Unyama mbaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unyama mbaya

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sipo, Aug 28, 2009.

 1. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mwili wa kichanga waopolewa ******
  Mwili wa mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja umekutwa ndani ya shimo la choo Jijini.

  Kamanda wa mkoa wa kipolisi Kinondoni, Mark Kalunguyeye, amesema tukio hilo limetokea mishale ya saa 4:00 asubuhi nyumbani kwa Bi. Asha Said, 60, pale Mwananyama Kisiwani.

  Akasema waili wa kichanga hicho unadaiwa kuwa ulitupwa katika shimo hilo la choo na mwanamke ambaye hajafahamika.

  Kamanda Kalunguyeye amesema mwili huo wa motto uliopolewa toka ****** na askari wa kikosi cha Zimamoto na uokoaji cha Jijini.

  Akasema mwili mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mwananyamala na hadi sasa Polisi wanaendelea kumsaka mwanamke aliyefanya kitendo hicho cha kinyama ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria

  Chanzo: Alasiri 27/08/09
  www.ippmedia.com

   
Loading...