Unyanyasaji wa kutisha kwa mtoto Nasra mkoani Morogoro: Aishi kwny box kwa miaka 4!

Qsm

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
414
250
Wana JF wote tuungane kwa pamoja bila kujali itikadi zetu, dini zetu kukemea unyanyasaji wa watoto hapa nchini. Katika Taarifa ya Habari jana nimejionea mtoto wa miaka minne Nasra aliyeathirika kwa unyanyasaji wa kutisha na mama yake mdogo baada ya mama yake mzazi kufariki dunia.

Tukio hilo limeniliza na kujiuliza maswali mengi! bila kupata jibu. Hivi hata majirani walishindwa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola kwa muda wote huo mpaka mtoto amefikia vile!! Ebu tupeane mawazo njia mbadala ya kushughulikia na kukomesha vitendo hivyo.
Rashid Mvungi akimuangalia mtoto wake Nasrah Rashid (4) ambaye ni mlemavu wa viungo aliyefungiwa
chumbani na kufichwa kwenye boksi bila ya kufanyiwa usafi tangu akiwa na umri wa miezi tisa.


Morogoro. Mwanamke aliyetambuliwa kuwa ni Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro juzi alishushiwa kipigo na wananchi kutokana na kumficha mtoto wa marehemu mdogo wake kwenye boksi kwa miaka minne.

Tukio hilo lilitokea juzi saa nne asubuhi baada ya majirani zake kutoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Dia Zongo kuhusu mtoto huyo, Nasra Rashid, kufichwa ndani ya boksi tangu akiwa na umri wa miezi tisa.

Zongo alisema majirani hao walimweleza pia kuwa jirani yao huyo hamfanyii usafi mtoto huyo wala kumtoa nje.

Baada ya kupata taarifa hizo, Zongo alimtafuta Mwenyekiti wa Mtaa huo, Tatu Mgagala na kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo na kumhoji mwanamke huyo ambaye alikuwa akijibu kwa kubabaika.

Moja ya maswali aliyoulizwa ni idadi ya watoto wake na akajibu kuwa ana wawili lakini wakati akiendelea kujibu maswali, ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa, hivyo kuwapa wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa mwanamke huyo kwa nguvu na kumkuta mtoto Nasra akiwa ndani ya boksi.

Ofisa mtendaji huyo alisema wakati wakimtoa mtoto huyo ndani ya nyumba, kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe walianza kumshambulia mwanamke huyo na kumlazimu mtendaji kutoa taarifa polisi.

Alisema muda mfupi baadaye, polisi waliwasili na kumkamata Mariam na kumpeleka katika ofisi ya kata ambako aliwekwa chini ya ulinzi.

Baadaye aliwekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi, Morogoro na mtoto alipelekwa Ofisi za Ustawi wa Jamii.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema wanaendelea kukusanya taarifa za tukio hilo ikiwamo matokeo ya vipimo vya madaktari kuhusu afya ya mtoto huyo kabla ya kuchukua hatua zaidi.

Kamanda Paulo alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa kosa la kumfanyiwa mtoto vitendo vya kikatili.

Hata hivyo, kamanda huyo alisema polisi wanakadiria kwamba mtoto huyo alianza kufichwa kwenye boksi hilo akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu.

Utetezi wa Mariam

Akijibu maswali ya polisi, mwanamke huyo alikiri kuanza kumlea mtoto huyo tangu akiwa na umri wa miezi tisa baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia mwaka 2010.

Pia mtuhumiwa alikiri kwamba mtoto huyo hajawahi kupewa chanjo yoyote wala kupelekwa kliniki.

Alikuwa akitoa maelezo hayo huku akiwa amemshikilia mtoto huyo aliyetapakaa uchafu ikiwamo haja kubwa na ndogo alizokuwa akitoa ndani ya boksi na kusema kwamba mara ya mwisho alimwogesha Julai mwaka jana.

Pia alisema alikuwa akimwekea chakula na maji ndani ya boksi lililokuwa nyuma ya mlango wa chumba.

Mume wa mwanamke huyo, Mtonga Ramadhani anayefanya biashara katika Soko la Mawenzi, Morogoro ambaye pia anashikiliwa na polisi, alidai kuwa hakuona sababu ya kutoa taarifa za kufichwa kwa mtoto huyo kwa sababu hamhusu na wajibu wake ni kutafuta chakula.

Alivyonaswa

Baadhi ya majirani wa mwanamke huyo ambao hawakutaka kutajwa majina, walisema Mariam alihamia katika nyumba hiyo mwaka 2010 na hawajawahi kumwona mtoto huyo akitolewa nje wala kufanyiwa usafi.

Walisema mtoto huyo alibainika baada ya kusikika akikohoa na kulia nyakati za usiku, jambo lililozua wasiwasi kuwa huenda mtuhumiwa alikuwa mshirikina anayefuga misukule.

Baba wa mtoto

Baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi alisema hakujua kama mwanaye alikuwa analelewa katika mazingira hatarishi.

Akihojiwa na Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu, Mvungi alisema alimzaa mtoto huyo nje ya ndoa na amekuwa akituma fedha za matumizi kwa mama yake mkubwa.

Mvungi ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, alisema baada ya mzazi mwenzake kufariki dunia alishindwa kumchukua mtoto wake kwa sababu tayari alishakuwa na mke.

Alisema hata hivyo, alikubaliana na upande wa familia ya marehemu kuwa mtoto huyo alelewe na mama yake mkubwa.

Mtoto azungumza

Wakati Mvungi akihojiwa, baadhi ya watu waliofurika katika Ofisi za Ustawi wa Jamii walianza kuangua kilio baada ya mtoto huyo anayeonekana mlemavu kuanza kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na maofisa wa Ustawi wa Jamii.

Swali: Unaitwa nani:

Jibu: Naitwa Nasra

Swali: Ulikuwa unapewa chakula gani?

Jibu: Ubwabwa na maharage

Swali: Una umri wa miaka mingapi?

Jibu: Miaka minne

Swali: Baba yako yuko wapi?

Jibu: (anamwonyesha kwa kidole)

Ngungamtitu alisema huenda ulemavu wa mtoto huyo umetokana na kuishi kwenye boksi au kukosa lishe yakiwamo maziwa ya mama, hewa safi na upendo.

Alisema si ajabu mtoto huyo kushambuliwa na magonjwa mbalimbali kama minyoo, pneumonia, utapiamlo na malaria, ndio maana aliagiza apelekwe katika Hospitali ya Mkoa kwa uchunguzi, chanjo na tiba.

Ofisa huyo alisema matibabu mengine atakayopatiwa ni pamoja na kunyooshwa viungo, mikono na miguu iliyolemaa.

Ngungamtitu aliwaomba wasamaria wema, mashirika ya dini na wadau mbalimbali kutoa misaada ya nguo, lishe, matibabu na mahitaji mengine kwa mtoto huyo.

Source: Mwananchi

 

Qsm

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
414
250
Kwa kweli unyanyasaji wa watoto huwa unaniumiza sana.

Ni moja ya mambo ambayo huniharibia kabisa siku yangu.

Kwa kweli my Bro! sikulala kabisa! yaani toka kutekwa nyara kwa wtt wa kike Nigeria na hili pia la mtoto wa kike tena kunyanyaswa na mwanamke mwenzetu! nashindwa kuwaelezea hali niliyonayo kuhusiana na masuala haya yakutisha hasa ikizingatiwa kuwa sisi ni wazazi!
 

kabuya

Member
Jun 12, 2013
85
125
Inauma sana hiki si kitendo cha kawaida kwa binadamu mwenye akili timamu huyu mama apimwe akili naona siyo mzima amewaliza watu wengi sana kwenye hili tukio
 

ram

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,045
2,000
Kilichonishangaza ni kwamba babake mzazi yupo, yaani huyu baba alikuwa haendi hata kumtembelea mtoto wake kujua anaishije? pamoja na hao waliokuwa wanamtesa kukamatwa nadhani hata babake mzazi anatakiwa kukamatwa, hata kama alikuwa hata familia yake ijue kama ana mtoto nje ya ndoa bado alitakiwa kupanga muda wa kwenda kumuona mtoto angala kila mwezi kama si kila wiki
 

nyamboto1

Member
Apr 22, 2014
30
0
Kilichonishangaza ni kwamba babake mzazi yupo, yaani huyu baba alikuwa haendi hata kumtembelea mtoto wake kujua anaishije? pamoja na hao waliokuwa wanamtesa kukamatwa nadhani hata babake mzazi anatakiwa kukamatwa, hata kama alikuwa hata familia yake ijue kama ana mtoto nje ya ndoa bado alitakiwa kupanga muda wa kwenda kumuona mtoto angala kila mwezi kama si kila wiki

Yupo tena nimfanyakazi waserikali anafanya ded morogoro then mume wa huyo mama anaulizwa Kwanini hakutoa taarifa kwakitendo chamkewe anajibu huyo mtoto anihusu mimi Sio ndugu yangu..
Kweli mtu mzima anajibu hivyo, Huyu baba kama anawatoto atakuwa ni mzalishaji sio mzazi..
Ukatili dhidi ya watoto unazidi kila uchao
 

Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,193
2,000
Kuna watu unaweza kujiuliza wana utu au mioyo ya nyama ya huruma kama watu wengine au wana mioyo ya chuma isiyo na chembe ya kuhisi lolote. Tukio lile kwa kweli linatisha na kuhuzunisha mtoto kuwekwa kwenye box muda wote huo huyo baba hakujishughulisha kujua mtoto wake anaishije au analelewaje?
Kuna jingine la Tanga pia juzi mtoto nae amefungiwa kwenye nyumba anajisadia humo humo na chakula anawekewa humo humo bila kujali kama kuna uchafu au hakuna
Naamini kuna wengine wanateseka sana au wamefungiwa ndani ya nyumba kwa mateso ni vile nyumba za watu zina milango kutoweza kujua siri zilizomo ndani
 

ram

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,045
2,000
Tena ningekuwa mimi, ningeanza na babake mzazi, inaonekana ameshatelekeza wengi, mfanyakazi wa serikali, fundi, unashindwa kumtunza mtoto, mtoto anakalishwa kwenye bozi wewe upo tu....NO! Huyo baba ashikwe, sasa aibu kaipata na familia imeshajua kama ana mtoto hadi amekuwa mlemavu

Yupo tena nimfanyakazi waserikali anafanya ded morogoro then mume wa huyo mama anaulizwa Kwanini hakutoa taarifa kwakitendo chamkewe anajibu huyo mtoto anihusu mimi Sio ndugu yangu..
Kweli mtu mzima anajibu hivyo, Huyu baba kama anawatoto atakuwa ni mzalishaji sio mzazi..
Ukatili dhidi ya watoto unazidi kila uchao
 

Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,193
2,000
Tena ningekuwa mimi, ningeanza na babake mzazi, inaonekana ameshatelekeza wengi, mfanyakazi wa serikali, fundi, unashindwa kumtunza mtoto, mtoto anakalishwa kwenye bozi wewe upo tu....NO! Huyo baba ashikwe, sasa aibu kaipata na familia imeshajua kama ana mtoto hadi amekuwa mlemavu
ram unaficha nini kama mtoto unaye na atakuja kwako muda ukifika je ni bora kusema hapa mwanzo wa ndoa yako au ni bora kuja kusema mwishoni
Unaogopa nini kama ushapata watoto huko nje huko
Ninavyowapenda watoto na unamuona mtu anamtesa mtoto kiasi kile inaumiza sana aise
 
Last edited by a moderator:

Qsm

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
414
250
Ni kweli kabisa baba mzazi awe mshtakiwa wa kwanza! ni ajabu je alipokuwa akienda kumtembelea mtoto hakugundua matatizo yanayomsibu mwanaye! Kweli dunia ina mambo! Mtoto alivyomzuri jamani ee Mwenyezi Mungu mjalie arudi katika hali ya kawaida katika ukuaji wake!
 

Geofane

Member
Feb 17, 2014
23
0
Wana JF wote tuungane kwa pamoja bila kujali itikadi zetu, dini zetu kukemea unyanyasaji wa watoto hapa nchini. Katika Taarifa ya Habari jana nimejionea mtoto wa miaka minne Nasra aliyeathirika kwa unyanyasaji wa kutisha na mama yake mdogo baada ya mama yake mzazi kufariki dunia.

Tukio hilo limeniliza na kujiuliza maswali mengi! bila kupata jibu. Hivi hata majirani walishindwa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola kwa muda wote huo mpaka mtoto amefikia vile!! Ebu tupeane mawazo njia mbadala ya kushughulikia na kukomesha vitendo hivyo.

Inauma sana kwakwel,ifike mahali tubadilike watanzania. tujiulize kama huwez kumlea mtoto wa ndugu yako kwasababu hayupo dunian nan atakulelea wa kwako? tuachane na hili la kusema hanihusu,kwan madhara yake ni makubwa sana kwa mtoto na kwa jamii. Tuguswe na turipot tunapoona hali isiyo ya kawaida kwa watoto ndan ya jamii zetu wanaokutwa na hatia hatua kali zichukuliwe dhidi yao liwe fundisho.
 

samilakadunda

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
1,760
1,500
tisa kumi, mimi ni huyu baba wa huyu mtoto navomfahamu kwa utanashati wake, weupe wake urefu wake na jinsi anavo ongea akiwa hapa ofisini huwezi amini kwamba ana mtoto anayeteseka kiasi hicho, MVUNGI?????? SITAKI KUAMINI,.
 
  • Thanks
Reactions: ram

Safety last

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
4,230
2,000
kilichoniuzi ni babake yuponimeumia sana huyu baba ningekuwa hakimu angenikom a ningefyeka mshahara wake wote uende kwa mtoto amesababishia mtoto kilema so sad
 

Safety last

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
4,230
2,000
kilichoniuzi ni babake yuponimeumia sana huyu baba ningekuwa hakimu angenikom a ningefyeka mshahara wake wote uende kwa mtoto amesababishia mtoto kilema so sad
 

NullPointer

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
3,467
2,000
makalio tu, hamna binadamu hapo, huyo baba, yule mwanamke wote makalio tu, sheria ichukue mkondo wake, wapewe adhabu kubwa sana kutoa fundisho kwa wengine, afu msako bora uanze nahisi kuna watoto wengi wanafanyiwa ujinga huu. Tunajitahidi kupunguza illeterates bongo afu makalio hawa ndo wanachochea.
 

Mp Kalix2

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
5,946
2,000
Mtoto azungumza

Wakati Mvungi akihojiwa, baadhi ya watu waliofurika katika Ofisi za Ustawi wa Jamii walianza kuangua kilio baada ya mtoto huyo anayeonekana mlemavu kuanza kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na maofisa wa Ustawi wa Jamii.

Swali: Unaitwa nani:

Jibu: Naitwa Nasra

Swali: Ulikuwa unapewa chakula gani?

Jibu: Ubwabwa na maharage

Swali: Una umri wa miaka mingapi?

Jibu: Miaka minne

Swali: Baba yako yuko wapi?

Jibu: (anamwonyesha kwa kidole
)


Polisi wanafaa waanze kumbana Baba mwenye mtoto!
Mtoto anamfahamu Baba yake ,kwa maana hiyo nikwamba anamtembelea mara kwa mara sasa alishindwaje kuona hiyo hali/afya ya Mtoto muda wote huo?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom