacomplain sana kwamba watu wamekufa wakati wanafanya mazoezi means mazoezi yalikua magumu kupitiliza
✅️wakati mi nipo kwenye hiyo kambi X watu hao ambao walifariki nawafahamu na walikua ni wagonjwa wa kudumu na wote vifo vyao vilisababishwa na afya zao
 
Back
Top Bottom