Ununuzi Mitambo ya IPTL na Dowans,vigezo vinalingana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ununuzi Mitambo ya IPTL na Dowans,vigezo vinalingana?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmaroroi, Mar 14, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Katika tamko la Waziri wa Nishati na Madini la kudhibitisha kufungwa kwa mjadala wa Serikali kununua mitambo ya Dowans na badala yake Serikali inafanya mpango wa kununua mitambo mipya yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 150,Waziri alielezea kushangazwa kwake na kamati ya Bunge kukataa kununuliwa kwa mitambo ya Dowans iliyotumika lakini siku za nyuma ilikubali kununuliwa kwa mitanbo ya IPTL ambayo nayo imekwishatumika.

  Je mitambo ya IPTL ilikuwa na mlolongo wa matatizo kama ilivyo ya Dowans na kama ni tofauti Waziri hajui,wana JF karibuni tuelimishane.
   
 2. M

  Mkora JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  IPTL mwenyewe anajulikana lakini Dowans hamna mwenyewe sasa tutanunua kwa nani ?
   
 3. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani Waziri anaendeleza harakati za kuwafanya watanzania kuwa hawanazo. Katika suala la dowans ilikuwa ni kununua mitambo, wakati suala la IPTL ni kununua mkataba, yaani sasa iwe ni mali ya TANESCO ili wawe wanaendesha kama mtera na kwingineko. Ingeweza kufananishwa endapo dowans wangekuwa na mkataba hai na TANESCO, lakini wao walichonacho ni mitambo tu!
  WAZIRI HUYU UCHURO, ni zao la mafisadi!
   
 4. n

  nzala Member

  #4
  Mar 14, 2009
  Joined: Dec 24, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  huyu waziri, inaonekana ni bendera fuata upepo,usije ukashangaa kesho kuwaita waandishi wa habari na kutangaza azma ya serikali kununua hiyo mitambo ya DOWANS.
   
 5. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyu waziri ni wale wale watoto wa mafisidi,kwanza atueleze DOWANS ni nani? aache ngonjera zake,tunataka tumjue mmliki halali wa dowans na tujue aliingia mkataba na nani? ila wana jf uwezo baadhi wa mawaziri wetu kuchambua mambo ni mdogo sana mpaka inatia huruma!
   
 6. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #6
  Mar 14, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jibu ni rahisi sababu Kama Mwakyembe alivyosema kuwa watanzania wakiwemo wabunge si mabwege tena kama zamani wamebadilika .Kwa sababu wamebadilika usitarajie yale ya ubwege wa zamani yarudie.

  Bunge na wabunge wa wakati ule walikuwa mabwege wa kutupwa ndio maana walishauri hivyo sasa hivi ubwege umewatoka ndio maana hawataki Dowans inunuliwe.Kwani Ngeleja alitakaje waendelee wabunge kuwa mabwege?

  Ila naona kuna kitu Ngeleja labda anataka au katumwa amchokoze mtu Fulani.Anauliza yule wa IPTL mbona hakufanyiwa kitu wakati huyu wa Richmond na Dowans anashupaliwa sana wakati wote ni wale wale maruhuni?.Ninachomshauri Ngeleja afunge domo lake analipanua mno.Masinga singa hujuana kwa vilemba asije kuumia.Kujifanya kibaraka sana wa singa singa mmoja na kumtukana singa singa mwingine wakati wewe sio singa singa kwaweza kumuumiza mwisho wa siku hata kama kawekwa na masinga singa wote wawili au mmoja wao.

  Nafikiri na yule mhusika wa IPTL taarifa umezipata za kwa nini unaandama wenye Dowans wakati kule IPTL ambako uko saaana hujigusi.Ngeleja angependa kujua why.Tupe jibu kupitia press kama Ngeleja alivyopitia press.
   
 7. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkataba wa IPTL ungeweza kuvunjwa kama serikali yetu wangetaka kufanya hivyo bila kuvunja sheria. Kwa mfano wangejaribu yafuatayo;
  1. Mkataba wa IPTL hivi sasa una zaidi ya miaka 10 na sidhani kama watakuwa hawajafanya kosa lolote hadi hivi sasa litakalotoa sababu ya kuukatisha. Inatakiwa tu serikali waunde timu ya wanasheria wazuri kuangalia loop holes.
  2. Wahusika wakuu wa IPTL wanajulikana hasa kwa kutokuwa safi. Rugemalira, aliyenunua BCom pale UDSM, ana makosa mengi wanayoweza kufuatiliwa na kumfunga ili tu kuimaliza IPTL nguvu na hivyo kuiua kirahisi.
  3. Harassment kwa wamiliki wengineo - The Malaysia mobs (Meachmar), ifanyike kwa bidii ili waelewe wazi kuwa sio safi kuiibia serikali bila kukiona cha moto.
  Tatizo ni kuwa, wanaotakiwa kufanya haya nao wanatamani kupata mikataba kama ya IPTL ili kujineemesha binafsi.
   
 8. t

  tk JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mazingira ya IPTL na Dowans hayana tofauti kabisa. Nadhani Waziri amejieleza vizuri sana.
  1. Wote IPTL na Dowans wameingia nchini kwa matatizo.
  2. Mitambo yote ni iliyokwisha tumika. Infact ya IPTL ni michakavu zaidi.
  3. Wote walikuwa na mikataba na Serikali.
  4. Mitambo yote inadaiwa na Benki.
  5. Hapa inaonyesha wazi kuwa wakina Sitta, Mwakyembe na Shellukindo ni wanafiki kwa kuwa na double standards. Inakuwaje wanatumia hoja ya Sheria ya Ununuzi wa Umma kukataza ununuzi wa mitambo ya Dowans wakati huo huo wanahimiza kununua kwa IPTL. Hapa lazima tumuamini Waziri kwa kuwa ame quote Hansard ambayo huwa haisemi uwongo.
  6. Mwakyembe aliudanganya umma kuwa management ya Tanesco haikupata kibali cha Board yake wakati Waziri Ngeleja anasema Bodi ilitoa kibali. Hapa lazima tumuamini Waziri mwenye dhamana ya Shirika hilo.
  7. Shellukindo na Mwakyembe walikuwa katika kamati hiyo na Sitta alikuwa Spika. Kwa hiyo kama wanakubali walikuwa mabwege mwaka mmoja tu uliopita mpaka wakapigia makofi uamuzi wa kununua mitambo ya IPTL jee huo ujajanja wa hivi sasa wameupata wapi?
  8. Walisema Tanesco na Kamati ya Zitto walikula mlungula kwa kutaka kukiuka sheria.. Kwa vigezo hivyo hivyo na Akina Mwakyembe inaonyesha nao wamekula mlungula kwa IPTL kwa kukiuka sheria hiyo hiyo. Unaona matokeo ya mambo ya kufuatana futana sasa siri yao nayo imefichuka.
  9. Serikali iache woga na ichukue maamuzi kwa maslahi ya taifa. Ikiwa Bunge litaleta maneno basi Rais avunje Bunge warudi kwa wananchi. Kwa mtindo wa sasa wa Primaries za CCM 75% ya wabunge hawarudi. Kwa hiyo hawana msuli wa kupambana na serikali.
  10. Spika Sitta kurudi kwake Bungeni kama Spika kuna wasiwasi asilimia 75 kutokana na anavyotaka kuendesha yeye kila kitu.
   
 9. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kuna tetesi nimesikia kwenye gazeti moja kuwa kwa kina Mwakyembe wana kampuni ya kufua umeme kwa kutumia upepo na wanatarajia kuizia Tanesco....kwa hiyo jamaa wameconclude kuwa ni mgongano wa maslahi ndio chanzo cha upinzani wa kamati ya madini na nishati.....sijui kuna mtu ana maelezo zaidi ya hili
   
 10. A

  August JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  My dear Son Ngeleja, recently i saw an article in one of the news paper that you want to contradict pairliament againtst Government on the issue of Dowans vs iptl that in both situation the issue is used machinery, without elaborating the fact that one contract is live contarct while the other one is a dead one, in a particular the dowans. Sasa kwa akili yako ya kisukuma na ya kisheria on those particular issue are thery the same? mbona nyinyi wasomi wa kitanzania mnapende kujiabisha hivyo kwamba kwa uelewako mdogo tu haya mambo ni sawa? pili mnataka kumuabisha Prof Shivji kwamba aliwafundisha kinyume mbele? au tulimpa wanafunzi wasio faa? Naomba Ngeleja na kundi lake watueleze hili na wachangiaji wengine, lakini mimi kwa uelewa wangu mdogo inaonyesha tanzania haiwezi kuendelea for the next 50 years ikiwa uchambuzi wetu ni kama wa ngeleja, ndio maana naona sisi ni kikwanzo cha maendeleo duniani kama si tanzania tu.
   
 11. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa Mzee Mwanakijiji ameahidi kutoa uhakika wa mmiliki wa Dowans kuwa ni Muarabu wa Oman,kwanini Waziri Ngeleja hakuwahi kumtaja wakati wamiliki wa IPTL wanafahamika?Mwakyembe kuwekeza kwenye sekta ya umeme bila utapeli ni kosa?Na kama RA na JK wanahusika kwa ujio wa huyo Muarabu kwa mgongo wa RA kuna nini kinavichwa.Hawa viongozi wa vificho hadi lini?
   
 12. A

  Audax JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wadau sisi hatuna serikali,watu woote ni wezi maana wale wanaoonekana kutetea maslahi ya nchi ni wabunge,hawapewi wadhifa wowote,cjui tufanye nini!!!!!
   
 13. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  IPTL tunanunua mkataba baada ya kukosa pa kutokea tofauti na DOWANS ambayo si mzigo kwetu tena
   
 14. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Mitambo imetumika katumia nani! si imefungwa mipya na Tanesco ndio wamezindua na wanaitumia? Kutumika ni issue nyepesi sana labda umiliki na namna ilivyoingia ndio dili.

  Serikali hainunui magari yaliyotumika lakini miradi inakuwa na magari baada ya mradi kwisha magari yanaenda serikalini na yanasajiliwa kwa namba za serikali ingali sheria haitaki kusajili magari yaliyotumika. Hii ni sawa na ya Mitambo sababu mwongozo wa mitambo ni pamoja na magari.
   
 15. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Bunge lilipitisha kununua IPTL na mitambo yake kupunguza gharama za umeme kwa kuwa mkataba wake haukuwa na tatizo.Kuhusu Dowans mkataba wake una dasari kwa kuridhi madudu ya Richmond na pia wameifungulia kesi Serikali huko Paris,Ufaransa.Sasa kwa nini Waziri Ngeleja anafananisha mitambo ya Dowans na IPTL,ni kwamba hajapitia vizuri hansad ya Bunge au ana ajenda yake nyingi,tutaona mbele ya safari.
   
Loading...