Unywaji pombe salama na bora kiafya

Apr 9, 2024
7
3
Naomba kujua unywaji pombe salama na bora kiafya ni kiwango gani kwa siku?
Bia ni kiasi gani na pombe kali konyagi au K.VANY ni kiasi gani? Wadau naomba kujuzwa kiwango sahihi kwa siku.
 
Naomba kujua unywaji pombe salama na bora kiafya ni kiwango gani kwa siku?
Bia ni kiasi gani na pombe kali konyagi au K.VANY ni kiasi gani? Wadau naomba kujuzwa kiwango sahihi kwa siku.
Hutegemea umri wa mtu, jinsia, historia ya magonjwa, uzito wa mwili na ulaji wa mtu. Kwa ujumla kama wewe ni mtu mzima wa umri (25-80) ukiywa bia 4 kwa wiki (500mls each) utakuwa vyema. Robo glasi ya wine ni nzuri kwa afya yako. Kama ni spirits kama Konyagi, Valeur n.k. nusu glasi kila baada ya siku 2 sio mbaya.

Kula na kushiba kabla ya kunywa. Epuka kutengeneza uraibu (adiction) kutokana na pombe, ni mbaya sana.

Kanuni nzuri; usinywe hadi kulewa.
 
Hakuna unywaji sahihi, kiwango chochote ni hatarishi

Hii imegundulika hivi karibuni
Screenshot_20240510-210142~2.png


Lakini bado unaweza ukanywa tu.

Kunywa ni kama kununua furaha, unajiskia mwepesi sasa hivi, kesho unarudi kawaida

Kwahiyo ile mantiki kwamba unajiua taratibu ili upate furaha inaeleweka kwa mtazamo wangu

Hata hivyo mitindo mingi ya maisha siku hizi inatuua taratibu.
 
Back
Top Bottom