Unywaji wa mafuta gari ndogo

Unywaji wa mafuta gari ndogo

Ulaji wa mafuta wa gari unategemea Vitu vingi hata iwe gari ndogo Kama ist

1.Ubora wa barabara , unatumia njia gani Mara kwa Mara Mana matumizi ya kuendesha lami na off-road Ni tofauti.

2. Ubora wa matairi, kuweka tairi au rims tofauti na maelekezo ya mtengenezaji , sometimes inachangia.

3. Kuweka mafuta ya kuunga unga, Lita 2 Mara Lita 3 Mara moja , kwa ufahamu wangu gari ikiwa na mafuta mengi inatumia vzr kuliko yenye mafuta kidogo.

4. Aina ya uendeshaji , jaribu kuendesha usizidi rpm 2,000 Yani gari ijiongeze speed yenyewe hii inasaidia

Hayo yote Ni nyongeza tu au kukumbusha ilihali najua wengi mnaendesha vizuri na kuzingatia service

Tofauti ya gari ndogo zinazotumia 1NZ engine consumption ya 12km per liter Ni constantly Japo engine ikiwa Bado mpya kabisa na yenye matunzo yote ndo inaweza kufika hizo 18km.
 
Mimi nilikuwa nikisafiri na ractis old model ilikuwa inaenda 17/L ila nikiwa mjini zinapungua kutokana na foleni.
Nimejikuta naipenda Ractis rafiki yangu anayo. Nataka niinunue unaweza kusaidia kuzijua sifa zake au nikimbie
 
Mkuu nimefanya research kama yako sana kitu kinachopelekea mafuta kutumika sana
1. Service ya gari sana sana coil na plugs zile hizi ndo zinachangia sana ulaji wa mafuta ya gari sababu kama una coil zilizoisha na sio original unywaji wa mafuta utaenda sana unaweza shangaa hadi 8km per liter

2. Aina ya safari kama ukiwa na trip ambayo unasimama sana na kwenda ile kwenye foleni kupunguza mwendo kwenye bumps zinachangia sana utumikaji wa mafuta sababu ile unavoanda kuipa gari nguvu kwa kukanyaga mafuta hua yanaenda sana speed 0 kwenda 40 hapo, na hii binafsi hata mm na ist nikiwa na safari kubwa ya mbali mkoani naenda hadi 16.5km per liter ila kimjini mjini 10-12

3. Matumizi ya AC Hasa ukiwa kwenye foleni una ac inapepea tu hii nayo inachangia sana matumizi ya mafuta kwenda sana hasa mda wa jua kali

Hayo ni machache yanayosababisha utumiaji wa wese kwenda
 
Kumbe unaweza kua gari cc990 ikala wese kama Subaru Forester XT 🤣
 
Back
Top Bottom