Unyanyasaji wa kutisha kwa mtoto Nasra mkoani Morogoro: Aishi kwny box kwa miaka 4!

Ujinga upuuzi na upumbavu tena nasikitika zaidi hata ustawi wa jamii wanatumia jina hilo kwenye taarifa zao
Wakuu nadhani wote mnakumbuka mtoto Nasra aliyefanyiwa unyama wa kutisha na mzazi wake
Alimficha zaidi ya miaka 4 toka kuzaliwa kwake mungu alivyo mkubwa mtoto alikuja kuonekana na kupelekwa hospitali kwa matibabu
Kwa bahati mbaya alifariki dunia siku kadhaa baadae mungu ailaze roho ya nasra mahali pema peponi AMEN.
Swali:Hivi ni haki kumwita Nasra ni mtoto wa box?
Kama kweli tunataka kumtendea haki mtoto huyu na abaki kama mtoto shujaa kwenye historia yake
Kwa heshima tutumie jina lake NASRA
Hii sio haki hata kidogo kumwita mtoto wa box upumbumbavu mkubwa naulaani maisha yangu yote.
 
Naunga Hoja Mkono 100%

Hili swala mkuu linaniumiza sana inamaana yule mtoto asingefariki mungu akamjalia kufiki umri wa utu uzima kuna watu wangekuwa wanamnyanyapaa kwa kumwita we ni mtoto wa box
Mbaya zaidi waasisi wa jina hilo ni watu na akili zao timamu wakiwepo wanahabari aaaggrrrhhhh..
 
Yaani mtuhumiwa namba moja hapo ni baba wa mtoto. Miaka minne hajawahi kumwona mwanawe kweli? Mbona mtoto amemtambua kama yeye ndiye baba!!, yeye yupo Morogoro mtoto yupo Morogoro, eti anatuma pesa tu za matumizi kwa mama Mkubwa wa Mtoto!
Inamaana hajiulizi Mtoto anakwenda clinic au la? Mtoto anafikisha miaka minne hakuwa hata na wazo la kumpeleka japo chekechea jamani?
Huyu baba ni muuaji, labda alimtoa kafara mwanawe, haiwezekani kabisa yaani.
Inasikitisha
 
Back
Top Bottom