Unyanyasaji wa kutisha kwa mtoto Nasra mkoani Morogoro: Aishi kwny box kwa miaka 4!

yaani mwisho wanaombwa wasamaria wema watoe msaada,wakati baba mtu yupo na ni mtumishi?miaka yote anatoa hela hajui mtoto anaendeleaje?Hivi nani katuroga?tunataka sympathy kwa ujinga wetu.Pole mtoto
 
Nimesoma Uhuru ya leo eti baba anasema kila alipokuwa anaenda kumsalimie binti yake alikuwa anaambiwa amelala. Hivi huyu baba ana akili timamu kweli! Akapimwe akili kwanza!
Mtoto alipoulizwa baba yake alimpoint yeye. Kwa hiyo mtoto ni ana maono ya ajabu yasiyo ya kibinadam kumjua baba yake wakati kila wakati baba akifika yuko usingizini. Ujinga
 
Chakusikitisha! Mama yake mdogo/ mlezi alipo hojiwa alipohojiwa alisema sababu ya kumlea vile yule mtoto nikotokana na kwamba mtoto ni muathirika ( HIV POSTIVE) akijitetea anasema aliona atawaambukiza watoto wake, nakuamua kumtenga. Nachoona hapa bwana MVUNGI kapeleka ugonjwa huu kwenye familia yake kwa umalaya wake. Kwahili ameniumiza zaidi. POLE MAMA MVUNGI NAJUA UPOKATIKA WAKATI MGUMU SANA.
 
So sad,why,amkosa nini huyo mtoto,hata kama hakuwa na uwezo wa kumtunza kwanini asimpeleke kwa baba yake au sutawi wa jamii?she desrved to be punished,severe punishment iwe ni fundisho kwa wanawake wengine wenye tabia kama hizi kwani naona sasa imekuwa ni matukio ya kawaida kuwatesa watoto wasio na hatia.
 
Chakusikitisha! Mama yake mdogo/ mlezi alipo hojiwa alipohojiwa alisema sababu ya kumlea vile yule mtoto nikotokana na kwamba mtoto ni muathirika ( HIV POSTIVE) akijitetea anasema aliona atawaambukiza watoto wake, nakuamua kumtenga. Nachoona hapa bwana MVUNGI kapeleka ugonjwa huu kwenye familia yake kwa umalaya wake. Kwahili ameniumiza zaidi. POLE MAMA MVUNGI NAJUA UPOKATIKA WAKATI MGUMU SANA.

HUYU MAMA MWEHU! ALIAMBIWA UKIMWI UNAAMBUKIZA KWA KULALA NA MUATHIRIKA! JE NI KWELI ALIMPIMA MTOTO NA KUKUTA NI POSITIVE! MIE SIAMINI ASEMAYO KWANI ANGEKUWA POSITIVE KWA MATESO ALIYOKUWA ANAPEWA ANGESHAKUFA SIKU NYINGI! napata hasira na hiyo familia Mungu wangu nisaidie. Ningekuwa hapo Morogoro wakati mama huyu anakamatwa! ningeondoka na sikio lake! nyambafu kabisa
 
kama mtumishi wa umma anatakiwa kuheshimu haki za binadam,,,,,kwa hili amekiuka bora afukuzwe kazi ikiwa wakwake tu amemshindwa je wengine atawaweza?
 
Amepimwa, mtoto nasra si muathika wa ukimwi, ilikuwa janja ya walezi katika kutapatapa, nilifanikiwa kumuona mtoto huyo akiwa hosp Moro, ukweli anaendelea vema na ameanza japo kushika vitu. Natumaini baada ya kupelekwa Dar afya yake itaboreka sana. Mungu mbariki na NASRA.
 
kweli angekuwa na virus angekuwa ashakufa siku nyingi. Mungu mjalie mtoto Nasra afya njema
 
Its so painful. Hivi hivi vitendo vimefanywa na binadamu huyu huyu naye mfahamu. Kwakweli Mwenyezi Mungu namuomba aingilie kati.
 
Its so painful. Hivi hivi vitendo vimefanywa na binadamu huyu huyu naye mfahamu. Kwakweli Mwenyezi Mungu namuomba aingilie kati.
Binadamu wakati mwingine wana roho mbaya zaidi ya mnyama........it is so painful kwa kweli. Inasemekana mtoto mwenyewe amefariki.
 
Hivi huyu mama ana kizazi na watoto? Hii itakuwa laana kwa kizazi chake. Na baba wa mtoto unatoa matunzo hata mtoto huendi kumwona? Msomi mzima. Damu yake itatafuna wanao.
 
Wapendwa huyu mama aliyekuwa na huyu mtoto ameshanyongwa maana hamna haja ya kujaza jela zetu na watu kama hawa....alaaniwe mpaka ashangae...
 
Majina ya wahusika yanalenga asili ya tatizo. Kule hakuna upendo.
 
najuta kuusoma uzi huu,,,,tumbo langu limevurugika ghafla nahisi kichefuchefu kwa ukatili wa kiwango hiki
 
Polisi wanafaa waanze kumbana Baba mwenye mtoto!
Mtoto anamfahamu Baba yake ,kwa maana hiyo nikwamba anamtembelea mara kwa mara sasa alishindwaje kuona hiyo hali/afya ya Mtoto muda wote huo?

Uweledi unahitajika katika hatua hii ilikuhakikisha haki inatendeka.

Mzazi wa aina hii hafai kukaa Uswahilini .Haiwezekani hata kama ni mtoto wa nje ya Ndoa wajibu wa kumlea unabaki pale pale bila kujali unandoa ya aina gani.

Uhai wa Mtu hauwezi kulinganishwa na hofu ya kuvunjika Ndoa.

Kauli ya mwisho ya ‘mtoto wa boksi’

Kuzikwa kishujaa
Ofisa ustawi wa jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungatuti alisema mwili wa mtoto huyo utasafirishwa leo kwenda Morogoro.
Ngungamtitu alisema mazishi ya Nasra yatatanguliwa na ibada itakayoambatana na utoaji wa heshima za mwisho katika Uwanja wa Jamhuri, hatua ambayo alisema inatokana na baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi kuwa mmoja wa watuhumiwa wa mateso yake.
 
Back
Top Bottom