Uno na Baba lao zilikuwa nyimbo za kukurupuka

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Mtikisiko wa Harmonize kujitoa WASAFI haukuwa mdogo japo japo kila upande ulijitahidi ku play low
Kuna sababu haziwekwi wazi sana lakini kuna moja ambayo ndio inaweza kuwa chanzo.. Na hii ni pale Harmonize alipoamua kuingiza siasa kwenye biashara pengine bila kushirikisha uongozi na viongozi wake kwa kupindua baadhi ya mashairi ya wimbo wake na kusifia wanasiasa

Wimbo asilia ni utunzi wake binafsi lakini gharama za kurekodi nk zilifanywa na WASAFI. Kwahiyo haikuwa sahihi kufanya lolote bila kushirikisha uongozi wa WASAFI ambao waliona hatari iliyopo ya kuchanganya SIASA na BIASHARA.

Pamoja na sababu nyingine zote hatimaye Harmonize alijitoa WASAFI lakini akiwa tayari ameshajitengeneza kwa utambulisho wake wa KONDE BOY.

Inapotokea ajali kishindo cha mwangwi wa sauti hufika mbali lakini walioko karibu hushuhudia majeruhi, vifo na uharibifu baada ya vumbi kutulia. Ni katikati ya Harmonize kujitoa WASAFI akapima upepo kwa kuachia UNO. Kazi yake ya kwanza akiwa nje ya WASAFI

Kwa haraka sana bosi wake wa zamani naye akaachia BABA LAO ili kuuthibitishia umma kwamba yeye bado yuko juu.

Nyimbo zote mbili zina kutambiana ndani yake na mafumbo na kwakuwa hazikuwa na maandalizi ya kutosha zimechuja haraka mno na katika hili Diamond ndio kapoteza zaidi kuliko Harmonize

Kwanza nyimbo zote mbili ni copy n paste. Harmonize anashutumiwa ku copy toka Kenya lakini Diamond iko wazi kabisa ka-copy wimbo alioshirikishwa Kongo DRC uliofanya vizuri sana. Alipokosea pakubwa Diamond ni kuangukia mtego uleule wa kuchanganya BIASHARA na SIASA, kwenye wimbo wake huo kawasifia wanasiasa tena wa upande mmoja

Diamond bila kufahamu na pengine panic ya Harmonize kujitoa WASAFI na kutoa wimbo fasta huku akitajwa kama mbunge mtarajiwa kwa njia moja kulimuumiza sana Diamond naye akaamua kusifia lakini kwa kufanya hivi kapoteza SEHEMU kubwa ya mashabiki wake

Msanii hapaswi kuwa na upande kwenye mambo ya wanasiasa, Mwanasiasa hana rafiki wa kudumu bali ana maslahi ya kudumu. Msanii anapoamua kuipa kisogo hadhira inayompenda kwa dhati na kuamua kuwageukia wanasiasa..Huyo siku zake zinahesabika.

All in all impact ya jambo hili itaonekana miezi michache ijayo kwa kila upande mwaka 2020 unaweza kuwa mchungu ama mtamu kwa wawili hawa.
 
Hayo ni maneno tu mkuu kama sijakosea diamond alitoa wimbo wa ccm ukiwa kama remix nyingine ya wimbo wake wa number one...Toka kipinde kile alizidi kupaa na kupata tuzo kibao tu, so kwa atakaepoteza zaidi ni konde boy, mond mchezo mzima wa huu mziki anaujua vema.

Kama uko makini na muziki huu ule wimbo wa baba lao ulitoka tu kwa ajili ya kulipa nguvu zaidi tamasha la wasafi, ndo mana wimbo una vitu kibao ambavyo vitafanya watu kuuongelea sana wimbo huo.Mfano wa vitu hivyo ni siasa na ile copy and paste ambayo wengi hawajui kuwa produza na mond waliomba copyrights za wimbo huo toka kwa wahusika wake.

If u know you know....
 
Diamond mwaka 2015 alijihusisha kwenye siasa watu Kama mtoa mada mkasema atashuka kimziki mbona sasa anafanya vizuri zaidi.Baba lao ni hit song na ilitolewa mahususi kwa ajili ya tamasha la wasafi na ndo ngoma iliyoamsha audience kuliko ngoma ya msanii yoyote kwenye tamasha lakini sasa Kila mahali unaolisikia kitaani club pamoja na kwenye harusi lakini pia sasa hiv Ina viewers mil 4.5 YouTube na pia inafanya vizuri kwenye nchi tofautofauti.
 
Hizi nyumbo zao especially Baba lao zinapendwa na generation ambayo haitambui hata siasa ina mchango gani kwao... Hichi kizazi cha 2000s ndo mashabiki wao wakuu na wamejaa mitandaoni hawa madogo ni mazombie mkuu hawana wanachojali
Wewe na mshana ndio ma zombie!
Mashabiki wakubwa wa diamond ni wanawake na ndio majority chochote kitachopendwa na wanawake wewe kikalagosi cha handeni huwezi shindana nacho
 
HAYO NI MANENO TU MKUU KAMA SIJAKOSEA DIAMOND ALITOA WIMBO WA CCM UKIWA KAMA REMIX NYINGINE YA WIMBO WAKE WA NUMBER ONE...TOKA KIPINDE KILE ALIZIDI KUPAA NA KUPATA TUZO KIBAO TU, SO KWA ATAKAEPOTEZA ZAIDI NI KONDE BOY, MOND MCHEZO MZIMA WA HUU MZIKI ANAUJUA VEMA.
KAMA UKO MAKINI NA MUZIKI HUU ULE WIMBO WA BABA LAO ULITOKA TU KWA AJILI YA KULIPA NGUVU ZAIDI TAMASHA LA WASAFI, NDO MANA WIMBO UNA VITU KIBAO AMBAVYO VITAFANYA WATU KUUONGELEA SANA WIMBO HUO.MFANO WA VITU HIVYO NI SIASA NA ILE COPY AND PASTE AMBAYO WENGI HAWAJUI KUWA PRODUZA NA MOND WALIOMBA COPYRIGHTS ZA WIMBO HUO TOKA KWA WAHUSIKA WAKE.
IF U KNOW YOU KNOW....
ULE WIMBO WA BABA LAO ULITOKA TU KWA AJILI YA KULIPA NGUVU ZAIDI TAMASHA LA WASAFI, NDO MANA WIMBO UNA VITU KIBAO AMBAVYO VITAFANYA WATU KUUONGELEA SANA WIMBO HUO.MFANO WA VITU HIVYO NI SIASA NA ILE COPY AND PASTE AMBAYO WENGI HAWAJUI KUWA PRODUZA NA MOND WALIOMBA COPYRIGHTS ZA WIMBO HUO TOKA KWA WAHUSIKA WAKE.
IF U KNOW YOU KNOW.
Yani wewe una akili nyingi sana mwalimu wako wa kwanza kabisa huko aliko anapaswa kujipongeza katengeneza mtu anayefikiri kwa kina na mapana!

God bless you dude!
 
Back
Top Bottom